GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Nina jamaa yangu ni mtumishi wa umma inabidi Paige Kura hakuna namna maana kwa MFUMO huu lazima watawabaini watumishi waliogoma "kuongeza idadi ya wapiga Kura"

Siku hizi wanaambiwa wenye namba za NIDA na Vitambulisho vya wapiga kura waende ofisi za mitaa yao wapewe mbolea kumbe wanakusanya taarifa
 
Ukiandika title ya thread yenye jina la polepole ..hawaiapprove hapa Jamiiforum.. sasa wana edit mini wakati polepole kila mtu kamsikia anaongea
 
21st to remember, sasa No reform no election imepata hoja ya msingi kabisa.

Pia nguvu ya CCM na amani ya Taifa leo ndio imetetereka.

Kama System za CCM zikiharibika leo na Lissu akashiriki uchaguzi na Tume iliyopo na kura zikihesabiwa manually basi Lissu atamzidi Samia mbali sana, kwa sasa System inaingia kwenye uchaguzi ikiwa na statistics za wapiga kura, wananchi wa Tanzania, kazi zao na kila kitu kuwahusu hivyo ni rahisi kumanipulate matokeo
 
Hii vipi kweli? Naiona inazunguuka sana!
Nikweli inawezekana ila huo UKIKI wake unatija kwa Taifa , wangelipatikana hata watu watano tu wanaougua huo UKIKI naamini hili Taifa lingepona chap.

Stay tuned movie ndiyo kwaanza limeanza

By One Man Show.
 
ACT na CHAUMA ni mifuko ya nyuma ya suruali kubwa CCM. Kwa maelezo ya Polepole bila mifumo huru hakuna uchaguzi kinachobaki ni igizo.
Ndio maana Lissu yuko Jela hili asigombee wakalazimika kuhesabu kura manually
 
Hatari sana, maana yake watapanga Rais, wabunge, madiwani, Chaumma, Act wapate kura ngapi kwa jinsi wanavyojisikia kutumia NIDA.

Kimsingi ni Samia na genge lao la wanamtandao ndio wataochagua viongozi wote Tanzania pande zote mbili za muungano.

Wakienda kwenye huu uchaguzi bila mabadiliko, baada ya uchaguzi watauza na kujimilikisha rasilimali zote zilizobaki na kuongeza makodi, mikopo zitakazoelekezwa kutunisha account zao binafsi.9
 
Back
Top Bottom