GE2025 Polepole amshauri Rais Samia asichukue fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2025

GE2025 Polepole amshauri Rais Samia asichukue fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwamba anataka ccm iondoke madarakani.hajasema Samia asipoenda kuchukua fomu alafu nini kinafuata
 
Kada wa chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole hii leo Agosti 08, 2025 amemsihi Rais Samia Suluhu kutochukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akihoji anataka kwenda kushindana na Salum Mwalimu wa CHAUMMA,

"Unataka ukagombee na Salumu Mwalimu wa CHAUMMA ndio unapata amani ya moyo, unapata amani ya moyo kabisa, unapata amani ya moyo kabisa ukagombee na Luhaga Mpina wa ACT Wazalendo, kweli?" - Humphrey Polepole, Kada wa CCM.
Mbona Yeye hakumshauri mwendazake asichukue fomu wakati anashindana na Braza K
 
Mnaweza mkamlaumu mama,kumbe naye anapewa maelekezo na mfumo nini afanye.Viapo vinabeba mambo mengi,kwani mfano asipogombea inadhaniwa nini atapungukiwa maana kama ni malipo ataendelea kupata pamoja na stahki zake nyingine.Tatizo ukute ni wale ambao wapo kwenye nafasi za uteuzi,wanajiuliza akija mwingine si atateua wengine,na wao wasugue benchi kama akina Kalemagi na wengine?
They have their future plans.
Kwaiyo sirmia ni kasuku?
 
Mbona Yeye hakumshauri mwendazake asichukue fomu wakati anashindana na Braza K
Hadi kwa maelezo haya hujui Polepole anaongelea nini?

Kwa kukusaidia unajua chanzo cha Lowassa kuamia UKAWA? ukishajua tuendelee
 
Hadi kwa maelezo haya hujui Polepole anaongelea nini?

Kwa kukusaidia unajua chanzo cha Lowassa kuamia UKAWA? ukishajua tuendelee
Wewe hujui chochote kuhusu huyo. Huyo ni mmoja wa watu makatili sana. Anaongea uzushi wake kwa kutetea kundi lake ambalo ndoto zao za kutoa Rais zimezimwa. Yeye anatekeleza ajenda yao bora tukose wote na ili kupata uungwaji mkono wa nyumbu ndio maana anaingiza na ajenda za Lissu.(Mtu ambaye alipopigwa risasi alikuwa mstari wa mbele kumuita kibaraka anayetumika na mabeberu). Ndio maana watu kama Lema wako skeptical.
 
Sawa wewe ndio unajua
 
Kada wa chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole hii leo Agosti 08, 2025 amemsihi Rais Samia Suluhu kutochukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akihoji anataka kwenda kushindana na Salum Mwalimu wa CHAUMMA,

"Unataka ukagombee na Salumu Mwalimu wa CHAUMMA ndio unapata amani ya moyo, unapata amani ya moyo kabisa, unapata amani ya moyo kabisa ukagombee na Luhaga Mpina wa ACT Wazalendo, kweli?" - Humphrey Polepole, Kada wa CCM.
Nini unataka?
CCM isitowe mpinzani au imuweke nani mwenye kaliba ya hawo ulowataja.
Wagombea wote sawa hakuna cha ajabu hapo.

Kwenye ligi hakuna timu dhaifu madhali imo kwenye ligi basi utacheza nayo tuu.
 
Nilikuwa napenda kulitumia neno la kujizima data Polepole kanikumbusha kuhusu kushupaza shingo
 
Hii nadhani imeisha.

Sipati picha 2029 vita vya uraisi.
 
jana wamama wa sokoni wanaulizana spika msaafu hata barabara ya kwenda kwake Ina vumbi alikua anafanya nini miaka yote ya ubunge na uspika..
Ingekuwa imepigwa lami wangesema tena spika alikuwa fisadi, kapendelea barabara ya kwenda kwake.
 
