GE2025 Polepole, Asante kwa ukweli wako kuhusu kiini macho cha Uchaguzi. Hoja ya tusishiriki, haina tija tena na Uchaguzi Upo!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hapana mkuu, nilitegemea ungekuwa sehemu ya kutuhamasisha kudai mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi!
Tuendelee kutiki na Polepole katufungua macho kuona namna watu wachache wakifaidi mema ya nchi na kufanya maamuzi wao wenyewe huku majority tukuendelea kugubikwa na lindi la matatizo hata kuipata paracetamol tu kwetu ni mtihani.
Ni vipi unafikiri kwamba hilo lori litaanguka ikiwa wengi wetu tutaitikia wito wa kutokujitokeza kupiga kura?
 
Hayo maendeleo labda kama umeyaona wewe, mtu akuibie halafu akuletee maendeleo? Seriously??
 
Sasa kama Mpina alishajiunga toka zamani na ACT kule CCM aliombaje kugombea Ubunge tena??

Mpina hana sifa za kugombea Urais kwa ACT kwasababu Sheria ya Vyama vya Siasa ya Tanzania (Political Parties Act, Cap. 258, Marekebisho ya 2011 – Act No. 11 of 2011) inasema:
"Mtu hataruhusiwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa zaidi ya kimoja kwa wakati mmoja."

Na kifungu cha 14(4) kinafafanua kuwa iwapo mtu ataamua kujiunga na chama kingine, uanachama wake wa chama cha kwanza unafutika mara moja kisheria, hata kama hajakata kadi ya kwanza rasmi.

kwahiyo huu ni ushahidi tosha kuwa zile rabsha za Mpina na Utawala zilikuwa drama.. Huyu ni Sellout tu wa CCM kuaminisha watu kuwa kuna wagombea...
 
Anatuambia tukapige wakati huo anakiri kwamba uchaguzi kufanyikao siyo huru na wa haki, sasa anataka tukapige kura ili tuendelee kuupa nguvu udhalimu au 😁
 
Hili ni bandiko la ki utu uzima toka kwa kaka Paskali.Unapaswa uwe na jicho la tatu kuuelewa uzi huu.Kama huwezi kuisikia the voice within,nakushauri upite tu kimya kimya au urudie kusoma taratibu neno kwa neno kilichoandikwa pengine unaweza kuelewa.
 
CHAWA WA MAMA ,shikamoo MZEE
 
Kunihamasisha Mimi kwenda kupiga kura, ni sawa na kumpigia debe Mbizi.....Kila siku naongezewa sababu za mimi kutokwenda kabisa Wala kusogelea kituo Cha kupigia kura....mifumo ya kijambazi inaongozwa na majambazi...miaka yote ya uchaguzi nilipokuwa nikienda kupiga kura walikuwa wananichora na kuniona jinga Fulani🤔...kumbe kura wanazo tayari na wananipotezea muda wa kutafuta riziki🙁
 
Kaka Paskali
1. Kwanini unatetea uovu kwa kuhofia yatakayotokea???
2. Kwani wakati tunaingia kwenye vita ya KAGERA, hatukujua kuwa kuna watu watakufa?? Mbona tuliingia?? Tungeachia mipaka kisa kuna kufa???

Kwenye hili siafiki hoja yako
Alitakiwa kunyamaza kuliko kuunga mikono kinachoendelea. Mayala anajiingizaga katika uovu kirahisi sana.
Mayala hii ni DHAMBI kaa nayo mbali
 
Alitakiwa kunyamaza kuliko kuunga mikono kinachoendelea. Mayala anajiingizaga katika uovu kirahisi sana.
Mayala hii ni DHAMBI kaa nayo mbali
Kabisa, kuna vitu busara inakutaka ukae kimya au useme kwa mujibu wa ukweli halisi wa mambo ulivyo. Kwamba eti kwa sasa ni too late, gari lipo mteremkoni hivyo si busara kusimama kwa breki, ni upotoshaji uliotukuka. Madhara ya kuendelea na hali ilyopo ni makubwa kuliko kubadili.

CC Pascal Mayalla
 
Kwanini wewe, maana mamlaka haikutaki hawakupi uteuz bado tuu unqjikomba mzee P bwana unazeeka vibaya.
 
Kwa nini uende kwenye Job interview huku ukijua kwamba tayari walisha fanya uteuzi wa mtu wao?
 
Ni nini kipya ambacho Polepole amekisema hakijasemwa humu?.
Naam, kama kweli watanzania tunatwka mapambano basi tuanze kuandaa nguvu maana pambano halali la mabadiliko lenye asilimia nyingi ni 2030

2025 ilikua ni dirisha zuri ila limeshavurugwa
 
Ukatiki vipi wakati umeshatikiwa?. Wewe hata ukienda au usipoenda tiki ipo pale pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…