Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM komredi Polepole ataongea na waandishi wa habari kuanzia saa 10.00 jioni.
Kikubwa ni nidhamu ya kuzingatiwa kwa watia nia ya kugombea Ubunge na udiwani kwa tiketi ya chama tawala yaani chama dume CCM. Baba Lao.
Mkutano unafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Updates;
Maendeleo hayana vyama!
Mh. Polepole ameanza kwa kueleza mafanikio waliyoyapata katika kutafuta Wagombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais wa Zanzibar.
Kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Polepole amewashukuru Wanadodoma kwa kuwapokea vyema katika mji huo na Wajumbe wote waliofika katika mji huo kuwa na wakati mzuri sana na kuwafanya kumaliza mkutano wao kwa amani na mshikamano mkubwa.
Sambamba na hilo, Polepole amewashukuru Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kwa kumpa dhamana Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kugombea kwa kipindi kingine ili akaikamilishe kazi aliyoianza katika muhula wa kwanza.
Zaidi ya hayo, Polepole amewashukuru wasimamizi wa Uchaguzi kuanzia kwenye Halmashauri kuu kwa kazi waliyoifanya kuanzia kwenye mchakato wa kumpata Mgombea urais Zanzibar na Wasimamizi wa uchaguzi waliowezesha kumpata Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Aidha, Polepole ameeleza kuwa kutokana na kuwapo kwa maswali mbalimbali yapo mambo mbalimbali ambayo chama kingependa kutoa ufafanuzi baada ya Uchaguzi wa Wagombea nafasi za Urais kukamilika.