GE2025 Polepole, Asante kwa ukweli wako kuhusu kiini macho cha Uchaguzi. Hoja ya tusishiriki, haina tija tena na Uchaguzi Upo!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
P kwa yakitaifa hata Press card ama ithibati za faa zitolewe sadaka.
 
, ghafla the rate of change of acceleration ni direct
Objection Mwanabodi!!!.
There is no such a thing like "the rate of change of acceleration". Just say "acceleration" maana hiyo acceleration yenyewe ndio "the rate of change of Velocity(speed)"

AU lah basi ungesema "The rate of change of velocity or speed".

Nawasilisha.
 

Duuh, uTanganyika kazi sana!
 
So unashauri watu waende kwenye uchaguzi ambao Tume ni Tawi la CCM?
 
Upo sahihi kabisa. Oktoba tunatiki kama kawaida. Mbona uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 hakuyasema haya huyu mpuuzi??
 
Huku niliko niliwahi kuona majiko ya gesi yanatembezwa mitaani na watu kuhamasishwa kuyanunua Kwa nusu bei lakini kwa sharti la kuwa na namba ya Nida.
Nilijiuliza sana nini uhusiano wa mimi kupunguziwa bei halafu nipewe sharti la kukabidhi namba yangu ya Nida?
Leo ndio nimeungaiaha dots kupitia kwa hii taarifa nzito ya HP.
Kweli kila kitu kina muda wake. Unaweza kujitahidi kuficha uovu wako lakini ni suala la muda tu.
 
Paskali Bana….. kama kawaida yako…..una hit the point then una i cosmetic the point 🤣

Dah
 
Kampeni ya #NoreformsNoelection iliyoasisiwa na CHADEMA ipo kwenye mchakato kwa zaidi ya miezi sita sasa.
Tundu Lissu kila anapoonekana Mahakamani huwa anevaa T-shirt yenye ujumbe wa NRNE kwa zaidi ya siku 100
Pole Pole ameongea kile kile kinachosemwa na wapinzani na kuhitimisha kwa hoja ile ile ya wapinzani ya kutokuwepo uchaguzi bila reforms....

Huu ujasiri uliojawa na kiburi cha watawala unaoonyesha kuwa Pole Pole kwa alichokisema jana hakiwezi kubadilisha chochote kwa uchaguzi ujao kiratiba mnautoa wapi? 🤔

Nimemsikiliza Kamanda wa kanda maalumu jana na huko nyuma Makamu mwenyekiti wa CCM na Mwenezi wake, wote wamejaa kauli za vitisho kwa wapiga kura wanaoonyesha kutokubaliana na uchaguzi wa mwaka huu bila reforms?

Yaani mfano wako wa Semi trailer lililowekwa kwa makusudi kwenye mtelemko ni halali kuendelea na mchakato asiwepo hata mtu mmoja wa kuhoji maamuzi yaliyotufikisha hapa? 😲
 
Ndg yangu Paskali, kwa jinsi ninavyokufahamu, sikutarajia kama ungeweza kuandika upuuzi kama huo.

Yaani unasema hakuna mapya aliyoongea Pole pole? Kwamba apuuzwe kwa vile hakuna jipya aliloongea?

Unawaambia watu wakapige kura kuchagua Chama gani ilihali kinachoshiriki Uchaguzi ni Chama kimoja?

Unawaambia watu waende kupiga kura ili iweje kabla ya wahusika kujitokezq na kutolea maelezo tuhuma anazotoa Polepole kuhusu mifumo ilivyounganishwa ili kuwezesha uchakachuaji wa kura kwa lengo la kuibeba CCM?

Unawaambia watu waende kupiga kura ilhali kuna tuhuma kwamba CCM imezingirwa na kundi lenye maslahi binafsi ambalo linamtumia Rais kwa malengo binafsi?

Kwa haya na mengine, wewe Ndg Paskali, kwa utu uzima wako, kwa malezi uliyopata, elimu ya Sheria na Uandishi wa habari, unapataje ujasiri wa kuandika haya?

Kweli umeandika haya ukiwa katika Hali ya kawaida? Au kuna msukumo gani ambao hautoki kwenye nafsi yako?

Kutokana na uzoefi wako humu na makala zako, unadhani unaweza kuwapotosha na kuwashawishi watu kirahisi hivyo??

Elimu aliyoitoa Polepole inatakiwa kusambaa kwa wapiga kura wote. Watu watapima, wataamua. Tusitumie elimu na uwezo watu kuwashawishi watu mambo ya hovyo. Tumuogopeni Mungu.

Ni Mimi Ndg Jifundu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…