Mimi bado naona hoja yake haina mashiko. Wizi wa kura ulikuwepo hata kabla ya Nida kuzaliwa.
Ballot stuffing haihitaji kuunganishwa na mfumo. Kukata majina ya wagombea hakuhitaji Nida. Kukimbia ofisi ili usipokee fomu za wagombea wa upinzani hakuhitaji Nida. Kuwatia ndani wagombea ili wasiweze kurudisha fomu hakuhitaji Nida. Kupokea fomu za mtu ambae ni dhahiri sio mwanachama wa chama husika hakuhitaji Nida. Kuwatangaza wagombea wa chama fulani kuwa wabunge wa viti maalum bila chama chao kuwapendekeza hakuhitaji Nida. Wakati tuhuma kuhusu mambo haya zinatolewa Polepole hakusema kitu.
Ameacha kukiri mambo ya msingi analeta ya Nida kwa sababu yatawatupia lawama wale anao waita wahuni watu wa mtandao. I am not impressed.
Amandla...
Your point of view is duly noted.
Ila tambua kitu kimoja mkuu - hayo yote uliyosema wanaweza kutupiwa lawama wakurugenzi wa uchaguzi au viongozi kadhaa.
Inaweza kuonekana ni isolated, individual incidents.
Hao wanaweza kuangushiwa jumba bovu, wakatumbuliwa na CCM ikaonekana kuwa relatively safi, so to speak.
Ukitafakari kwa kina hili bomu jipya utagundua kwamba lenyewe ni ultimate veto ya CCM kama chama na taasisi.
1) Inawahusu watawala wa juu na chama chote plus serikali na usalama wa nchi. It's systemic and systematic fraud!
2) Mfumo unaoingilia moja kwa moja INEC (actually inai-override kiasi kwamba INEC inakuwa subordinate kwake!)
3) Haina justification whatsoever. Kwingine kote ulikotaja walau kanuni na sheria zinaweza kutumika kuhalalisha haramu (uenguaji wagombea, nk)
4) It's deeply embedded and mysteriously hidden. Nobody knows about it until there is an insider whistleblowing such as Polepole.
5) Huwezi kui-expose na kui-fight kabla ya whistleblower maana hujui kwamba ipo.
Inaweza kuendelea kuwatafuna kimya kimya muda mrefu sana, hadi mgundue mmeumia vya kutosha.
Again, it's safe to say this is one of the greatest scandals in the history of our country.