Poleni Wapinzani Tanzania, tambueni na myatafakari yafuatayo

Unakosea sana kwa kuangalia hilo la maccm kuhamia upinzani kama ni tatizo kubwa sana.

Upinzani unashindwa kuitoa ccm madarakani kwa sababu uchaguzi si HURU na wala si wa HAKI.

Maccm hawataki TUME HURU kwa kuwa wanajua uchaguzi HURU na wa HAKI ndiyo kiama chao. Hivyo wanatumia VITISHO, ULAGHAI na MTUTU WA BUNDUKI ili kung’ang’ania madarakani.

Unaweza kuniambia Sheikh Ponda alisema neno lipi la UCHOCHEZI hadi astahili kukamatwa!?

1594917869530.jpeg

Kwa kutazama filamu ya kiuchaguzi inayoendelea hivi sasa, ninaishiwa maneno ya kuzungumza. Lakini, kwakuwa JF ni a house of great thinkers, chukueni yafuatayo ili mchanganye na zenu kuelekea Oktoba 2020:
1. Kila katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, CCM lazima 'imuondoe' kada wake mmoja kindakindaki ili ajiunge na 'upinzani'.
2. Kila kwenye uchaguzi mkuu wa vyama vingi, CCM hujitahidi kuhakikisha kuwa ina mgombea zaidi ya mmoja kwenye Urais na Ubunge ili kuzigawa kura za upinzani.
3. Kila mwaka wa uchaguzi, CCM, katika umakini na utaalamu wa hali ya juu, hukikuza chama kimoja kuwa 'tishio' cha upinzani ili kubadili upepo wa kisiasa.
4. Mrema, Lowassa na Membe wanahusika na 1 na 2 hapo juu.
5. NCCR-Mageuzi, CHADEMA na ACT-Wazalendo wanahusika na 3 hapo juu.
6. Hapa Tanzania, wapo wapinzani kweli na wapinzani 'feki'. Wapinzani feki ni wengi zaidi ya wale wa ukweli.
7. Zitto yupo kwa kazi maalum kwa manufaa ya CCM katika kila uchaguzi mkuu kuanzia 2000.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha, Tanzania)
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👊🏽👊🏽👊🏽

Dhana nzima ni potofu.

Sikubaliani nayo.

1. Mrema alitaka kuwa Rais wa nchi hii kikwelikweli sio kwa maigizo, pamoja na kwamba uwezo hana.

2. Lowassa, bila shaka yoyote ile alijua ndiye atakayekuwa Rais wa Tanzania 2015, hadi alipokatwa. Kwa kuamini kwamba anao wafuasi wengi nyuma yake, akatafuta chombo cha kumfikisha kwenye urais. Kwa bahati mbaya kajikuta mamluki waliokuwa wakimhadaa angali CCM hawakuwa tayari kuachia vitumbua vyao. Wakamtosa.

3. Membe alipania kumpinga Magufuli, sio kwa maigizo, bali kiuhalisia kwa jinsi Magufuli alivyopavuruga huko ndani ya CCM. Akategeshewa aende kutubu na kuomba msamaha, hakwenda.

Lakini katika yote hayo niliyoweka hapo juu, wote watatu, Mrema, Lowassa, Membe hakuna mmoja kati yao aliyeonyesha dhamira ya kweli ya kuchukizwa na yanayofanyika ndani ya chama chao CCM.
Wote watatu, msukumo wao ni kushika cheo cha urais bila kujali watakifanyia nini wakishakishika.
Hawakuwashawishi wananchi waone utofauti wao na chama wanachokiacha nyuma.

Kwa hiyo ni dhana potofu kufikiri kwamba CCM inafanya mipango hii maksudi kuwazuia wapinzani kushika madaraka. Uwezo huo CCM hawana.

Kwa sasa sitachambua upotofu wa CHADEMA na vyama vingine katika kudhani kwao kwamba ujio wa watu hao ndiyo itakuwa nafuu kwao.
 
Unadhungumzia dhuluma nchi gani we fisadi wa fitina. Unakaa unapumua sehemu Zote na bado unadai dhuluma. Unasafiri. Unakula. Unaj hapa JF. Nk. Punguzeni upumbavu watanzania wenzangu. Kila mtu mwanasiasa how.
Tujifunze tu Kenya, huwezi pata hata shamba achilia mbali kiwanja. Wakati Tz unalima na kujenga popote. Tunasahau kuwa ni msingi uliojengwa na serikali tunayosema ni ya kidikteta. Watanzania tunafanya maigizo ya yule mchunga mbuzi aliyeita chui! chui wakati hakuna chui. Siku alipokuja chui kweli hata alipoita watu wakasema ni utani.
Tuikosoe serikali yetu na kuielekeza kwa heshima badala ya kejeli na dharau. Wazungu wanaohubiri demokrasia duniani, ikifika suala la nchi yao, hawako tayari kuidharau nchi yao hata kidogo. Sisi tunadiriki kusema nchi ya hovyo. Si uhame nenda huku kwenye nchi nzuri.
 
