GE2025 Polepole ni mwana CCM wa itifaki na maslahi - Rostam Aziz

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wala huna haja ya kuijua sana CCM ili uikosoe...

Suala la kukiuka kanuni zao na wahuni kufanya maamuzi watakayo halihitaji mtu awe kaishi ndani ya CCM kwa miaka yake yote...

 
DP kampuni ya Dubai,hutoa huduma sehemu tofauti ikiwemo UK,rostam hajafikia hizo level
Na alichosema rostam ni kweli, polepole hana nasaba na CCM


Huko Uk na kwingineko, DPW hawana mikataba ya kishenzi kama huo alioutengeneza Rostam. Na kwenye mataifa hayo yote DPW haijawahi kupewa bandari mama, hata kwenye nchi moja, wanapewa bandari za ziada; siyo bandari kuu.
 
Rostam na Kikwete ndio waharibifu wakubwa wa Taifa hili. Wanamtaka Samia kwa nguvu zote kwa sababu wana uwezo wa kumtumia kadiri watakavyo, kwa manufaa yao.

Samia aingiwe na hekima asikubali kuendelea kutumika. CCM impate mtu strong ambaye hataweza kutumika na hawa waharibifu wakubwa, Jakaya na Rostam
 
Kusanyikeni tu na saiz kisha sema atakua hatoi taarifa maana akitoa taarifa mkata network ana mhujumu
 
'Roast la hamster'' hatimaye limeanza kucheuwa harufu ya viungo vikali vya Uajemi.
Mwenye kupeleka maelekezo kwa Godfather wa wahuni kavaa jezi kaingia uwanjani mwenyewe.
Polepole piga hapo hapo kwenye pressure points.
 

View: https://www.instagram.com/reel/DM5x8glx9yA/?igsh=MXJzaGFvcTl1ZXR3ZA==
Nimemsikiliza aliye wahi kuwa mweka hazina wa CCM na mbunge wa Igunga bwana Rostam Aziz ana mengi ya kusema kuhusu Humphrey Polepole.

Anasema hizi mila na desturi nzuri ndani ya chama zinaingelewa na mtu ambae hajawahi kuwa ndani ya CCM aliibuliwa tu na kupewa u katibu wenezi.

Kubwa zaidi kumbe Magufuli alifariki akiwa cha nchi taabani kiuchumi.!

====
Alichokisema Rostam Aziz, ni kuwa Humphrey Polepole sio mwana CCM wa kiitikani bali ni mwana CCM wa kiitifaki na maslahi. Kwa maelezo yake ni kuwa Polepole alikuwa hajulikani ndani ya CCM hadi mwaka 2015 ambapo baadae alipata uongozi. Kwa udogo wa uzoefu wa Polepole ndani ya CCM inampa mashaka Rostam Aziz kuwa anaweza kujua mila na desturi za CCM. Amekosoa kuwa Polepole hana Moral Authority ya Kuzungumza anayozungumza.

Rostam pia ameshutumu kuwa hizi ni kati ya athari ya kuwachukua watu na kuwaleta ndani ya chama chao ikiwa mtu hajalelewa katika misingi ya chama. Amesema nchi ilipokelewa na Samia ikiwa na hali mbaya kiuchumi, na Rais amefungua uchumi, hivyo kumkosoa Rais Samia ni wivu tu.
 
Chama makini ni vema kikawa kinapokea maoni ya kukikosoa:

Chama ni watu na watu huwa wanafanya makosa:

Chama kinachotaka kiwe kinasifiwa tu kinakosa hadhi ya kuitwa chama cha siasa:

Acheni watu watoe maoni yao kwa uhuru:

Kama ya uwongo yatapiga na kama ya kweli yatafanyiwa kazi:

Nchi haiwezi kwenda kwa kuisikiliza CCM tu:
 
Polepole ni kama popo vile. Kwanza uso hajulikani ni kijana au mzee. Pili afya yake yaonekana mgogoro. Tatu haijulikani kama ana familia au ni msela tu. Nako CCM aliletwa na Magufuli baada ya ya kushiriki bunge la Katiba.

Na wakati wa Magufuli ndiyo tuliona uvunjaji wa Katiba wa hali ya juu na kukandamiza demokrasia na uhuru wa maoni. Na kipindi hicho hakuthubutu kusema lolote kwa vile alikuwa kwenye top cream ya wanaoamua na kupanga hatma ya Tz

Huyu mtu hana lolote la kumchukulia serious
 
Ni kwanini wana CCM hawakuhoji Polepole alipopewa ukatibu wenezi ndani ya CCM, nafasi ambayo inamruhusu mtu aliyeishika kuwa na taarifa nyingi za siri ndani ya chama. Walikuwa wapi vijana walio waandaa kushika nafasi za uwongozi?
 
Nyumbu wa vyuma vimekaza, sasa hivi wanakula wanavimbiwa wanaanza kuropoka na kutukana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…