Polepole ana watu na ana hoja, sijui CCM wafanyeje ili kumdhibiti?

kwa hiyo unataka tufuatilie maigizo ya uchaguzi wa CCM ambao hata wenyewe hawajui mgombea wao wa uraisi kateuliwa na nani!
 
Na wewe ukimaliza kuongea unadhani tutakuelewa? Wewe wa Facebook huwezi kuiona impact ya hoja za polepole. Komaa tu na Umbea
 
Chawa na kunguni ndio wameachiwa jukumu la kumjibu😂😂😂
 
Ukweli ni kuwa Polepole anaongea yale ambayo watanzania walio wengi ama wanayajua kwa kiasi fulani au mazingira yamewafanya kuwa na hisia fulani. Kwa hiyo Polepole anaweka wazi, anafafanua, na kuna wakati anatoa uthibitisho ulio wazi.

Kwa sasa, wasiojua wanasema kuwa Polepole anapiga kelele zisizo na msaada lakini wasichokijua ni kuwa anachokifanya ni kujenga mazingira ambayo wananchi wengi watambue kuwa nchi imetekwa. Ufahamu huo ndio kwa siku za mbeleni utaamsha mori na hamasa ya watu kujipambania ili kuondoka kwenye utumwa dhalimu. Ukitaka mtu ashiriki kikamilifu ni laxima hiyo mtu hicho anachokipambania kiiguse nafsi yake, ndipo dhamira humjengea ujasiri na moyo wa kujitoa.
 
Naunga mkono hoja, anayo yaongea yanajulikana, ila yeye ameamua kuthibitisha kiwa ni kweli.
Ila tatizo ni kuwa hakita badilika kitu.

Hakubadiliki kitu kwa sababu wahusika wametiwa upofu. Wanaamini kwa vile wamefanya uovu mwingi huko nyuma, na hakuna aliyewahi kuwagusa, basi itaendelea kuwa hivyo hivyo. Wasichokijua ni kuwa wanaweza kubananishwa katika nyakati wasizozitarajia. Na hali hiyo imewahi kutokea kwa wengi.

Kule Liberia, Samwel Doe aliwahi kuwatesa na kuwaua watu wengi, hakuamini kuna mtu atakayeweza hata kumgusa, lakini wakati alipoamini amejiimarisha ndipo walioumizwa walipoinuka, hata hakuamini waliokuwa wanamlinda wameenda wapi, alikimbia kwa miguu kwenda mashambani, ambako nako alikamatwa na kutandikwa na kila aliyetaka. Baadaye aliwekwa juu ya kichanja cha mahindi, kila aliyetaka kumfanya chochote aliruhusiwa, wapo waliomfinya, waliomtandika makofi, waliomtemea mate, na wengine waliamua kumvua nguo zote na kumbakiza kama alivyozaliwa, mwingine akaona wanamchelewesha, akamtandika na jiwe kichwani, akapoteza uhai, waliokuja baadaye wakawa wanachukua tu picha mbalimbali za maiti iliyoachwa utupu.
Hata uwe na nguvu kiasi gani, kinachoweza kukuhakikishia mwisho wa maisha yako, ni kutenda haki. Ukiwa mtenda haki, hata watu wakaudhulumu uhai wako, bado kuna wengi watauheshimu na kuukumbuka mwisho wako kwa kumbukumbu iliyo njema itakayovifanya vizazi vyako viendelee kupendwa na kuheshimika.
 
Haiwezi tokea kwa hapa Bongoland.
 

Kwahiyo Lissu basi sasa mupo na Mzee wa V8?
 
Hahaha nasikia Rostam anamshonea HP suti ya zawadi ila hajajua atamfikishiaje hiyo suti.

Nakumbuka sakata la Dr.Mwakyembe walusema muhudumu wa hoteli alimbadilishia Mwakyembe mataulo na alikuwa wakala wa Rostam.

Baada ya hapo Dr.Mwakyembe ngozi ilibadirika lucha ya kutibiwa India kwa mwaka mzima.

Hahaha wakipata anwani tu wanamzawadia suti baada ya hapo tuna msahau.
 


Nchi inatafunwa kama samaki kibua aliyekaangwa.
 
Umeongea meengi, waliomuua samuel doe akina charles taylor na prince johson hawakuibuka tu from nowhere, bali waliingia msituni kupambana nae kivita!
 
HP ameuishi na kufahamu ujamaa Cuba hawezi kupokea zawadi kijinga namna hiyo.
 
Ipo siku WaTanganyika watajipata... Wataamka na kupambana kulinda vya kwao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…