Polepole: Muda wowote kuanzia sasa naenda kuyataja magazeti makubwa Mawili ya ‘hovyo hovyo‘ nchini Tanzania

Akizungumza mubashara kabisa leo asubuhi ndani ya kituo cha redio cha Magic FM ambacho pia kinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole amesema kwamba kuanzia sasa muda wowote ataenda kuyataja magazeti mawili makubwa aliyoyaita mwenyewe kuwa ni ya ‘hovyo hovyo‘ nchini Tanzania.

Sababu kuu ya yeye kuja na hili ‘tamko‘ ni kitendo cha magazeti hayo mawili makubwa nchini Tanzania kuacha ‘kuripoti‘ vizuri na kwa haki juu ya kuhama kwa aliyekuwa Meya wa CCM Arusha Lazaro kuja CCM.

“ Labda niwaambieni tu kama kuna mtu ambaye ndani ya CHADEMA alikuwa na umuhimu mkubwa, amekisaidia hicho Chama, amefanya makubwa na hata Uwezo wake wa Kiutendaji hadi Kiupeo ni mkubwa kuliko wengi walioko huko ni huyu Lazaro. Binafsi nilishtushwa sana kumuona amehamia kwetu na baadae nilianza kufurahi kwani nilijua kuwa kumpata Mtu kama Lazaro basi CCM tumepiga bao la kisigino. Lakini angalia namna haya magazeti mawili ambavyo yaliripoti juu ya ujio wake huyu aliyekuwa Meya wa Arusha akiwa CHADEMA. Hawajamtendea haki na wamemripoti kama tu ni mtu mwepesi mwepesi wakati anaweza akawa ana uwezo kuliko huyo anayewadanganya au hao wachache wanaowadanganya ndani ya hicho Chama “

Je, wewe unayahisi haya magazeti ni gani?

Namalizia kwa kutuma salamu zangu nyingi na za dhati kabisa kwa wakazi wapendwa wa Tabata Relini na Sinza Kijiweni.
Sasa kwani anawalazimisha wenye vyombo vyao vya habari waandike anachokitaka yeye? Huu nao ni udikteta. Anaweza kuamuru vyombo vya dola kuyafungia hayo magazeti.
Nilifurahi sana Magazeti yangu pendwa yaliificha hiyo habari ndani huko. Tena likisema habari nyingine halafu huko ndani akatajwa huyu aliyehitimisha safari ya kwenda alikokwenda. Bure kabisa Slow Slow na kweli anapaswa kuwa Slow.
Hivi Polepole anafikiri bado kuna mtu anashitushwa na mpinzani kuhamia CCM kwa siku za leo? Hizo ni zilipendwa.
 
Akizungumza mubashara kabisa leo asubuhi ndani ya kituo cha redio cha Magic FM ambacho pia kinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole amesema kwamba kuanzia sasa muda wowote ataenda kuyataja magazeti mawili makubwa aliyoyaita mwenyewe kuwa ni ya ‘hovyo hovyo‘ nchini Tanzania.

Sababu kuu ya yeye kuja na hili ‘tamko‘ ni kitendo cha magazeti hayo mawili makubwa nchini Tanzania kuacha ‘kuripoti‘ vizuri na kwa haki juu ya kuhama kwa aliyekuwa Meya wa CCM Arusha Lazaro kuja CCM.

“ Labda niwaambieni tu kama kuna mtu ambaye ndani ya CHADEMA alikuwa na umuhimu mkubwa, amekisaidia hicho Chama, amefanya makubwa na hata Uwezo wake wa Kiutendaji hadi Kiupeo ni mkubwa kuliko wengi walioko huko ni huyu Lazaro. Binafsi nilishtushwa sana kumuona amehamia kwetu na baadae nilianza kufurahi kwani nilijua kuwa kumpata Mtu kama Lazaro basi CCM tumepiga bao la kisigino. Lakini angalia namna haya magazeti mawili ambavyo yaliripoti juu ya ujio wake huyu aliyekuwa Meya wa Arusha akiwa CHADEMA. Hawajamtendea haki na wamemripoti kama tu ni mtu mwepesi mwepesi wakati anaweza akawa ana uwezo kuliko huyo anayewadanganya au hao wachache wanaowadanganya ndani ya hicho Chama “

Je, wewe unayahisi haya magazeti ni gani?

Namalizia kwa kutuma salamu zangu nyingi na za dhati kabisa kwa wakazi wapendwa wa Tabata Relini na Sinza Kijiweni.
Mkuu salamu zako kwetu wa Tabata Relini na Sinza Kijiweni zimefika!!!!
 
Habari wanajamii.....leo katika redio ya magic ( redioccm)..Polepole alikuwa live na amesikika akilalamikia magazeti mawili ambayo hayaandiki habari za ccm bali wapinzani ndio wanaandikwa Ameenda mbali na kudai watayashitaki
Hii wadau imekaaje.
 
Mwanachi na nipashe wamezidi wawafungie mapema wanaleta uchochezi wa wawazi wataleta maafa kwa taifa

State agent
 
Wayafungie tu kwani kwasasa tunajua kilakitu
 
Habari wanajamii.....leo katika redio ya magic ( redioccm)..Polepole alikuwa live na amesikika akilalamikia magazeti mawili ambayo hayaandiki habari za ccm bali wapinzani ndio wanaandikwa Ameenda mbali na kudai watayashitaki
Hii wadau imekaaje.
Yaani huyu jamaa alidhani kumnunua Kalisti ni jambo kuuuubwaaaa , kumbe ni sawa na kupiga bomu mochwari !

Poor Polepole !
 
Mwanachi na nipashe wamezidi wawafungie mapema wanaleta uchochezi wa wawazi wataleta maafa kwa taifa

State agent
Acha upumbavu wewe yaani huo vijarida vya jamhuri na Tanzanite? Hivyo ndivyo vijigazeti vya hovyo kupata kutokea nchini
 
Yaani huyu jamaa alidhani kumnunua Kalisti ni jambo kuuuubwaaaa , kumbe ni sawa na kupiga bomu mochwari !

Poor Polepole !
Polepole kaanza kulewa madaraka na kuzani watanzania ni wajinga hawajui magazeti ya hovyo kuwa ni Jamhuri na Tanzanite
 
Back
Top Bottom