#COVID19 Polepole: Hatuwezi kuzuia watalii kwa sababu ya Corona, tutapambana nayo kama tunavyopambana na Upinzani. Nchi inategemea watalii

WATALII WAANDALIWE MAZINGIRA SALAMA KWAO NA KWETU KWANZA. WAKIINGIA HAPA BONGO WASIJICHANGANYE NA SISI MPAKA KWANZA ZIPITE SIKU 14 tuwapime tena, NDIO TUJUE WAPO SALAMA AU WANA MAAMBUKIZI.

TUKUMBUKE DUNIA NI HII HII MOJA. TUSIPO CHUKUA HATUASTAHIKI SISI, MADHARA YATAENDELEA KUUTAFUTA ULIMWENGU WOTE NA SI WANDENGEREKO PEKE YAO.

 
Katika kuonyesha jinsi viongozi wa CCM wasivyo thamini na kuheshimu Watanzania wenzetu ambao ni wanachama wa vyama vingine nje ya CCM hata kama ni kaka zetu, Dada zetu,wajomba nk. Katibu wa Itikadi mbele ya TV amewafananisha watu na ugonjwa wa Corona.
Hakika tumeuona ukweli wa chama hiki kuwa hakina heshima kwa Watanzania na kina kiburi cha ajabu sana.
Jee tufanyeje kuwaadhibu maana wameshindwa kumuadhibu Polepole? Au ni kweli Watanzania wasio wanaccm ni sawa na Corona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kasema wapinzani hajasema watanzania huwezi jua labda anaongelea wapinzani wa Tanzania kwenye world cup championship
 
Hili la bunge sijamuelewa.

Kwani polepole alichaguliwa lini kuwa msemaji wa bunge???

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Kama wapinzani ni corona kwa mujibu wa Hamphrey Polepole basi CCM ni Ebola.

Huyo msigombane naye kwa maneno mengi nanyie mpigeni kwa hoja tu.
 
Ana maana ugonjwa wa Korona ukiingia CCM unakuwa mzuri. Kwa mwendelezo ugonjwa wa Korona ukiingizwa nchini na wageni unakuwa mzuri kwa nchi!!!!!!!!!

Polepole katubu haraka.
 
Yupo sawa polepole! Hatukufunga mipaka wakati wa ebora, wakati wa mafua ya ndege, wakati wa kipindupindu! Sembuse corona!!
Uko sawa mkuu.

Acha kutetea upumbaf Kama anavowaita huyu kichaa mwenzenu...!!
Kuifananisha CORONA VIRUS(Covid-19)na sijui Ebola,SARS(Mafua ya ndege) na Chorela Ni UCHIZI NA UPUMBAFU.....!!
Hivi unaweza kutushawishi kuwa magonjwa ya Ebola,SARS na kipindupindu yamewahi KUENEA DUNIA NZIMA KAMA ILIVO CORONA wakti huu?
Polepole ni CHIZI lazima akemewe na akome kupotosha Umma wa Tanzania.
 
Ni kweli,lakini si busara tukiendelea kuweka rekodi za wagonjwa wa Corona wanaotoka nje either ni watalii au Watanzania kwa kufanya hivyo tutawaletea taharuki Wananchi wetu.
Ni vema tukajizuia kusema sana maana hatujui kesho ikoje,na kamwe tusichanganye siasa na maisha ya watu maskini otherwise kama tumejiakikishia tunazo immunities za kutosha.
Na wapinzani nao wajiweke mbali na matamko kuhusu hili janga,sio lazima kila kitu kiwe in public wakutane waandae maelezo wanayoyaona yanafaa kwa maandishi na kuyawakilisha serikalini.
Janga la Corona sio mtaji wa kisiasa Bali ni suala la Usalama na afya za wananchi,ni wajibu wetu kushikamana kama Taifa na kushauriana kwa pamoja kuliko kila ka kikundi/mtu /Taasisi kutoa matamko yenye kuligawa Taifa.
 
Kipimo cha upinzani kuimarika ni kipi?
Umesahau enzi zile Dk slaa alivyokuwa anasimama jukwaani? Umesahau Dk slaa alisema nchi haitawalika mpaka mkuu wakati huo akanywea? Umesahau Dk slaa alivyoimarisha chama mpaka wabunge wakafika zaidi ya 40. Au unajifanya hujui.
 
Acha nimshukuru Mungu tu kwa kila jambo


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…