Polepole: Hii sio awamu ya Sita bali ni ya Tano kipindi cha pili, aliyeondoka ni Magufuli peke yake

Polepole: Hii sio awamu ya Sita bali ni ya Tano kipindi cha pili, aliyeondoka ni Magufuli peke yake

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Wakuu,

Mbunge wa kuteuliwa na mtunga Sheria Humphrey Polepole, anadai hii awamu ya rais Samia sio awamu ya sita.

Rais Samia alisema yeye ndiye rais ya awamu ya Sita. Kwamba ni awamu ya sita kipindi cha kwanza.

"Hii serikali sio mpya,haikupigiwa kura, huwezi ukaita awamu ya sita, awamu lazima iwe na miaka10, ilani na Sera zinazopaswa kutekelezwa ni zile tulizozinadi 2020, asiwadanganye mtu kuwa hii ni awamu ya sita,Kwa sababu aliyeondoka ni Magufuli peke yake" kasema polepole.

RAIS SAMIA ANASEMA UFISADI ULIFANYIKA AWAMU ZILIZOPITA SIO AWAMU YAKE YA SITA
"Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya serikali, na yanageuka kusema serikali ya awamu ya 6 ufisadi umerudi mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo, mambo hayo yalifanyika huko nyuma, gari bovu linaangushiwa awamu ya 6 sitakubali"
Rais Samia Suluhu akiwa Bandarini.

Je, nani yupo sahihi na Sheria inasemaje?

 
Polepole anasema yupo anawafuatilia watu fulani. Ambao hakuwataja kwa jina ila amesha wapa warning kuwa wakivurunda atawaambia wazi wazi kuwa umevurunda. Inaonesha kuna watu wanataka waachane na ile miradi mikubwa ya awamu ya magufuli
 
Wakuu,

Mbunge wa kuteuliwa na mtunga Sheria Humphrey Polepole, anadai hii awamu ya rais Samia sio awamu ya sita...
Polepole anatakiwa kujua Samia ni Amiri Jeshi Mkuu!

Anaesema hii ni awamu ya Sita ni Rais Samia Mwenyewe! Sasa kama anapinga hii sio awamu ya Sita ajue anapingana na Rais Samia mwenyewe!

Kifupi anatakiwa ajue sonono aliyokuwa nayo juu ya Rais Samia sasa itaenda kumuonesha kuwa Samia ni Rais Kweli na Amiri Jeshi Mkuu
 
Polepole jamani wampeleke Milembe, anaweweseka, Godfather kamuacha yatima,

Polepole anamtishia box la kura MWENYEKITI WA CCM Taifa, haaa haaa haaa mnafiki, chakubanga, kiroboto atulie watu wale nchi kama yeye alivyokuwa akiila na maviete.

MAISHA yanaenda kasi sana Polepole anaweweseka?? Dunia hadaa..
Comrade Kinana ka anamcheki kwa mbali...

Everyday is Saturday................................😎
 
Hivi polepole alinyang'anywa hela zote alizopiga nini? Mana inaonekana hana cha kupoteza kwa sasa. Ila polepole akipata chochote atanyamaza tu.

Huyu jamaa asingekuwa mnafiki, basi alikuwa ni mwanaharakati jasiri.

Enzi za Kikwete, polepole alikuwa anaikosoa CCM wazi wazi.

Pia, hawa ndio waliokusanya maoni ya katiba mpya.

Jiwe alikuja kumvuruga polepole na kumfanya mnafiki. Leo hii hata afanye vipi, watu hawawezi kumuelewa Polepole kwa sababu aliishajidharirisha enzi za Jiwe!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Polepole jamani wampeleke Milembe, anaweweseka, Godfather kamuacha yatima,

Polepole anamtishia box la kura MWENYEKITI WA CCM Taifa, haaa haaa haaa mnafiki, chakubanga, kiroboto atulie watu wale nchi kama yeye alivyokuwa akiila na maviete...😎
Fisi anajaribu kumtisha simba amwachie japo kipande cha mfupa.
 
Back
Top Bottom