Poleni sana wapambanaji mlio mstari wa mbele kupigania UKOMBOZI wa Nchi hii.

Poleni sana wapambanaji mlio mstari wa mbele kupigania UKOMBOZI wa Nchi hii.

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
667
Reaction score
1,403
Naomba tusikate tamaa, kwa hali ilivyo sasa, inaonekana wamepanga kumsimika madarakani si kwa kuchaguliwa bali kwa nguvu, yaani iwe kwa kuumiza watu au kwa namna yoyote ile. Kwa hali hii, nadhani sasa kuna haja ya kupanga mikakati na njia mpya kabisa za kutafuta HAKI katika Taifa hili.

Kama mababu zetu pamoja na uduni wa wakati ule lakini walithubutu kupambana na wakoloni kudai Uhuru, itakuwaje sisi wa enzi hizi za sayansi na Teknolojia tushindwe kupigania HAKI?

Kwa hatua ya sasa, nadhani viongozi wetu wa mapambano wakutane na wapenda haki wengine wakiwemo viongozi wetu wa Dini, Taasisi za kimataifa na za kikanda, Mashirika mbalimbali, Mabalozi nk. ili kutathmini hali hii na kupendekeza njia mbadala ya mapambano.

Mungu yupo pamoja na Watanzania.
Tusikate tamaa. Ni dhambi kubwa kukata tamaa.
 
Back
Top Bottom