Polepole: Hii sio awamu ya Sita bali ni ya Tano kipindi cha pili, aliyeondoka ni Magufuli peke yake

Polepole: Hii sio awamu ya Sita bali ni ya Tano kipindi cha pili, aliyeondoka ni Magufuli peke yake

Polepole anatakiwa kujua Samia ni Amiri Jeshi Mkuu!

Anaesema hii ni awamu ya Sita ni Rais Samia Mwenyewe! Sasa kama anapinga hii sio awamu ya Sita ajue anapingana na Rais Samia mwenyewe!

Kifupi anatakiwa ajue sonono aliyokuwa nayo juu ya Rais Samia sasa itaenda kumuonesha kuwa Samia ni Rais Kweli na Amiri Jeshi Mkuu
Mjibuni kwa hoja badala ya vitisho simply mna vyombo vya dola!
 
CCM si huwa wanasema kuwa endapo makada wao wakigombana, basi huwa wanatafuta suluhu kuhusu tofauti zao ndani ya vikao vyao rasmi vya chama. Sasa mbona hawa waliokuwa makatibu waenezi kila siku hawaachi vituko vya kupigana vijembe pasipo hata kusuluhishwa?

Hiyo lugha ya awamu za uongozi katika nchi ziliasisiwa na CCM yenyewe. Wao waliamini kuwa baada ya kupita awamu ya uongozi wa Baba wa Taifa, awamu zitakazofuata ziwe za Rais atokanaye na chama chao, apishwe na kutawala vipindi viwili vya uchaguzi vyenye jumla cha miaka 10.

Kwa muktadha huo, ili kumtafuta mpeperusha bendera katika kinyang'anyiro cha nafasi ya urais, Rais aliyepo madarakani hapaswi kushindanishwa na kada mwingine katika kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano. Hivyo basi hupewa nafasi ya kutawala mpaka amalizie kipindi chake cha pili.

Kwa mantiki hii, awamu ya utawala ndani ya CCM huendana na dhamana pamoja na ridhaa ambayo kada wa chama hicho amepewa fursa ya kuwa Rais na Mwenyekiti Taifa. JPM pamoja na kutokuweza kukamilisha muda wake wa utawala wa miaka 10, bado aliweza kupitishwa kuwa mgombea na hatimaye kuwa Rais atokanaye na chama chake.

Baada ya mauti kumfikia, hapo ndipo ilikuwa mwisho wa awamu yake. Awamu huusishwa na mtu na wala siyo muda wa utawala, na pia awamu humuangalia Rais na Mwenyekiti Taifa aliyepo madarakani. Rais SSH yupo sahihi kabisa, yeye ndiye Rais wa awamu ya 6.
 
Tumia Akili Awamu ZIMEANZA kutumika kuanzia Utawala wa Mwinyi
Wewe umeona una akili hapo? Kama zimeanza kutumika wakati wa mwinyi mnaitaje ya magufuli ni awamu ya tano badala ya nne?. Awamu zinatajwa kwa kila Rais akipita au kafa na awamu imepita. Ndiyo maana hii inaitwa ya sita kuanzia nyerere mpaka samia
 
Tumia Akili Awamu ZIMEANZA kutumika kuanzia Utawala wa Mwinyi
Kwahiyo kama zimeanza kuanzia utawala wa mwinyi ya nyerere haihesabiki kama ni awamu?? Ama wewe upo awamu ya ngapi na umeanza kuhesabu kwa raisi yupi??
 
Kwa hiyo Rais akitawala kipindi kimoja(miaka5)kipindi cha pili akashindwa kwenye sanduku la kura awamu yake inafutwa mpaka ifike miaka kumi?

Hii ni awamu ya sita na Rais ni wa sita awamu ubadilika baada ya Rais kubadilika ndio maana pamoja na Hayati Mwl Nyerere kutawala kwa kipindi kirefu cha miaka26 lakini tunaita hiyo ni awamu ya kwanza
 
Mang'ula amesema ilani ya uchaguzi ilizunguzia kujenga gati bagamoyo huyu rais atuonyeshe ilani yake aliyoingia nayo kwenye uchaguzi
 
Wakuu,

Mbunge wa kuteuliwa na mtunga Sheria Humphrey Polepole, anadai hii awamu ya rais Samia sio awamu ya sita...
Wewe kubali tu tuko awamu ya 5. 2020 tumemchagua magufuli wewe jitahidi kuendeleza msimamo wa kimagufuli ndio watu walimchagua. Ukifanikisha hilo hakika watu watakupenda sana. Mungu akubariki mama yetu.
 
... fisi anajaribu kumtisha simba amwachie japo kipande cha mfupa.
Yale yote aliyoahidiwa na mwendazake anaona hayatimii,
Amepanikii maana mama Rais anatembelea mawaziri wakuu wastaafu, mara kongamano la Jenerali Nnauye, yaani katengwa kisaikolojia anaumiaa.

Ka vile playground, wamemtenga, wanachezea midoli na bembea yeye hawampi!

Bahati mbaya hakuna anayemsikitikia ingawa kuna nguvu nyuma yake inamfamganya watanzania wapo nyuma yake.

Siasa mchezo mchafuu.

Everyday is Saturday................................😎
 
Hata ikiwa ni awamu ya kumi hiyo itatusaidia nini sisi?
Kwangu mimi awamu maana yake ni kipindi cha mtawala akiwa madarakani, na hapa Tz mtawala ni rais.
Rais=awamu
Nyerere (awamu ya kwanza)
Mwinyi (awamu ya pili)
Mkapa (awamu ya tatu)
Kikwete (awamu ya nne)
Magufuli (awamu ya tano)
Samia (awamu ya Sita)
Chakubanga (awamu ya saba?!)🤣
 
Inawezekana polepole yuko sahihi kwa maana kwamba aliyebadilika ni rais peke yake. Kwa hiyo tunaweza kusema Samia ni rais wa sita katika awamu ya tano
 
Kwahiyo ni serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Raisi wa sita enhee? Sisi tunapotumia neno " awamu" tunamaanisha serikali inayoongozwa na fulani haijalishi amekaa madarakani miaka mingapi ila tunaangalia amekaa kwa muda huo amekaa madarakani mara moja tu alipomaliza muda wake wa miaka ya yeye kukaa madaraka kwa kushika nafasi ya uraisi kwisha ama ameiacha na hatukuwa tena na uwezo wa kisheria kurudia nafasi ile ya uraisi ndipo tunasema awamu. Nyerere tumemuhesabia amakaa madarakani kwa awamu moja tu alipomaliza ameachia ngazi.
 
Nyerere aliyetawala Tanzania kwa miaka 21 alitawala kwa awamu ngapi?
Ila ulifanyika uchaguzi..kupata serikali mpya na wabunge wapya chini ya mwinyi kama rais..hivyo ikaitwa awamu ya pili mwinyi akiwa rais wa pili..nikuulize wewe mchumia tumbo..baada ya JPM kufa kuna uchaguzi uliofanyika? ili kuharalisha kua hii ni awamu nyingine..au ni kumalizia awamu ya 5 kwa mujibu wa katiba?

#MaendeleoHayanaChama
 
Polepole anatakiwa kujua Samia ni Amiri Jeshi Mkuu...
Katiba inasemaje..au tunaedeshwa ni mtu mmoja kwa mawazo yake..kwahiyo angesem awamu ya 10 mngekenua meno tu..njaa ya kichwani mbaya sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom