Pole sana mtani, ila iga busara za Uamsho walipoachiwa huru

Kesi
Bosi Mbowe kesi bado anayo. Yaani ni kama ilivyokuwa kwa Sabaya tu. Sabaya walivyomuachia akasema ataitisha presa conference aseme yote, mhhhh nikajisemea moyoni huyu kaisha. Sasa mshaurini huyu Mwenyekiti wenu wa kikundi cha ngo ajitafakari

Bado kudai katiba mpya Ni kosa la jinai?. Kwamba Mbowe akidai katiba mpya atafunguliwa upya kesi ya igaidi?.

Kesi ikishafutwa haiendelei, Bali DPP atatakiwa kufungua mashtaka tena. Itabidi aanze kesi upya. Halafu mahakama sio kama chooni unaingia na kutoka itabidi DPP aelezee ni kwa nini ameifungua kesi upya?. Kuna Jambo gani jipya ambalo ameliona kwenye kesi ya awali imewafanya aifungue upya.
 
Hawawezi thubutu..kwa mashahidi wao ambao kila saa wanaomba kwenda chooni kuharisha
 
Eti tufanye nchi isitawalike. Wee..!! Unaijua dola wewe!!??? Saivi hali shwari sijaona anayeweza kuleta fyokofyoko..!!

Dola ipi?. hawa mapolisi wanaoua wafanyabiashara wa kitanzania na kuiba pesa zao refer mauaji ya wafanyabiashara was mahenge na juzi mauaji ya mfanya biashaa wa mtwara .

Amani ya Tanzania imehifadhiwa na Mungu na wananchi wa kawaida na sio Viongozi Wala dola.
 
Wapumbavu kama wewe nchi hii bado ni wengi! Wacha wenzako wapiganie haki wewe baki kulamba nyayo za hao unaowaabudu!
Hata Mimi mchunga ng'ombe was huku kazuramimba niliyebahatika kuliona darasa la tatu tu, na mshinda mtazamo kidato Cha SITA wa shule yetu ya kata pale mtaani kwetu. Akina chineembe na sautiyamnyongwa wa chama mbogamboga.
 
DPP ana uwezo wa kuendelea na kesi hata sasa hivi...! Msijidanganye...


Uzi mzuri wa kumfaa Mtani

Please usimdharilishe DPP. Yani afunge ushahidi mapema kabla ya mashahidi 10 waliobakia halafu afute kesi unadhani yeye ni mjinga.

Kumbuka DPP wa sasa ameikuta hii kesi ikiwepo, hivyo ameweza kuona kasoro nyingi ndio maana kasitisha ushahidi wa Jamhuri na baadae kufuta kesi.

Please, mahakama sio chooni unaingia na kutoka Ni sehemu ya heshima. Msiinajisi mahakama Kama mlivyofanya kwenye Bunge. Msiitumie mahakama Kama chombo Cha kuminya haki bali muiache Kama chombo Cha kutoa haki.
 
Hizi propaganda zenu za miaka 20 iliyopita kwanini hamtaki kuzi update?

Kama una ushahidi wa Mbowe kuhusika peleka polisi then muende nao mahakamani.
Ndio sasa uone maajabu ya ccm! Kumbe walikuwa na kesi nzuri hivi kabatin halafu wakatunga ile ya michongo! Daah! Maana hyo ya chacha kulikuwa na mtu amekufa kweli! Hii nyingine vituo vya mafuta vililipuliwa kwenye kidaftari cha "msomi"
 
Yaani Mbowe alifunguliwa mashtaka ya ugaidi kwa vile anadai katiba mpya? Kweli ujinga nchi hii umekithiri.
 
Walikaa jela wakina mandela na bado maisha yakasongo, kuna mtu alikuwa jeuri na kiburi kama jiwe? Leo hii yuko wapi?
 
magufuri seremaaa
 
Ana haki ya kuongea yote na kuwashukuru wote walionyesha utu kwake ni haki yake. Yule asiye na shukrani kwa walionyesha utu wakati wa shida huyo ni sawa na punda tu. Ni shetani tu anayefurahia shida ya mtu mwingine
Kama ni kushukuru waliomwonea huruma angetangulia kumshukuru rais Samia ambaye pamoja na mahakama kumwona ana kesi ya kujibu aliamua kuingilia kati na kupitia DPP akaifuta kesi. Wa pili angekuwa shehe mkuu aliyetamka bila kupepesa macho na KUMWOMBA sio kushauri kwamba rais aifute kesi ya Mbowe na wenzake.
 
Yaani hiyo kuachiwa kwa dpp kutokua na nia kuendeleza mashtaka anaweza kamatwa tena na kesi kuendelea ilipoishia.
Huyu alishapata ugonjwa wa urais. Ana behave presidential wakati sio president. Ugonjwa huu pia wanayo wagombea ccm waliyoshindwa kuteuliwa. Kuna january makamba na madilu na yule alikua waziri wa nje. Na ndio maana mbowe anajiona kama rais mbadala na kuongoza chadema kibabe kama mali yake binafsi.
Ukigombea urais ukashindwa haijalishi kwenye hatua gani tatizo unaweza kupata ugonjwa wa urais.
 
Naona unasumbuliwa na bawasilia dalili zake ni kuwashwawashwa inatibika njo dm mtoa post nikupe dawa ugonjwa huu unadharirisha sans
 
Uamsho? Hujui nyuma yake nyamaza kimya.
 
Aachana na siasa mbowe ,nimzee kivipi mtu Yuko imara kiasi hicho,. Kawagusa ukingo wa utumbo mpana mnalo hilo
 
Hujui sheria, DPP atasema anaonesha nia ya kuendelea na kesi
 
aisee
Kwanza, napinga yote uliyoandika!

Pili, AKILI si nywele! Wengi wana nywele lakini hamnazo!
aise?hata mimi nataka nimpinge tu huyu jamaa lakini sina hoja,hebu weka hoja timpinge pamoja bhana,haiwezekani jamaa liongee kwa hoja hivi halafu tumpinge bila kuweka hata hoja za kuzugia!
 
aisee
aise?hata mimi nataka nimpinge tu huyu jamaa lakini sina hoja,hebu weka hoja timpinge pamoja bhana,haiwezekani jamaa liongee kwa hoja hivi halafu tumpinge bila kuweka hata hoja za kuzugia!
Hoja ya kwanza... huwezi kulinganisha Uamsho na Mbowe.
Hoja ya pili... yawezekana changamoto za Uamsho ziliisha walipotoka kizuizini.
Hoja ya tatu... changamoto anazosimamia Mbowe bado ni endelevu.
Hoja ya nne... Uamsho hawakuwa threat kwa serikali na ccm
Hoja ya tano... Nchi yetu haina dini. Uamsho ni kikundi cha kidini.
Hoja ya sita... Mbowe anasimamia hoja jumuishi na mtambuka
Hoja ya saba... Hivi kesi ya Uamsho nayo iliaanika serikali??
Hoja ya nane... Ni upofu kumwambia mwanasiasa akae kimya wakati yeye, wananchi na wanasiasa wenzake wanajua nguvu yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…