Polepole na Musukuma tuacheni na machinga wenu nasi tupumue

Polepole na Musukuma tuacheni na machinga wenu nasi tupumue

Sheria zipo mbona hazifuatwi kila kitu kimefanywa Siasa.
Kabisa na hili linakera haswa. Kama hamtaki wamachinga wafuate sheria kwanini wananchi wengine wafuate hizo sheria. Hili la wamachinga ni kama vile linatuambia hatuna serikali which is a pity.

Ukienda Lagos unaweza kudhani hakuna serikali namna lile jiji lilivyo chafu na wao walianza kama sisi tulivyoanza baada ya uchafuzi wa 2015. Hali kadhalika DRC ni kama hakuna serikali mambo ni holela kila kona. Wao pia walianza kama sisi tulivyoanza 2015 maana serikali za awamu zilizotangulia zote ziliweza kuwadhibiti na miji yetu kdg ilikuwa inatazamika. Ukitetea kikundi fulani cha watu kutofuata sheria na wengine pia hawatazifuata hizo sheria mwisho wa siku huwezi kuwaongoza wananchi wote.
 
Ni haki yako lakini nami pia ni haki yangu kufanyabiashara bila bughudha toka kwa wapigakura wenu mnaowatetea wakae mbele ya biashara zetu.
Nyie mnawaoana wamachinga kuwa wao ndio wanahitaji hela ya kula na watoto wao mkijua watoto wetu wanashushiwa na Mungu! Jinsi mnavyowatetea kwa sababu ya kura ndivyo nasi tunavyopata hasira ya kutaka kupambana nao, mnachokijenga mtakiona.

Hakuna haki ya kuvunja sheria mkuu.
 
Naunga mkono hoja, Wamachingwa watengewe maeneo yao. Lakini kwa vile waliruhusiwa kufanya biashara popote na rais wa nchi wa wakati huo, then wasifukuzwe kama mbwa, kama wahalifu kama vibaka, wasivunjiwe vibanda vyao na kuporwa mali zao, maadam mwanzo waliruhusiwa kufanya kiholela sasa wapangiwe utaratibu.
P
Acha kujitafutia umaarufu kwenye suala ambalo halihitaji sifa ila utekelezaji WA sheria!! Watu hawawezi kuishi Kama mifugo
 
Kama mashuleni na vyuoni wapo Sukuma Gang kwanini huku ukatae!
Ukikutana na msukuma jambo lake la kwanza akufanye uwe msukuma (mfano Hangaya), makabila yetu huwa hayana chifu mwanamke.
Sii kweli, machifu wanawake walianza siku nyingi since time immemorial, chifu wa kwanza mwanamke ni yule aliyemmegesha 'tunda', yule aliyekatazwa asile 'tunda' lile, aliletewa 'tunda' na akamegeshwa!.
 
Sio sawa kuwafurusha kama Mbwa
Mbona wengine wanafurushwa kama panya! Utakuwa ulikuwa Uswizi wakati wakazi wa Kimara wakifurushwa, wapo waliolala nje na vichanga vyao mwezi mzima. Fikiria mtoto anazaliwa tu anapata surubu! Akikua atakuwa nani kama si Kingai.
 
Mkuu Jidu La Mabambasi , sitetei kabisa the anarchy and lawlessness, wala Polepole na Musukuma, nao pia hawatetei, tunachosema ni, maadam waliruhusiwa kufanya biashara holela na popote, sasa mambo yamebadilika, wawe treated fairly . Msivanjie vibanda vyao, msiwapore mali zao, na muwatafitie mahali karibu na masoko kufanya biashara, muwapange vizuri, wajengewe vibanda vizuri standard na uniform wafanye biashara zao rasmi na sio holela.
P
Kwani sheria zinasemaje?

Sheria ya mipango miji inasemaje?

Ningekuona wa maana Kama ungekuwa unweka reference kutoka kwenye sheria kusindikiza unayozungumza!

Unaongea Kama layman
 
Polepole ningekuheshimu sana kama ungeachana ku deal na vitu vidogo vidogo kama hivi na badala yake ujikite kwenye KATIBA MPYA - Mbona zamani ulikuwa na busara sana nini kimekupata ndugu?



 
Polepole ningekuheshimu sana kama ungeachana ku deal na vitu vidogo vidogo kama hivi na badala yake ujikite kwenye KATIBA MPYA - Mbona zamani ulikuwa na busara sana nini kimekupata ndugu?




Kuwa na busara zote ila ujue ukijiunga na CCM tu, busara zote hutoweka! Tekinolojia ya mchina inawaharibu marafiki zao.
 
Pole sana mkuu...umeongea kwa uchungu Sana....I feel your pains....

Halafu wanatokea watu aina ya ndg.Polepole wanaongea Kama vile wako "ndotoni"..

Pathetic
Polepole akili huwaga kazikalia matakoni
 
Back
Top Bottom