Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
- Thread starter
-
- #101
Unaungana na nani? kwanza niseme wako machinga ambao hawana tatizo kwa kua wako maeneo sahihi lakini wako machinga hata Kama ni ndugu zetu wamegeuka kuwa kero ni mtu mwenye upeo mdogo ndiye anaweza kusapoti.Machinga walio futa njia za waende kwa miguu au kupiga mabanda karibu kabisa na barabara unawaungaje mkono? Machinga wanaotandika nguo katikati ya barabara kariakoo na kuzuia fast movement ya watu na mzigo unawaungaje mkono? Bado sijaongelea watu waliopachikwa jina machinga ili Hali sio hawa ni watu walioacha fremu na kujenga vibanda vingi barabarani vyenye biadhaazinazofika hata milioni sita kwa kibanda sio tu wanakwepa kodi bali wanavuruga mipango miji.Hakuna anayeona wivu au kuwachukia machinga bila sababu after all watz 50%ni machinga tofauti ni style lakini hii style ya Sasa sio tu inatuvua nguo kwa wageni na wenyeji bali tunatengeneza kizazi kisichofikiri na kisicho na utaratibu.Ni hatari sanaMimi naungana nao, they are very right.
P
Kila kukicha wametumwa na mabeberuKumejitokeza wanaccm wanaoamini kuwa nchi hii ya wanaccm na wao wakisema sisi watwana tufuate. Musukuma anashiriki biashara za machinga Kariakoo amekuwa akiwatetea wamachinga akimtumia Polepole kumuunga mkono na kumshambulia Mkuu wa Mkoa Makalla.
Suala la wamachinga limeanzishwa na sisi wananchi tunaobughudhiwa na wamachinga mbele ya biashara zetu na pia watumiaji barabara wengine.
Polepole na Musukuma mjue na sisi wengine tutafika mahali tupambane na wamachinga wenu waondoke mbele ya biashara zetu, sisi kuwa na fremu za maduka si kwamba ni matajiri ila tuliamua kutimiza wajibu wetu kufuata sheria za nchi.
Polepole na Musukuma mwachieni Mkuu wa Mkoa atuondolee wamachinga wenu na mjue sisi pia tunazo familia zinazokula ugali na mchicha mara moja kwa siku tofauti na nyie mnaokula mara sita kwa siku, mjue hivi sasa kukaa ndani ya fremu ya duka kunahitaji uvumilivu wa ziada kwani mauzo yameshuka sana kutokana na CCM kushindwa kuujenga uchumi kwa zaidi ya miaka 40 mkisingizia mabeberu!
Indonezya ilitawaliwa kama sisi na hao mnaowaita mabeberu lakini wametutoka wako mbali sana huku nyie mmebaki kukomba kura, hicho ndicho muhimu kwenu.
HATUWATAKI WAMACHINGA WALIOZAGAA BARABARANI.
Vijijini wamebaki wazee tu vijana wote wako mijini kwenye umachinga.Ngoja tuone...
Mkuu Munjombe , nawaunga mkono,Mhe. Humphrey Polepole na Mhe. Joseph Kasheku Musukuma.Unaungana na nani?
Utaratibu upi?.Naunga mkono hoja, Wamachingwa watengewe maeneo yao. Lakini kwa vile waliruhusiwa kufanya biashara popote na rais wa nchi wa wakati huo, then wasifukuzwe kama mbwa, kama wahalifu kama vibaka, wasivunjiwe vibanda vyao na kuporwa mali zao, maadam mwanzo waliruhusiwa kufanya kiholela sasa wapangiwe utaratibu.
P
Mjini kumejaaMkuu Jidu La Mabambasi , sitetei kabisa the anarchy and lawlessness, wala Polepole na Musukuma, nao pia hawatetei, tunachosema ni, maadam waliruhusiwa kufanya biashara holela na popote, sasa mambo yamebadilika, wawe treated fairly . Msivanjie vibanda vyao, msiwapore mali zao, na muwatafitie mahali karibu na masoko kufanya biashara, muwapange vizuri, wajengewe vibanda vizuri standard na uniform wafanye biashara zao rasmi na sio holela.
P
Uchaguzi ukikaribia wote wapiga kura wao watarudishwa barabarani.Ndg 2024 au 23 jiandaeni kuona marundo yawatu barabarani nanje yamaduka yenu Kama kawaida kwasababu ya zigizaga zaccm kwenye mipango
Nyuma mbele mbele nyuma (huku kijijini kwetu kunawadudu fulani wamekaa Kama nyoka akifukuliwa najembe lang'ombe toka ardhini utaona akiguswa mbele anarudi nyuma bila kugeuka(hiyo ndo ccm