Tuikosoe serikali yetu na kuielekeza kwa heshima badala ya kejeli na dharau. Wazungu wanaohubiri demokrasia duniani, ikifika suala la nchi yao, hawako tayari kuidharau nchi yao hata kidogo. Sisi tunadiriki kusema nchi ya hovyo. Si uhame nenda huku kwenye nchi nzuri
Unaona unavyochanganya mambo?
Magufuli sio nchi, unalielewa hilo au wewe ni kilaza?

Nimeona nikusitue tu kwa hili, hayo mengine juu pia inaonekana huelewi chochote; unajpigia tu bila mpangilio.
 
Kajisemea Askofu Bagonza Mkuu, “Tulipokuwa na Chuo Kikuu kimoja Nchini hatukuwa na wajinga wengi kama ilivyo sasa ambapo tuna vyuo vikuu vingi.”

Unaona unavyochanganya mambo?
Magufuli sio nchi, unalielewa hilo au wewe ni kilaza?

Nimeona nikusitue tu kwa hili, hayo mengine juu pia inaonekana huelewi chochote; unajpigia tu bila mpangilio.
 
Unakosea sana kwa kuangalia hilo la maccm kuhamia upinzani kama ni tatizo kubwa sana.

Upinzani unashindwa kuitoa ccm madarakani kwa sababu uchaguzi si HURU na wala si wa HAKI.

Maccm hawataki TUME HURU kwa kuwa wanajua uchaguzi HURU na wa HAKI ndiyo kiama chao. Hivyo wanatumia VITISHO, ULAGHAI na MTUTU WA BUNDUKI ili kung’ang’ania madarakani.

Unaweza kuniambia Sheikh Ponda alisema neno lipi la UCHOCHEZI hadi astahili kukamatwa!?

View attachment 1508723
Mkapa aliwahi kuyasema haya; tena kiuwazi hivyo?

Kuna 'audio' yake kuhusu maneno haya?

Kama ni kweli, nampa heshima yake kuhusu hili.

Kwa nini vyama vya upinzani wasitengeneze bango la kuwafikishia ujumbe wananchi popote nchini wakati huu wa kampeni kuelekea kwenye uchaguzi.
Itakuwa rahisi wananchi kuuelewa ujumbe kuliko wao kulipigia tu kelele kiholela.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hapo kwenye namba 7 umesahau kumuweka na Mbowe
Kwa kutazama filamu ya kiuchaguzi inayoendelea hivi sasa, ninaishiwa maneno ya kuzungumza. Lakini, kwakuwa JF ni a house of great thinkers, chukueni yafuatayo ili mchanganye na zenu kuelekea Oktoba 2020:
1. Kila katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, CCM lazima 'imuondoe' kada wake mmoja kindakindaki ili ajiunge na 'upinzani'.
2. Kila kwenye uchaguzi mkuu wa vyama vingi, CCM hujitahidi kuhakikisha kuwa ina mgombea zaidi ya mmoja kwenye Urais na Ubunge ili kuzigawa kura za upinzani.
3. Kila mwaka wa uchaguzi, CCM, katika umakini na utaalamu wa hali ya juu, hukikuza chama kimoja kuwa 'tishio' cha upinzani ili kubadili upepo wa kisiasa.
4. Mrema, Lowassa na Membe wanahusika na 1 na 2 hapo juu.
5. NCCR-Mageuzi, CHADEMA na ACT-Wazalendo wanahusika na 3 hapo juu.
6. Hapa Tanzania, wapo wapinzani kweli na wapinzani 'feki'. Wapinzani feki ni wengi zaidi ya wale wa ukweli.
7. Zitto yupo kwa kazi maalum kwa manufaa ya CCM katika kila uchaguzi mkuu kuanzia 2000.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha, Tanzania)
 
Kwa kutazama filamu ya kiuchaguzi inayoendelea hivi sasa, ninaishiwa maneno ya kuzungumza. Lakini, kwakuwa JF ni a house of great thinkers, chukueni yafuatayo ili mchanganye na zenu kuelekea Oktoba 2020:
1. Kila katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, CCM lazima 'imuondoe' kada wake mmoja kindakindaki ili ajiunge na 'upinzani'.
2. Kila kwenye uchaguzi mkuu wa vyama vingi, CCM hujitahidi kuhakikisha kuwa ina mgombea zaidi ya mmoja kwenye Urais na Ubunge ili kuzigawa kura za upinzani.
3. Kila mwaka wa uchaguzi, CCM, katika umakini na utaalamu wa hali ya juu, hukikuza chama kimoja kuwa 'tishio' cha upinzani ili kubadili upepo wa kisiasa.
4. Mrema, Lowassa na Membe wanahusika na 1 na 2 hapo juu.
5. NCCR-Mageuzi, CHADEMA na ACT-Wazalendo wanahusika na 3 hapo juu.
6. Hapa Tanzania, wapo wapinzani kweli na wapinzani 'feki'. Wapinzani feki ni wengi zaidi ya wale wa ukweli.
7. Zitto yupo kwa kazi maalum kwa manufaa ya CCM katika kila uchaguzi mkuu kuanzia 2000.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha, Tanzania)
Mzee TUPATUPA naona umeanza kuchanganyikiwa!
 
