Chikuvi2021.
Awamu ya sita imechaguliwa na nani, sera zake ni zipi, ilani yake ni ipi, maono yake ni yapi, kazi iendelea inamaanisha nini, kazi gani iendelee?
Strategy ni hii, tunatukana kila alichofanya JPM, ingawa tulikuwa wasaidizi wake wakuu. Kila kizuri tulishiriki, vibaya hatuwepo.
Elimu watoto milioni kumi kwenda shule serikali ya sasa inakwambia sio kitu, Maji, Umeme wa uhakika wanatafuta sababu za kijinga.
Afya, barabara, sheria za madini rasilimiali, kuliokoa taifa kwenye janga la Covid -19, Corona kwa kuhimiza kuchukua tahadhari, barakoa, kunawa mikono, lakini hakutakuwa na Lockdown wanakwambia wote ujinga.
Nidhamu serikalini imeshuka,Ufisadi, rushwa, madawa ya kulevya, ukiritimba umerudi kwa nguvu, familia chache kuitawala Tanzania labda ndio tunamaanisha awamu ya sita.
Janga la Corona bila serikali makini Wananchi wangeuliwa na polisi (mfano ni Kenya) wakionekana mtaani, wengi wangekufa na njaa, familia nyingi zingevunjika. Watoto kukosa elimu (Uganda).
Polepole anajaribu kuwakumbusha mlikuwa pamoja, mkachaguliwa kwa mgongo wa JPM 2015. Mmemzima labda mipango yenu baadaye ni kumuua. Visasi. Gwajima kumfunga mdomo kisa msimamo wake.
Ushauri Fanya kazi zaidi ya Magufuli utapendwa, Fanya Umeme, maji, huduma serikalini zipatikane kwa Watanzania.
Bei za pembejeo, mbolea, mafuta, petrol, diesel, vifaa vya ujenzi viwe rafiki. Punguza mfumuko wa bei.
Tengezeza ajira, sio kwa washikaji wachache kama wewe Chikuvi2021, wahuni ndugu zako. Futa kesi ya Mbowe.
Utapendwa zaidi.