Uchaguzi 2020 Polepole: Kura ya maoni inaonesha Rais Magufuli anakubalika na wananchi kwa 90% na CCM inakubalika kwa 70%

Uchaguzi 2020 Polepole: Kura ya maoni inaonesha Rais Magufuli anakubalika na wananchi kwa 90% na CCM inakubalika kwa 70%

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM komredi Polepole amesema katika kura ya maoni iliyofanyika kuelekea uchaguzi mkuu imeonyesha Wananchi zaidi ya 90% wanamkubali sana Rais Magufuli na zaidi ya 70% wanaikubali CCM.

Komredi Polepole amesema hayo jijini Mbeya alikoendesha harambee ya kuichangia CCM na kuvunja rekodi kwa kukusanya sh 160 milioni kati ya sh 156 milioni zilizobajetiwa

Wananchi wa Mbeya wamesema watampiga chini Sugu liwake jua au inyeshe mvua na kwamba watamchagua mgombea yoyote atakayeteuliwa na CCM

Chanzo: Channel ten tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti isiyo ya kiserikali Twaweza umebaini kuwa umaarufu wa Rais wa Tanzania, Dokta John Magufuli umeshuka kutoka asilimia 96 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 55 mwaka huu.

Asilimia 55 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani mwaka 2015. Kukubalika huku kumepungua kutoka 96% mwaka 2016, na 71% mwaka 2017.

Kiwango cha kukubalika kwa Rais kimeshuka kutoka kwenye rekodi ya juu kuwahi kuwekwa na Rais wa Tanzania mpaka rekodi ya chini tangu takwimu hizi zianze kukusanywa mwaka 2001.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amesema''umashuhuri wa Rais unaposhuka chini unaakisi kuwa hali ya maisha ya wananchi inazidi kuwa ngumu, umasikini, elimu , huduma za kijamii, changamoto za uwekezaji na wafanyabiashara kufunga biashara zao''.

Wakati huo huo serikali imekanusha dhana kwamba umaarufu wa Rais John Pombe Magufuli unapungua kama taasisi hiyo ya kiserikali inayojihusisha na utafiti nchini humo ya Twaweza inavyodai kwenye ripoti yake.

Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Bwana Humphery PolePole amesema Rais Magufuli bado ni maarufu sana nchini Tanzania kutoka na sera zake.Hasa katika uboreshaji katika masuala kama elimu, afya na miundombinu ya barabara na umeme.

Twaweza: Umaarufu wa Rais Magufuli umeshuka
2018
 
Ijumaa , 3rd Aug , 2018
Na Mwandishi wetu

Idara ya Uhamiaji inadaiwa kuishikilia hati ya kusafiria (passport) ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze ambaye aliiwasilisha mwenyewe baada ya kutakiwa kufanya hivyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi huyo wakati akizungumza na wanahabari leo Agosti 3, 2018 na kudai kuwa suala hilo halitawayumbisha, na wataendeleza majukumu yao kama kawaida.

"Niliombwa nifike Uhamiaji na kupeleka pasi ya kusafiria, nikatekeleza, lakini mpaka leo sijapata maelezo wala barua ya kwanini washikilie pasi yangu, niliomba pasi ya muda niende Nairobi kikazi lakini nilinyimwa", amesema Eyakuze.

Uhamiaji yatuhumiwa, hati ya Eyakuze | East Africa Television
 
MATOKEO YA MALAWI VIPI HAYA MANBO HAYATABIRIKI
 
Mwanaccm pekee aliyeshinda kwa kishindo kihalali kwa asimilia nyingi ni Jakaya Kikwete mwaka 2005.
Hata yeye mwaka 2010 alikuwa amechokwa kura zikapungua.

Utakuwa ni mchezo wa futuhi mtu ufanye mambo ya ovyo ovyo halafu uje ushinde kwa asilimia 90.

Only fools from L7 can buy that.
 
Back
Top Bottom