Poleni Sana DC na DED Mliotimuliwa: Kesho Watoto wenu wataenda Shule kama watoto wa Mwananchi wa Kawaida

busar

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
1,071
Reaction score
1,067
Nimewaza mengi na kuwaonea huruma. Lkn Cheo ni Dhamana, iwe ulihongwa au ulikipata kwa sifa za kiutendaji, ni DHAMANA

Inawezekana yako mengi katika yaliyofanya hawa watu watimuliwe, lkn Mh. Rais katika maongezi yake liko jambo kubwa kalisema ambalo ndio hasa limeshababisha WANA CCM KURUDISHA KADI ZAO CHAMANI, jambo lenyewe ni HONGO ILIYOPELEKEA KUHAMISHA MRADI KUTOKA ULIPOTAKIWA KUWA NA KUPELEKWA MAHALA PENGINE.

Kimsingi Rais amewatoa kwa sababu za Utovu wa NIDHAMU NA RUSHWA. je ni lini watapelekwa mahakamani?

Huzuni yangu kubwa ni stress ndani ya familia. Waza tu unapata taarifa ya kufukuzwa kazi kwenye watsap group ya MADC wenzako, Classmates wenzako, au group la mtaaani kwako. Usipokuwa makini unaweza kumchukia alieitupia badala ya alie kutengua.

Ushauri, tukiwa na nafasi za kisiasa tuziweke mbali familia zetu. DCs na DEDs mkiteuliwa msihamie na familia zenu kwenye vituo vya kazi. Nendeni wenyewe, mtaziponya na masimango na Huzuni.
 
Safi sana
 
DC amwache mke wake mjini?
 
hizo ndo kazi za kisiasa serikalini maana muda wowote inayeyuka
 
Dogo, siku hizi baadhi ya misemo ya Kiswahili imebadirika. Mfano ule usemao, "Aliyeko juu mngoje chini". Siku hizi tunasema, "Aliyeko juu, mfuate hukohuko"! Ukijifanya unamsubiri chini, utamsubiri hadi Yesu akukute hapo atakaporudi mara ya pili! Ahahahahaha!!!
 
Nimpe big up Mh Rais kwa maamuzi hayo mazuri,DC huyo mpuuzi sana kazingua sana toka akiwa Uvinza hata kusababisha vifo na migogoro mikubwa kati ya wakulima na wafugaji yeye alikuwa anataka chake tu na apekuliwe ac zake
 
Dhamana
 
Au sijui ile "haraka haraka haina baraka", sasa imagine una mgonjwa mahututi kwenye gari halafu utembee kindezi kwasababu wahenga walikaa enzi hizo wakasema haraka haraka haina baraka? [emoji3]

Baadhi ya misemo, nahau na methali zimepitwa na wakati.
 
Zinabadirika kwendana na wakati! Ahahahahaha!!
 
Ubaguzi mbaya sana katika dunia hii. Unakaa na kiburi cha uteuzi baadaye unatumbuliwa
 
Huzuni yangu kubwa ni stress ndani ya familia. Waza tu unapata taarifa ya kufukuzwa kazi kwenye watsap group ya MADC wenzako, Classmates wenzako, au group la mtaaani kwako. Usipokuwa makini unaweza kumchukia alieitupia badala ya alie kutengua.
Fikiria stress walizopata wananchi waliohujumiwa kwa hiyo rushwa
 
"Ushauri, tukiwa na nafasi za kisiasa tuziweke mbali familia zetu. DCs na DEDs mkiteuliwa msihamie na familia zenu kwenye vituo vya kazi. Nendeni wenyewe, mtaziponya na masimango na Huzuni."

Hapo umeongea point kubwa sana
 
Hayo ni mambo ya DP World tu mambo ya kuhamisha miradi hayawezi kumfanya mwananchi arudishe card za chama,2025 mama anayo kazi tena kubwa
 
Hayo ni mambo ya DP World tu mambo ya kuhamisha miradi hayawezi kumfanya mwananchi arudishe card za chama,2025 mama anayo kazi tena kubwa
Wanaitwaje Majina yao. Isijekuwa ni wanajumuia na wameuunga mkono TEC
 
DED ni permanent and pensionable!

Anaondoka na LSSE 3,400,000/= aliyokuwa nayo kuelekea RS mtwara au utumishi watakakompangia kuingana na taaluma yake.

Kimbembe ni Kwa DC, atapewa 40% ya mishahara yake yote kama pension Kisha wanatemana nae, kama alikuwa mtumishi wa umma kabla ya udc atenda kuomba kuresume alikotoka kama kutakuwa na nafasi.

Kufanya kazi serikalini ni uhakika wa kustaafu.

Kutumbuliwa ni uhamisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…