Polepole: Muda wowote kuanzia sasa naenda kuyataja magazeti makubwa Mawili ya ‘hovyo hovyo‘ nchini Tanzania

Polepole: Muda wowote kuanzia sasa naenda kuyataja magazeti makubwa Mawili ya ‘hovyo hovyo‘ nchini Tanzania

Habari wanajamii.....leo katika redio ya magic ( redioccm)..Polepole alikuwa live na amesikika akilalamikia magazeti mawili ambayo hayaandiki habari za ccm bali wapinzani ndio wanaandikwa Ameenda mbali na kudai watayashitaki
Hii wadau imekaaje.
Hivi hajakiona "kijarida" chao cha Tanzanite, jinsi kinavyowachafua watu walio na heshima zao??

Kwake yeye chombo cha habari kinachoeleza ukweli wa mambo yanavyoendelea hapa nchini, ndiyo chimbo kinacholeta uhochezi na kuwa wanatumika na mabeberu!

Wanataka nchi nzima tujiunge na ile "Praise and worship for Magufuli"

Hata kama watawatumia Polisi "wao" kuwadhibiti wapinzani, hilo jambo halitakuja fanikiwa nchini Tanzania
 
Polepole kaanza kulewa madaraka na kuzani watanzania ni wajinga hawajui magazeti ya hovyo kuwa ni Jamhuri na Tanzanite
angalia aibu hii
 

Attachments

  • Apandacho mtu ndicho atakachovuna ( 268 X 480 ).mp4
    370.1 KB
Tatizo polepole anawadharau watanzania kawaona ni wajinga kupindukia hawajui ni magazeti gani ya hovyo yasiyo na Tija kwa Taifa, polepole muogope mungu na pia ujue watanzania wanaumia na dharau zako dhidi yao na endapo utafanya udikteta kwa magazeti pendwa na kuyaacha magazeti ya kishetani Tanzanite na menzake ya hovyo ujue laana ya wananchi itakuandama vilivyo ingawa unajivunia kamati za ufundi toka kijijini kwenu.
 
Hivi hajakiona "kijarida" chao cha Tanzanite, jinsi kinavyowachafua watu walio na heshima zao??

Kwake yeye chombo cha habari kinachoeleza ukweli wa mambo yanavyoendelea hapa nchini, ndiyo chimbo kinacholeta uhochezi na kuwa wanatumika na mabeberu!

Wanataka nchi nzima tujiunge na ile "Praise and worship for Magufuli"

Hata kama watawatumia Polisi "wao" kuwadhibiti wapinzani, hilo jambo halitakuja fanikiwa nchini Tanzania
Tatizo kubwa ni dharau polepole amewadharau watanzania kwa kiwango kibaya sana, anachokiamini yeye hujiona ni kimetoka mbinguni kwa mungu, hawezi kuona vijarida vya kijinga jinga kama Tanzanite na vyenzake vya musiba kaamua kuwakomoa wenye magazeti pendwa kwa vigezo vyako binafsi visivyo na Tija yeyote.
 
Yaani huyu jamaa alidhani kumnunua Kalisti ni jambo kuuuubwaaaa , kumbe ni sawa na kupiga bomu mochwari !

Poor Polepole !
Kapiga cha juu kapata 10% kwenye huo ununuzi huko Arusha kalewa tamaa na sifa kaamua kuja na vioja pasipo kutambua kuwa wananchi wanamchora tu.
 
Polepole muogope mungu hata kama unatumwa kuwakomoa watu lakini Akili za kuambiwa uwe unazichanganya na za kwako
 
Polepole ni kiboko ya Wapinzani anawakimbiza wamepoteana
Kamkimbiza nani? Kiboko ya nani? Wamepoteana wapi? angekuwa na nguvu angehangaika kuwaonea kuwakomoa wenye magazeti pendwa? Aache kila gazeti liwe huru kufanya wajibu wake kwani watanzania siyo wajinga wanaujua ukweli wote.
 
Naona sasa mmeamua hata huo mfumo Wa chama kimoja mmeona hautoshi mnataka kuja na mfumo Wa kila kitu PEKE YENU !
 
Katibu mkuu ccm yupo kweli

Yupo ila alijipambanua kama kiongozi anayeamini kwenye siasa safi za ushindi wa kupitia box la kura. Ila amejikuta chama chake ndio kinaratibu siasa chafu za kunajisi box la kura, huku yeye ndio akiwa katibu mkuu. Yaani amekuwa ni kama sheikh aliyeingia kuuza kitimoto, je atawezaje kuendelea kuhubiri kuwa kitimoto ni haramu?
 
Pesa kweli ni sabuni ya roho, Humphrey amenawiri siku hizi hata ile sura ya grandpa inapotea.
 
Back
Top Bottom