Pole Sheikh Yahya....!

Pole Sheikh Yahya....!

yap mpeni pole
icon7.gif
 
Mbona kuna watabiri wengi hatujadili utabiri wao, kwanini yeye tu ndo anapewa coverage kubwa sana tena front page , kuna mawili hao wanaompa coverage nao ni washirikina au ndo kazi ya usalama kutufanya kujadili uchawi na kuacha mambo mengi sana ambyo ni consructive na productive,tusijadili utabiri wake, tujadili KWANINI tunajadili utabiri wake ndo tutapata jibu muafaka.
 
kilichojificha hakijadiliwi,,,,....bali kionekanacho,,
hekima hufunika ukaidi,,,
bali kioo cha mpumbavu ni matendo mbele hadhira
 
amejivisha utukufu,
bila kujijua ni mfu,
na mawazo ya hofu,
kwa kutufanya vipofu.

na imani za kuzimu,
naye ataka zidumu,
yafaa kumshutumu,
kuupinga wake wazimu.

si mtu wa kumsikiliza,
bali wa kumkimbiza,
kumwandalia baraza,
na viboko kumcharaza.

ni mfuasi wa shetani,
na tena ni hayawani,
kwa yake ya firauni,
tabia iso kifani.
 
hongera mtunzi wa shairi. ujumbe umefika
 
utabiri tu bana hana lolote. hard disk yake ilikwisha kufa siku nyingi, na atashije mjini pasi kuwadanganya na kuwatia hofu wasomi ili apate chakula yake na familia?

Daaah Ngoshwe unaroho ngumu, mtabiri atakushukia, huko Pangoni mwako kwa njia za kijini, hahaaaa Shehe Yahya, uchawi wako si mali kitu, duuuh pole, amua kumcha Mungu wako.
 
Ugali unatafutwa kwa njia mbalimbali, anajitahidi naye ili ale.
 
lakini ni shehe wa waislamu jamani, tusije kuwa tunawakwaza jamaa zetu
 
Uislamu kamwe haukubali ushirikina! Mtu kama mtu atambulike kwa zake tabia na wala asihusishwe na usilamu. Sheikh Yahaya hebu usiupake matope uislamu.
 
Sheikh Yahaya hebu usiupake matope uislamu.
kuna kila sababu ya kuuchunguza uislamu kwanza kabla hatujaanza kumshambulia yahya kama nu kweli anaupaka
matope ama, laikini nijuacho mimi uislamu ueandaa aya nyuingi
zitumiwa kama albadili kuwadhuru watu, sasa hapa ninahitaji kueleweshwa kidogo kwa upande huu, hasa ukizingiti
Mfano maadili ya Bilblia ni kuwasamehe na kuwaombea wanaotuudhi, sasa huo wa kusoma albadili siyo ushirikana?
 
Mimi nauhakika uislam kama uislam kama zilivyo dini nyingi tu inasisitiza maadili mema na kumcha Mungu, uislam unasisistiza elimu na unasisitiza upendo baina ya jamii ndio maana neno ISLAM kwa maana yake halisi lina maana ya UNYENYEKEVU ikiwa na maana ya kumnyenyekea Muumba wa mbingu na ardhi yaani MUNGU. Ndio ni kweli hata mimi nilisha sikia mara nyingi tu watu ( hasa Waislamu) wakitishia kuwadhuru wengine kwa kusoma hiyo Al-Badr. kwa ufahamu wangu ( Waislam watanikosoa) Badr ni moja kati ya vita nyingi alizopigana Muhamad na waislam wa mwanzo katika kuulinda na kuutetea uislam. So mtu anapoomba dua ya kumdhuru mtu kwa kutumia Al- badr kimsingi anaomba dua ya kumdhuru mtu kwa kutumia damu ya watakatifu waliokufa katika viat hiyo. Ki ukweli kama mtu hana hatia dua ya al-badr haiwezi mdhuru mtu hata kama muombaji atakesha uchi akioomba hakuna kitu, ni sawa Wakristoi eti mtu akutishe kukudhuru kwa kuomba dua kutumia watakatifu kama say wale mashahidi wa uganda! So mimi naamini Al- badr haimdhuru mtu,. Ila tu nikubakiane na wachangiaji wengine, watu wengine ( kama Yahaya) na wenzio wakati mwingine hutumia tu kivuli cha dini na kutumia maandishi yafanaanyo na Koran kuwalaghai wasiojua, maana ni kweli wengi wetu ahtuwezi tofautisha koran na kiarabu lakini ki ukweli ni vitu viwili tofauti!. uislam unapiga sana vita ushirikina wa aina zote ikiwemo kupiga bao kama afanyao Yahya, So let us be fair tuhukumu utabiri wa Yahya kama Yahya na wala tusitumie utabiri to condamn the Islam simply because we are not Muslims!
 
Oh! Mbuzi ashakuwa mjuzi,
kwa wingi wa ufukunyuzi,
Azikuna zote nazi wapata shida wajuzi,
Haya sie tulo wagunduzi hayo mambo ya kiugunduzi,
Kaziye ni utambuzi siye yetu uchakuzi,
Aseme yote kiupanuzi na hata yo ya uchaguzi,
Keshaanza dahari mamboye alibashiri na ufafanuzi,
Wazamaji na wafike wa matopeni wapige mbizi,
Bakuli zetu ziijadili na mwishowe zitwae utambuzi,
Yu mkweli Yahaya kwa wake Ubaya, au wapo wa haya wanotutia ukengeuzi,
Tupae na tulonayo mabawa na wavae walonayo mavazi,
Ionekane ilofanywa kwetu, tumbaini alo mpuuzi.
Dunia yetu ni wazi na ubinadamu u kazi'
Amani Kwenu Wazazi'
 
Back
Top Bottom