Kada wa chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole hii leo Agosti 08, 2025 amemsihi Rais Samia Suluhu kutochukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akihoji anataka kwenda kushindana na Salum Mwalimu wa CHAUMMA,

"Unataka ukagombee na Salumu Mwalimu wa CHAUMMA ndio unapata amani ya moyo, unapata amani ya moyo kabisa, unapata amani ya moyo kabisa ukagombee na Luhaga Mpina wa ACT Wazalendo, kweli?" - Humphrey Polepole, Kada wa CCM.
😂😂😂😂😂😂😂😆😆😂😂😂😁😁😁🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
KWAKO ALBERT MSANDO

Ninavyojua Albert Msando ni Mwanasheria (Wakili), aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya nafasi anayoitumikia hadi sasa.
Kwenye taaluma ya sheria huwa kuna viapo ambavyo ukishaapa basi baadhi ya mambo inakubidi uachane nayo ili kulinda heshima ya taaluma, kwa mfano uongo, kisheria uongo ni kosa la jinai.
Sasa sielewi ukishakuwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa, nafasi ambayo ni ya kisiasa kwamba inakubidi uachane na viapo vya awali ambavyo ni vya kitaaluma kisha ukubali kutumikia siasa za uzushi, fitina na kubagazana, upambe na uchawa tunaoushuhudia ndani ya CCM.
Sijui, lakini pia siamini kama ndivyo.

Msando amemuomba Humphrey Polepole wajadili kuhusu katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ibara ya 100(2) inayotamka kwamba "Mkutano Mkuu wa CCM Taifa utakuwa ndio kikao kikuu kupita vyote na ndicho kitakachokuwa na madaraka ya mwisho."

Ni kweli kwamba mkutano mkuu wa taifa ndiyo mkutano mkuu na wenye mamlaka ya mwisho kama ilivyotajwa kwenye ibara hiyo.
Lakini asichokijua Msando "Wakili" huyu au DC huyu, labda kajitoa ufahamu sijui, ni kwamba mkutano mkuu uliomteua na kumchagua Samia ni mkutano mkuu "MAALUMU" tu.
Hivyo inapokuwa kitu kinaitwa "maalumu" maana yake ni cha dhalura, kwa ajili tu ya jambo fulani kama ilivyofanyika kwenye mkutano huo kwani ulikuwa maalumu tu kwa ajili ya kujaza nafasi ya makamo mwenyekiti wa CCM.

Kwa hiyo, mkutano huo haukuwa na jukumu la kuchagua mgombea u-Rais kwa sababu mkutano mkuu wa kuchagua mgombea u-Rais hutangazwa kufanyika baada ya wagombea kuchujwa ktk ngazi ya vikao zaidi ya viwili kabla ya kufikia ngazi mkutano mkuu.
Ina maana Msando na uwakili wake hakuliona wala kujiuliza hivi? Au kaamua kama ilivyo kwa wengine kujichetua na kujitoa ufahamu, kuweka pembeni taaluma na kuwa mpambe asiyetumia hata akili za kawaida tu!?🤦🏻‍♂️

Pili, Albert Msando anahoji kupitia "Ibara ya 14(2) juu ya Haki ya Mwanachama kuhudhuria na kutoa maoni yake katika Mikutano ya CCM pale ambapo anahusika kwa mujibu wa Katiba."
Hoja hii inalenga kuhalalisha wale waliotumwa kutoa hoja ya kuhalalisha Samia awe mgombea u-Rais bila kupitia mchakato wa ndani ya chama.
Hata hili Msando hakujiuliza ni kwa nini licha ya katiba ya nchi kutoa uhuru wa maoni usio na mipaka, lakini sheria ya nchi imedhibiti uhuru huo?
Sisi ndani ya chama chetu pia tuna katiba, kanuni na taratibu pia, kilichofanyika ktk mkutano ule ni udikteta wa kukanyaga misingi ya chama chetu, na ndiyo maana wanachama ambao hawako tayari kuona ukiukwaji huo wamehoji uhalali na kutaka mchakato uanze mpya.

Haya nametokea si kwa bahati mbaya, ni kwa makusudi na ni matokeo ya unafiki na ukimya wa wanachama kuyakalia kimya maonezi wanaofanyiwa wanasiasa wengine nchini na ndani ya chama.
Tulipowaona wapinzani wakisurubiwa tulidhani na kuamini kuwa "Hao si wenzetu ktk chama".
Lakini yametugeukia ndani ya chama, wapo walioshtukia lakini wengi wa wanachama wamebaki kimya kutokana na sababu mbalimbali na moja ya sababu hizo ni unafiki.