Hayajifunzi haya majitu! Wacha yamchukue Membe lakini mimi nasema hawapati hata wabunge 10, hana umaarufu huo! He is overrated. Yanakuja tena kugawa kura za wapinzani, maana yatataka kusimamisha wagombe kila jimbo! Zitto ana tamaa sana
 
Mkapa aliwahi kuyasema haya; tena kiuwazi hivyo?

Kuna 'audio' yake kuhusu maneno haya?

Kama ni kweli, nampa heshima yake kuhusu hili.

Kwa nini vyama vya upinzani wasitengeneze bango la kuwafikishia ujumbe wananchi popote nchini wakati huu wa kampeni kuelekea kwenye uchaguzi.
Itakuwa rahisi wananchi kuuelewa ujumbe kuliko wao kulipigia tu kelele kiholela.
Mkapa Kayaandika kwenye kitabu chake kitafute ukisome, pia nazani kuna mdau humu alikifanyia uchambuzi wake humu.
 
Unadhungumzia dhuluma nchi gani we fisadi wa fitina. Unakaa unapumua sehemu Zote na bado unadai dhuluma. Unasafiri. Unakula. Unaj hapa JF. Nk. Punguzeni upumbavu watanzania wenzangu. Kila mtu mwanasiasa how.
Acha Mkuu, upuuzi wa wanasiasa wa leo unaathiri pakubwa maisha ya kila mwananchi.
 
Wenye maamuzi ni wananchi na bado hawajaamua kuamua!! Yawezekana iko siku "ghushi" ikawa halisi na "halisi" ikawa ghushi!!
 
Unakosea sana kwa kuangalia hilo la maccm kuhamia upinzani kama ni tatizo kubwa sana.

Upinzani unashindwa kuitoa ccm madarakani kwa sababu uchaguzi si HURU na wala si wa HAKI.

Maccm hawataki TUME HURU kwa kuwa wanajua uchaguzi HURU na wa HAKI ndiyo kiama chao. Hivyo wanatumia VITISHO, ULAGHAI na MTUTU WA BUNDUKI ili kung’ang’ania madarakani.

Unaweza kuniambia Sheikh Ponda alisema neno lipi la UCHOCHEZI hadi astahili kukamatwa!?

View attachment 1508723
Hakika hakika Mkuu! Je ni kwanini haitakiCCM wagombea binafsi kama katiba inavyosema "haki ya kuchagua na kuchaguliwa?"
TUME HURU... KATIBA MPYA... UMOJA WA KITAIFA
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mkuu ni UHUNI na UDIKTETA unaoendelezwa na hili genge la wahuni wa ccm. Dikteta hakuwa na madaraka yoyote yale 2015 kuwazuia wapinzani kufanya shughuli zao kwa miaka mitano. Katika kipindi hicho cha miaka mitano ametumia boba ya madaraka yake kuwanyanyasa wapinzani kwa kila namna ikiwemo kuwateka, kuwakamata, kuwabambikia kesi, kuwa shambulizi na hata kuwaua.

2020 inafika uhuni na udikteta ule ule waliofanyiwa kwa miaka mitano bado unaendelea dhidi ya wapinzani huku akiwa hataki kuisikia tume huru ili aendelee kuiba chaguzi za Wabunge na Rais.

#TUMEHURU2020 #KATIBAMPYA2020

Hakika hakika Mkuu! Je ni kwanini haitakiCCM wagombea binafsi kama katiba inavyosema "haki ya kuchagua na kuchaguliwa?"
TUME HURU... KATIBA MPYA... UMOJA WA KITAIFA
 
Pesa ya lowasa ale mbowe, lawama abebe zito!
Kama unaamini Lowassa alitoa pesa kwa Mbowe basi unadhibitisha ni Lowassa ni mtoa Rushwa.
Na kama Lowassa ni mtoa Rushwa na ulisikiliza hotuba ya Rais akimsifu siku ile pale Lumumba nje akimpokea Lowassa basi ni wazi #1 aangaliwe vizuri kwani kuna usemi 'ndege wa aina moja huruka pamoja'.
Jee naye ni mla Rushwa na mtoa Rushwa?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kayasema November, 2019 Mkuu. Ngonja nitaitafuta audio yake kama ipo. Wazo lako la kuitengenezea bango ni zuri sana.

Mkapa hatimaye kaona mwelekeo wa Nchi si mzuri na kinachoweza kubadili mwelekeo huu mbaya wa Nchi ni kuwepo uchaguzi huru na wa haki kupitia Tume huru.

Huyu aliyewahi kuwaita wapinzani MALOFA 2015 mpaka kaamua kutoa kauli hii basi kaangalia mbali sana kuhusu hatima ya Nchi na huyu dikteta akiwa madarakani.

Back
Top Bottom