Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Kamarada Humphrey Polepole leo Jumamosi Oktoba 17, 2020 atazungumza na Vyombo Vya Habari.
---
Mgombea urais kupitia CCM, John Magufuli Oktoba 19, 2020 ataendelea na mikutano ya kampeni katika mikoa sita akianzia Pwani na kumalizia mkoani Dodoma Oktoba 26, 2020.
Wakati Magufuli akichanja mbuga katika mikoa hiyo, mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan ataendelea na mikutano Zanzibar na Kassim Majaliwa ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM atakuwa Mtwara na Lindi.
Hayo yameelezwa leo Jumamosi Oktoba 17, 2020 na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Amesema mbali na mkoa wa Pwani, Magufuli ataendelea na kampeni katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na kumalizia Dodoma.
Amesema Samia ataelekea Zanzibar na kuhitimisha mkoani Morogoro na Majaliwa mikoa ya Kusini ikiwa ni pamoja na Lindi na Mtwara.