Uchaguzi 2020 Polepole: Kura ya maoni inaonesha Rais Magufuli anakubalika na wananchi kwa 90% na CCM inakubalika kwa 70%

Uchaguzi 2020 Polepole: Kura ya maoni inaonesha Rais Magufuli anakubalika na wananchi kwa 90% na CCM inakubalika kwa 70%

Ningeamini kama utafiti huo ungefanywa na chombo huru siyo hivi vyombo vya CCM! Anyway michango siyo kipimo cha kuonyesha umaarufu wa Magufuri.

CHADEMA wakisema wachangishe zitapatikana zaidi ya hizo.
 
Baada ya uchaguzi ndio utaelewa mwana Sacco's
Matokeo ya uchaguzi Tanzania na kukubalika ni vitu viwili tofauti. Ukikubalika na polisi na tume huna haja ya kukubalika na wananchi.
 
Cha kusitaajabisha ni kwamba Sample ilichukuliwa Lumumba wote wana CCM wakamkubali mwenyekiti kwa 90% waoo wenyewe wakajikubali kwa 70% akili ndogo kabisa ndo maana amesema atawaka tu kwenye kura za maoni
 
Utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti isiyo ya kiserikali Twaweza umebaini kuwa umaarufu wa Rais wa Tanzania, Dokta John Magufuli umeshuka kutoka asilimia 96 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 55 mwaka huu.

Asilimia 55 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani mwaka 2015. Kukubalika huku kumepungua kutoka 96% mwaka 2016, na 71% mwaka 2017...
Huyu jamaa kesi yake iliishia wapi ?
 
Kila mtu anamdomo lkn hiyo kura ya maoni imesajiliwa ofisi ya takwimu?
 
Utafiti umeufanyia wapi?vipi mkurugenzi Wa Twaweza mmeshamrudishia passport yake.?
 
Needless to read. Kwa hiyo ndivyo ccm walivyokubaliana na tume kuwa iwe hivyo. Maanake tayari ccm wana matokeo yote kibindoni.
 
Sasa ni kipi kinamuogepesha kuruhusu TUME HURU!? Na hii sample yake ilikuwa ni ya ukubwa gani na katika mikoa ipi?


Mkuu, hayo ndiyo maelekezo yanatolewa kwa Tume ya Uchaguzi. Hawatakubali Yohana apate 57 %...... Unless huyo mtu hajipendi.
 
Mwanaccm pekee aliyeshinda kwa kishindo kihalali kwa asimilia nyingi ni Jakaya Kikwete mwaka 2005.
Hata yeye mwaka 2010 alikuwa amechokwa kura zikapungua.

Utakuwa ni mchezo wa futuhi mtu ufanye mambo ya ovyo ovyo halafu uje ushinde kwa asilimia 90.

Only fools from L7 can buy that.
Hata wakipiga kura mapolisi watupu hafiki hata 50%. Maigizo hayana mvuto tena.
 
Sasa ni kipi kinamuogepesha kuruhusu TUME HURU!? Na hii sample yake ilikuwa ni ya ukubwa gani na katika mikoa ipi?

Uoga alionao kurubusu tume huru ni ishara kuwa anajua hakubaliki
 
Back
Top Bottom