Uchaguzi 2020 Polepole aongea na Waandishi wa Habari kuhusu mazingatio kwa wagombea wa CCM, aweka wazi ratiba ya uchukuaji fomu ya Wabunge na Madiwani

Uchaguzi 2020 Polepole aongea na Waandishi wa Habari kuhusu mazingatio kwa wagombea wa CCM, aweka wazi ratiba ya uchukuaji fomu ya Wabunge na Madiwani

5 Julai 2020
Mbeya, Tanzania

CCM NYANDA ZA JUU KUSINI : Walalama na kusema tumechoka kuongozwa na upinzani.



Sasa CCM lazima tuchukue hatua dhidi ya wasaliti walio ndani ya chama maana subira ya kungojea imekuwa ndefu na lazima tufanye hima tusikose kupata kura nyingi za wananchi 2020 hapa mkoani Mbeya.

Source : MbeyaYetuOnlineTV
 
10 Julai 2020
Dodoma, Tanzania

Nyufa ndani ya CCM, Makundi yaibuka

Tayari wana CCM ya Zamani wakiwakilishwa na MNEC toka Momba Songwe amefikisha ujumbe juu ya kutoridhika na CCM Mpya kuwasahau waliokipigania chama 2010 - 2015



MAGUFULI AMPA MAKAVU ALIYELALAMIKA WANAOHAMIA CCM KUPEWA VYEO, "NATAKA AWE MJUMBE WA NEC"
 
Hiyo barua fake iliandikwa hapo Ufipa!
Lakini imeakisi ukweli maana ndicho magamba wanachofanya kwa Sasa......

VIJANA WA CCM TUKAE KWA KUTULIA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kila nikiangalia hii picha ya Joshua Nasari, nikikumbuka na swali lililoulizwa na Mjumbe Wa NEC toka Songwe kuhusu wahamiaji kupewa Vyeo badala ya vijana waliopo CCM nacheka Sana.

Definitely tuache Hawa vijana wajinafasi kwa kuwa sioni ndani ya UVCCM mwenye uwezo wa kuwazidi. Nilipokuwa nasema Sana kuhusu hili miaka ya kuanzia 2017 Hakuna waliokuwa wanaunga mkono Hoja hiyo kila mtu alikuwa anaimba litania, Ngonjera,Pambio za Masifu, kupiga Manyanga nk.

Niliwaambia ifikapo 2020 mtakumbuka haya niliyokuwa nawaandikia na niliwaambia CCM Asilia itakuwa imetekwa na kutiwa mfukoni. Ni Dhahiri baada ya chuo Cha kivukoni kushindwa kupika vijana wa CCM Chadema inatusaidia jukumu Hilo.

Huwa nawaambia mnapata wapi ujasiri wa kuwaita Chadema Nyumbu? Hahahahah tutulie infact hatuna vijana wanaofikia viwango vya Hawa watu. Tutulie tuendelee na kujifua.

Ukiona baba yako anawagawia watoto wa Jirani Urithi ujue wewe ni mvuta bangi na mla Unga. Akikupa Urithi utauza upate hela ya kulamba Unga.

Ole Mushi
0712702602
 
10 Julai 2020
Rondo, Lindi
Tanzania

MEMBE - CCM INAHITAJI MJASIRI KAMA MIMI
Siasa za Tanzania na uchaguzi 2020. Kipindi cha Mwandishi wa habari mahiri, mwanadiplomasia na Mwanasheria wa Mahakama Kuu ndugu Jenerali Ulimwengu anazungumza na Bernard Membe.



Baada ya leo Halmashauri Kuu ya CCM ikiwa imeunga mkono kufukuzwa uanachama toka CCM siku ya Jumatatu 13 Julai 2020 Bernard Membe atarudisha rasmi kadi ya chama cha CCM na hivyo Membe amekubali kuvuliwa kwake uanachama.

Endelea kusikiliza mahojiano kuhusu kinachofuata baada ya kutimuliwa rasmi na yeye kuafiki kuwa nje ya CCM . Agusia idara za Usalama hushauri vyema lakini viongozi wanasiasa hawatilii maanani ushauri huo mzuri wa idara.

Bernard Membe anasema WanaCCM wengi katika kupiga kura hawataunga "Juhudi za Maendeleo ya Vitu" bali watapiga kura kuungana na wengine kuchangua wale wa upande wa sera za Maendeleo ya Watu.

Source: Jenerali Online
 
Ole wenu CCM msimpitishe huyu nabii wenu!
IMG_20200713_162849.jpg
 
Mimi nimeona kitu kimoja muhimu sana mezani kwa Polepole nacho ni madini(kitabu) "The Looting Machine- By Tom Burgis"
Ahsante Polepole nimekitafuta na kukipata, nikaona kamstari kanasema "It's forbidden to piss in the park" nikacheka sana acha nikisome at least 50 pages kwanza.
TheLooting.PNG
 
Watia nia wa hilo li chama wanaongoza kwa rushwa..sijui watazirudishaje pesa zao wakishachàguliwa.
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM komredi Polepole ataongea na waandishi wa habari kuanzia saa 10.00 jioni.

Kikubwa ni nidhamu ya kuzingatiwa kwa watia nia ya kugombea Ubunge na udiwani kwa tiketi ya chama tawala yaani chama dume CCM. Baba Lao.

Mkutano unafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Updates;

Maendeleo hayana vyama!



