Polepole na Nape ni wajasiri, wamegoma kufa na siri moyoni, ndio maana wanasema ukweli



Kwa kweli tunawapongeza sana Nape na PolePole. Kufanya kosa siyo kosa, kosa ni kuendelea kufanya.

Kwa kweli ni lazima uwe kichaa au mwendawazimu, kwenda kushiriki huu uchafu wa CCM, wanaouita uchaguzi. Kwa sasa aduimkuu wa ustawi wa Tanzania, ni CCM.

Hakuna mwanafamilia wala ndugu yangu wa karibu anayeweza kwenda kushiriki huo ushetani.
 
Eti October tunatick, m@v!!! Mnifanye msukule hivi hivi najiona?
Ukatiki ili waendelee kufaidi nchi. Walishawaona watanganyika ni wajinga hawajitambui. This time ni kuwaachia hakuna kupiga kura
 
Ya leo imewapiga utosini. Lazima watatoka nje. Jeshi la mtu mmoja lakini makombora yake ni hatari. Tumuunge mkono Polepole kaonyesha uzalendo
 
Tatizo vyombo
 
Mamho ni mengi muda ni mchache tatizo watanganyika umelala usingizi mzito hili nalo litapita
Hapa viongozi wa Dini, taasisi za kiraia na kimataifa, Wanasheria waungane na wananchi kutibu hiki kidonda. Tuombe bunge la kimataifa itoe mwelekeo kwa raia liamshwe chapu.

MUDA WA RAIS UMEISHA AKAE PEMBENI KWANZA TUSAFISHE MATAKATAKA YOTE NA KUFLASHI VIRUSI VYOTE VYA CCM ILI TUINGIE KWENYE UCHAGUZI wa huru na hako.

Nape njoo utubu.
 
Philosophical thoughts by Bishop Benson Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)


WOTE TUKO NJIAPANDA: Tupande gari gani?

Humphrey Polepole ametuweka njia panda sote. Anayedhani hayuko njia panda, yawezekana tayari ni abiria wa gari la mbele. Tutafakari:

1. Kuna watu usipowasikiliza, ni hasara. Ukiwasikiliza ni hasara pia. Humphrey Polepole ni mmoja wao. Usipomsikiliza unakosa mengi. Ukimsikiliza, anakushawishi kutenguka katika basdhi ya misimamo yako. Chagua kwa hekima.

2. Nani ni bora? Shetani aletaye habari njema au malaika aletaye habari mbaya?
Tuangalie kwa makini vipa umbele vyetu:
-Mungu/Taifa/Chama
Vs
-Chama/Taifa/Mungu

Chagua kwa hekima.

3. Twaweza kumpuuza Humphrey Polepole. Je tutapuuza madhara ya kumpuuza? Chagua kwa busara kati ya kupuuza huku usiweze kupuuza madhara ya upuuzi wako.
Kama anasema uwongo anamdanganya nani? Mungu? Wananchi? Yeye mwenyewe?

4. Kama ni kweli tufanyeje? Kama ni uwongo tufanyeje? Kwa nini aliyoyasema yanafanana na imani na uzoefu wetu? Kwa nini wanaosema aliyoyasema ni uwongo hata wao wanajiona ni waongo?

5. Viapo vyetu viko njiapanda: kukiuka kiapo kwa kusema kweli au kutunza kiapo kwa kuficha ukweli? Tunapoapa twamwapia mwanadamu au Mungu? Tukishupaza shingo (Impunity), twamfanyia Polepole, Katiba, Katiba, wananchi?

6. Hatujui tumefikaje hapa. Tuna uwezo wa kujua tutokeje. Tulinde kura moyoni? Tutiki wakati imeishatikiwa? Tusubiri reform?
Tupige kura kuamua kama tuchague au tusichague?

Unyenyekevu si udhaifu
TURUDI MEZANI
UKWELI ULIOCHELEWA NI BORA KULIKO UWONGO UNAOFARIJI.
HAKUNA TOBA ILIYOCHELEWA
 
Awataje na watu wanaoteka na kuua raia wenzetu ili tuwashughulikie kwa mujibu wa sheria zetu.
 
Tuwe na katiba mpya kwanza ndo tuingie kwenye uchaguzi. Bila katiba mpya hili DUDE alilolisema Polepole haliwezi kuondolewa. Syndicate ya CCM, tume ya uchaguzi na Nida

Hata ungelinda kura usiku na mchana hutoboi
 
Well said. Polepole kashusha kombora. Hata Bi kilemba lazima atakuwa ameziona siku zake leo hata kama.zilishasimama.
 
Polepole anaachia moja moja ,najua atakapokuja tena atakuja na kubwa kuliko alivyokuja nayo , wenyewe watatafutana ,soon kelele ya October tunatick zitaanza kupungua.

Masikini Mama wa watu atajiondokea zake kwa haibu eeeh! Mungu Baba.
 
MaCCM ni majitu ya kishetani sana. Inasikitisha kuwa haya maibilisi bado yapo madrakani yanaendelea kuichafua nchi yetu ya Tanganyika. Mungu shuka haraka uje kuyaangamiza haya mashetani ya CCM.
 
Kuwa na subira, taratibu tutafika huko. Namba 9 wetu Gwajiboy anapiga jalamba ili aingie uwanjani. Stay tuned.
Bado siku 3 tu ateme cheche. Alitoa siku 10 za kufunguliwa kanisa.....bado siku 3.
 
Polepole anaachia moja moja ,najua atakapokuja tena atakuja na kubwa kuliko alivyokuja nayo , wenyewe watatafutana ,soon kelele ya October tunatick zitaanza kupungua.

Masikini Mama wa watu atajiondokea zake kwa haibu eeeh! Mungu Baba.
Polepole anapiga dozi kidogo kidogo, ili mgonjwa apone, lakini dozi ya jana ilikuwa kali sana. Mgonjwa mpaka sasa bado ana wenge la dozi.
 
MaCCM ni majitu ya kishetani sana. Inasikitisha kuwa haya maibilisi bado yapo madrakani yanaendelea kuichafua nchi yetu ya Tanganyika. Mungu shuka haraka uje kuyaangamiza haya mashetani ya CCM.
Shetani ana nafuu zaidi ya CCM na tume yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…