Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Kumejitokeza wanaccm wanaoamini kuwa nchi hii ya wanaccm na wao wakisema sisi watwana tufuate. Musukuma anashiriki biashara za machinga Kariakoo amekuwa akiwatetea wamachinga akimtumia Polepole kumuunga mkono na kumshambulia Mkuu wa Mkoa Makalla.
Suala la wamachinga limeanzishwa na sisi wananchi tunaobughudhiwa na wamachinga mbele ya biashara zetu na pia watumiaji barabara wengine.
Polepole na Musukuma mjue na sisi wengine tutafika mahali tupambane na wamachinga wenu waondoke mbele ya biashara zetu, sisi kuwa na fremu za maduka si kwamba ni matajiri ila tuliamua kutimiza wajibu wetu kufuata sheria za nchi.
Polepole na Musukuma mwachieni Mkuu wa Mkoa atuondolee wamachinga wenu na mjue sisi pia tunazo familia zinazokula ugali na mchicha mara moja kwa siku tofauti na nyie mnaokula mara sita kwa siku, mjue hivi sasa kukaa ndani ya fremu ya duka kunahitaji uvumilivu wa ziada kwani mauzo yameshuka sana kutokana na CCM kushindwa kuujenga uchumi kwa zaidi ya miaka 40 mkisingizia mabeberu!
Indonezya ilitawaliwa kama sisi na hao mnaowaita mabeberu lakini wametutoka wako mbali sana huku nyie mmebaki kukomba kura, hicho ndicho muhimu kwenu.
HATUWATAKI WAMACHINGA WALIOZAGAA BARABARANI.