Mh. Polepole ameanza kwa kueleza mafanikio waliyoyapata katika kutafuta Wagombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais wa Zanzibar.

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Polepole amewashukuru Wanadodoma kwa kuwapokea vyema katika mji huo na Wajumbe wote waliofika katika mji huo kuwa na wakati mzuri sana na kuwafanya kumaliza mkutano wao kwa amani na mshikamano mkubwa.

Sambamba na hilo, Polepole amewashukuru Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kwa kumpa dhamana Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kugombea kwa kipindi kingine ili akaikamilishe kazi aliyoianza katika muhula wa kwanza.

Zaidi ya hayo, Polepole amewashukuru wasimamizi wa Uchaguzi kuanzia kwenye Halmashauri kuu kwa kazi waliyoifanya kuanzia kwenye mchakato wa kumpata Mgombea urais Zanzibar na Wasimamizi wa uchaguzi waliowezesha kumpata Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Aidha, Polepole ameeleza kuwa kutokana na kuwapo kwa maswali mbalimbali yapo mambo mbalimbali ambayo chama kingependa kutoa ufafanuzi baada ya Uchaguzi wa Wagombea nafasi za Urais kukamilika.
 
Fomu za ubunge na udiwani kupitia CCM,wagombea wanadaiwa. Kulipia gharama za uchaguzi Mara utakapo rudisha fomu tarehe 17, ambapo ni udiwani ni Kati ya TSH 150,000 Hadi 250,000 kwa mgombea mmoja.kwa gharama za kuchangia uchaguzi kwa ngazi ya wabunge kila mgombea anatakiwa kulipa Kati ya sh 250,000 Hadi 500,000.

Gharama hizi zinatofautiana kata kwa kata,wilaya kwa wilaya,mkoa kwa mkoa.tunaomba chama Cha mapinduzi kitoe maelekezo kamili kwa wagombea kiasi Cha kulipa fomu na kiasi Cha kuchangia uchaguzi ili kifanane nchi nzima kuliko Hali ilivyo sasa.

Hii inafanya walio wengi kuweza kununua fomu za kuomba uteuzi Ila watashindwa kuchangia gharama za uchaguzi na mwisho watatenguliwa na wataambiwa hawana sifa kwa kigezo Cha kukosa fedha za kuchangia uchaguzi.
 
13 Julai 2020
Dodoma, Tanzania

Polepole : Mabango au Vipeperushi viwe vya ktk nguzo au mtandaoni haviruhusiwi na CCM Mpya

Watia nia ktk kutaka kuteuliwa kugombea uongozi wa nafasi vyombo vya dola kupitia CCM Mpya wasomewa makatazo ikiwemo vipeperushi ktk mitandao ya kijamii
 
13 Julai 2020
Mbeya, Tanzania

Polepole : Uwanja lazima uwe sawa kwa watia nia CCM Mpya

Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, awakumbusha watia nia wa CCM Mpya kuwa hakuna kuhusisha rushwa ya aina yeyote, wapambe au mabango kwani baadhi ya wana CCM Mpya hawana uwezo kifedha wa kujinadi ktk mitandao, nia ni kutoa haki sawa kwa wanaCCM Mpya.

 
13 Julai 2020
Mbeya, Tanzania

Tulia Trust na marafiki wa Dkt Tulia wamchangia pesa Dkt. Tulia achukue fomu ya ubunge
Kesho 14 Julai 2020 ni siku ya wanaCCM kuanza kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa na CCM Mpya kuwania nafasi za uongozi katika vyombo vya dola.


Source : MbeyaYetuOnlineTV
 
Polepole hapa utatuma barua ya karipio au ulikuwa humaanishi ulichosema leo mjini Dodoma kuhusu wanaCCM kujizuia kuhusisha makundi ktk mchakato wa kwenda kuchukua fomu za kutia nia.
 
Huu ni woga wa CCM Mpya. Zoezi la kutia nia ubunge na udiwani limepooa kupitia CCM Mpya, linafanywa kwa kificho gizani na kutojiamini kisa na sababu mazingatio yanayotolewa Dodoma kuwa wanaogopa makundi.

13 Julai 2020
Dodoma, Tanzania

Polepole : Mabango au Vipeperushi viwe vya ktk nguzo au mtandaoni haviruhusiwi na CCM Mpya

Watia nia ktk kutaka kuteuliwa kugombea uongozi wa nafasi vyombo vya dola kupitia CCM Mpya wasomewa makatazo ikiwemo vipeperushi ktk mitandao ya kijamii

Hili la kukataza vipeperushi vya watia nia naunga mkono,ilikuwa ni ulimbukeni na matumizi mabaya ya rasilimali fedha.
 
19 Julai 2020
Je Gwajima ameshafeli vigezo, masharti na makatazo kwa watia nia CCM kuanza kampeni kinamna?

GWAJIMA AWAJIBU WANAOSEMA KAKIMBILIA SIASA ASEMA “HARUDI NYUMA, AMETOKA KUPIGANA VITA"
Gwajima anasema anapanua huduma nyingine ili apate nafasi Bungeni atunge sheria, huduma za maji, kuleta barabara n.k

 
GwajiBoy naona ameamua 'kujilipua' asiteuliwe na kamati ya wilaya ya CCM na kurahisisha kazi ya Kamati ya Maadili ya CCM Mpya Dodoma kuelekea kuteua wagombea wake 2020.
 
Back
Top Bottom