#COVID19 Polepole aweka msimamo wake wa kutochanjwa

#COVID19 Polepole aweka msimamo wake wa kutochanjwa

Jasusi Mbobezi

Senior Member
Joined
May 17, 2020
Posts
195
Reaction score
851
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook, alipokuwa akiongelea kuhusiana na muziki wa Singeli, sentensi yake ya mwisho ilikuwa ni kutoa msimamo wake kuhusu chanjo, amesema chanjo ni hiyari na yeye hatachanja.

Huyu ndiye Polepole ninayemfahamu, Mungu akujalie ufike mbali, kile kiti kinakufaa kabisa.
 
Polepole ulimuangalia kwa jicho la kisiasa kutokana na mlengo wake wa kiitikadi, kama haupo upande anaousimamia unaweza kumchukia. Lakini linapokuja suala la imani yake kuhusu Mungu anayemuamini hapo ni lazima tu utamtaka.
 
Polepole ulimuangalia kwa jicho la kisiasa kutokana na mlengo wake wa kiitikadi, kama haupo upande anaousimamia unaweza kumchukia. Lakini linapokuja suala la imani yake kuhusu Mungu anayemuamini hapo ni lazima tu utamtaka.

Mungu gani huyo?hao ‘mungu’ wao alikua Magu ndiye waliyekua wanamnyenyekea na Kabudi wake.
 
Hasira tu hizo za kutolewa ukatibu mwenezi na kukata tamaa ya teuzi.......hamna lolote. Jambo la kupendeza ni kuwa watu makini kuliko yeye wameshachanja tayari. Hana ishu anaweza kurudi tu na kuwa Shuja wa chadema kama mwanzo maana kuwaongoza chadema ni rahisi sana.....we jifanye unapingana tu na serikali au raisi, hata km hujui wapi unaelekea
 
Kuku wanazo chanjo kibao. Ingekuwa chanjo zao zinaambukiza kama hizi za corona basi kungekuwa na barakoa za kuku na ingekuwa biashara kubwa sana duniani. Barakoa ya mdondo, just imagine!!!

Hili suala la kuchanja ama kuto chanja linatugawa mapande mawili, kuanzia ngazi ya familia, uzao, ukoo, taifa na kimataifa na kidunia.

#Hachanji mtu hapa.
 
We Màtaga Acha ujinga,wanatakiwa juchanjwa ni wale wenye miaka 50+ au wenye changamoto mbalimbali.
He huyo Polepole wako ana miaka 50.
 
Back
Top Bottom