CCM si huwa wanasema kuwa endapo makada wao wakigombana, basi huwa wanatafuta suluhu kuhusu tofauti zao ndani ya vikao vyao rasmi vya chama. Sasa mbona hawa waliokuwa makatibu waenezi kila siku hawaachi vituko vya kupigana vijembe pasipo hata kusuluhishwa?
Hiyo lugha ya awamu za uongozi katika nchi ziliasisiwa na CCM yenyewe. Wao waliamini kuwa baada ya kupita awamu ya uongozi wa Baba wa Taifa, awamu zitakazofuata ziwe za Rais atokanaye na chama chao, apishwe na kutawala vipindi viwili vya uchaguzi vyenye jumla cha miaka 10.
Kwa muktadha huo, ili kumtafuta mpeperusha bendera katika kinyang'anyiro cha nafasi ya urais, Rais aliyepo madarakani hapaswi kushindanishwa na kada mwingine katika kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano. Hivyo basi hupewa nafasi ya kutawala mpaka amalizie kipindi chake cha pili.
Kwa mantiki hii, awamu ya utawala ndani ya CCM huendana na dhamana pamoja na ridhaa ambayo kada wa chama hicho amepewa fursa ya kuwa Rais na Mwenyekiti Taifa. JPM pamoja na kutokuweza kukamilisha muda wake wa utawala wa miaka 10, bado aliweza kupitishwa kuwa mgombea na hatimaye kuwa Rais atokanaye na chama chake.
Baada ya mauti kumfikia, hapo ndipo ilikuwa mwisho wa awamu yake. Awamu huusishwa na mtu na wala siyo muda wa utawala, na pia awamu humuangalia Rais na Mwenyekiti Taifa aliyepo madarakani. Rais SSH yupo sahihi kabisa, yeye ndiye Rais wa awamu ya 6.