Polepole na Musukuma tuacheni na machinga wenu nasi tupumue

Polepole na Musukuma tuacheni na machinga wenu nasi tupumue

Kwenye hili la wamachinga, hakuna unafki wowote, ni JPM ndie aliwaruhusu, hivyo wamachinga hawana kosa lolote. Waondolewe kistaarabu kwa utaratibu na kupangiwa maeneo mbadala na sio kuwavunjia usiku kama ile ya vingunguti.
P
Ruhusa ya JPM iliishia alipofariki kwani ilikuwa ruhusa ya mdomo na si sheria, vinginevyo tukubaliane kuwa itadumu mpaka yeye atakaporudi na kuitengua! Sikutegemea utasema hivyo.
 
Mkuu bado nakushangaa!
Lazima pawepo na change katika mindset.
Ati watafutiwe sehemu ya biashara
Ati wapangwe vizuri ili biashara zao ziende.
You are talking of impossibles here!
Kama biashara zingekuwa hivyo nani asingetaka kuwa machinga.
What does it take to be a machinga.
Hao wenye maduka wao kwa nini wasiende kufanya umachinga wakati huku wakiandamwa na kodi ya pango, TRA,Kodi ya Ardhi, jengo, kodi za wafanyakazi, umeme, maji na kuondoa uchafu n.k.
JK aliwajengea jengo pale Ilala, mpaka leo liko wazi-hakuna anayetaka gharama za biashara.

Tuwe realistic , hatuwezi ku rationalise machingaism, its lawlessness.
Nilishawahi fika Capetown,pale Central Park kama sijakosea,ukipanda juu kuna vibanda vingi sana vya wafanya biashara wadogo wadogo,pale wamejazana wakongo wanasuka,wabongo wananyoa na wabongo wengine wapo wanauza madawa ya kulevya na wizi😂😂😂
 
Naunga mkono hoja, Wamachingwa watengewe maeneo yao. Lakini kwa vile waliruhusiwa kufanya biashara popote na rais wa nchi wa wakati huo, then wasifukuzwe kama mbwa, kama wahalifu kama vibaka, wasivunjiwe vibanda vyao na kuporwa mali zao, maadam mwanzo waliruhusiwa kufanya kiholela sasa wapangiwe utaratibu.
P
Mbona huwa hamatetei wanaobomolewa nyumba za makazi na kulazimika kulala nje! Nyie lazima mnamasilahi na umachinga. Hivi hizo familia zinazolala nje mnaona haziteseki kuliko wamachinga wenu ambao mnakuwa tayari kuacha shughuri muhimu za maendeleo mnakaa mnawabembeleza machinga!
Mbagala na maeneo mengine toka uhuru hawana maji yanayofaa kwa matumizi ya binaadamu, haya ndiyo mambo muhimu.
 
Mi nakuekewa mkuu.
Siyo siri Magufuli hakuwa kada kinda kinda wa CCM.
Na tuseme wazi tu, ndio maana aliwa purge viongozi waandamizi wa CCM na kuwabeza viongozi waliopita ili kujenga CCM ya muelekeo wake.
Magufuli alidiriki kuwateua viongozi toka vyama vingine na kuacha wakereketwa wa chama, ali mradi wateuliwa toka vyama vingine wanaimba yale anayoyataka.
Mwalimu alianzisha msimamo wa Tujisahihishe katika chama, mwaka 1976/77 ili ku inculcate sense of rectifying political mistakes.
CCM isipoendesha ilani ya Tujisahihishe tutakuwa wanafiki.
Msimamo wa Machinga kwa chama ulikuwa na lengo la Magufuli kujipatia political base, nje ya chama.
Magufuli alitambua kazi aliyoipata kwenye uchaguzi wa 2015,na mwanasiasa yoyote anataka watu,na kiasili Magufuli alikuwa na chuki ya watu wenye hela au matajiri, kwa hiyo kwake hawa aliwaamini na kuwapenda
 
Mimi ni kada wa CCM na ni strategic communicator na strategic thinker, hivyo sio kweli CCM haina watu hao, inao tena wengi tuu wa kutosha, tatizo ni...
naomba nisimalizie, mwacheni JPM apumzike kwa amani. Lets handle with care hii issue ya machinga.
p
All issues concerning all people should be handled with care, but this one is too much, a wastage of time and manpower.
Linashusha heshima na uwezo wetu kwenye utawala bora.
 
Kumejitokeza wanaccm wanaoamini kuwa nchi hii ya wanaccm na wao wakisema sisi watwana tufuate. Musukuma anashiriki biashara za machinga Kariakoo amekuwa akiwatetea wamachinga akimtumia Polepole kumuunga mkono na kumshambulia Mkuu wa Mkoa Makalla.

Suala la wamachinga limeanzishwa na sisi wananchi tunaobughudhiwa na wamachinga mbele ya biashara zetu na pia watumiaji barabara wengine.

Polepole na Musukuma mjue na sisi wengine tutafika mahali tupambane na wamachinga wenu waondoke mbele ya biashara zetu, sisi kuwa na fremu za maduka si kwamba ni matajiri ila tuliamua kutimiza wajibu wetu kufuata sheria za nchi.

Polepole na Musukuma mwachieni Mkuu wa Mkoa atuondolee wamachinga wenu na mjue sisi pia tunazo familia zinazokula ugali na mchicha mara moja kwa siku tofauti na nyie mnaokula mara sita kwa siku, mjue hivi sasa kukaa ndani ya fremu ya duka kunahitaji uvumilivu wa ziada kwani mauzo yameshuka sana kutokana na CCM kushindwa kuujenga uchumi kwa zaidi ya miaka 40 mkisingizia mabeberu!

Indonezya ilitawaliwa kama sisi na hao mnaowaita mabeberu lakini wametutoka wako mbali sana huku nyie mmebaki kukomba kura, hicho ndicho muhimu kwenu.

HATUWATAKI WAMACHINGA WALIOZAGAA BARABARANI.
😍👍
 
Mbona huwa hamatetei wanaobomolewa nyumba za makazi na kulazimika kulala nje! Nyie lazima mnamasilahi na umachinga. Hivi hizo familia zinazolala nje mnaona haziteseki kuliko wamachinga wenu ambao mnakuwa tayari kuacha shughuri muhimu za maendeleo mnakaa mnawabembeleza machinga!
Mbagala na maeneo mengine toka uhuru hawana maji yanayofaa kwa matumizi ya binaadamu, haya ndiyo mambo muhimu.
Watetezi wa kweli wa haki za binaadam, tunawatetea wote ila humu jf watetezi ni wengi na threads ni nyingi hivyo zingine za wakati wanatetewa itakuwa wewe zilikupita. Mifano ya utetezi wa haki dhidi ya bomoa bomoa tulitetea
P
 
Mkuu Erythrocyte , hiki kitu kinachoitwa Sukuma Gang, is a hoax!, it doesn't exist in reality, it's just a make up of that mzushi wa Twitter lakini in reality hakuna kitu kama hicho.
P
Kama mashuleni na vyuoni wapo Sukuma Gang kwanini huku ukatae!
Ukikutana na msukuma jambo lake la kwanza akufanye uwe msukuma (mfano Hangaya), makabila yetu huwa hayana chifu mwanamke.
 
Back
Top Bottom