Kuna mwanasiasa mmoja wa chama cha upinzani aliwahi kusema, "mkitumaliza kutushughulikia sisi wapinzani, mtarudi kushughulikiana wenyewe" na hamtakuwa na wa kuwatetea.
Mama alipoanza kuwashughulikia wale jamaa hatukujali kwani tuliwaona si wenzetu, kuwa ni wapinzani, lakini sasa anatufanyia wenyewe ndani ya chama na tumeanza kugawanyika, wachache wamejitokeza kupinga hilo.

Msando ameendelea kumuuliza Polepole kwamba, "Kwa maelezo yako kwa nyakati tofauti unatambua kwamba wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa walikutana na kufanya maamuzi. Na kikao hicho kina madaraka ya mwisho. Je kwa uzoefu wako kiungozi na kitaaluma ni utaratibu gani unapaswa kufanyika kutengua maamuzi ya kikao cha mwisho au kupinga madaraka ya kikao kikuu cha chama?"
Swali hili ameliuliza kama yupo kizimbani au Mahakamani, lakini jibu lake ni rahisi, kwanza kikao au mkutano ambao si halali ktk kuketi kwake, kikiketi na kufanya maamzi au maazimio ya kitaasisi au chama, chenyewe kinakuwa kimekiuka kanuni, taratibu au katiba na kwa hiyo automatic kimejifuta.
Kama ni kamati ya siasa inafutwa kwa kufanya uasi, kuanzia katibu chama, mwenyekiti na wajumbe wake wanakosa sifa, wanatutwa uongozi na kubaki wanachama wa kawaida tu.

Pili, vyama vya kisiasa kwa kiasi fulani vipo chini ya msajili wa vyama vya siasa, kama utaratibu ndani ya chama haujazingatiwa msajili ana mamlaka ya kutengua maamzi haramu ambayo yamekiuka misingi ya katiba na kanuni ya chama.
Kitendo cha msajili kuukalia kimya ukiukwaji uliofanywa na akina Samia ni udhaifu mkubwa sana na ni aibu kubwa, si kwake tu bali niabu kwa ofisi mbele ya umma.

Mwisho, Msando ameuliza swali hili kwa mtindo ule ule wa kimahakama wanavyouliza mawakili, kwamba "Kwa mwanachama ambaye maamuzi ya chama hayajampendeza au hakubaliani nayo akishasema mawazo yake kwa namna yoyote ile aliyoichagua hata kama ni nje ya vikao rasmi desturi na utamaduni wa CCM unaousisitiza unaelekeza nini?"

Kuna namna ya kikatiba na kanuni ya kulalamikia jambo lililokosewa ndani ya chama, moja ni kupinga ndani ya kikao, pili ni kuandika barua kwa mamla za juu kuomba au kupinga uamzi uliofanyika.
Changamoto iliyopo tangu muda mrefu ni kwamba ukiandika barua mara nyingi unamwachia PS, hawa maPS wengi wanamilikiwa na wanasiasa mafisadi ambapo PS hawezi kuipeleka barua kwa katibu wa chama kabla haijapitia kwanza kwa mwanasiasa huyo, na yeye ndiye wakusema "hii sawa iende kwa katibu lakini hii hapana usiipeleke."

Sasa umeshapeleka barua ofisini ukampa PS na haijafikishwa sehemu husika, unabaki unalaumu viongozi kuwa wamekupuuza barua yako kumbe haijawafikia.
Wakati mwingine inawafikia lakini tunafahamu viongozi wetu wasivyojali mambo ya msingi, wanachojali ni umbea, majungu na fitina, zaidi ni kulinda maslahi ya makundi ya wanasiasa.

Kwa hiyo, baada ya njia zilizoelekezwa ktk chama kuwa na changamoto kama hizi, njia inayobaki ni mwanachama au kiongozi aliyekerwa au kutokubaliana na maamzi fulani kuueleza umma wa wanachama ili waelewe kinachoendelea au kilichokosewa ndani ya chama chao.
Na hatua hii si lazima wanaolalamikiwa wachukue hatua za kulishughulikia, wanaweza kuyashughulikia malalamiko au kuyapuuza kama tu tunavyoona Mama na Nchimbi wake wamepuuzia maonyo, makatazo na mawazo ya wanachama na viongozi wa dini.
Kwa kuwa umma wa wanachama umeshaelewa makosa yaliyofanywa na waliojiteua bila kufuata utaratibu na misingi ya chama, kazi hiyo ya kutengua haramu inakuwa ni ya Mungu mwenyewe ambaye ni wa wanyonge.

Kwiyeya Singu. 0784977072
 
Back
Top Bottom