Uchaguzi 2020 Polepole ni wa kupuuzwa, eti CHADEMA haina hospitali, kwani Muhimbili ni ya CCM?

Uchaguzi 2020 Polepole ni wa kupuuzwa, eti CHADEMA haina hospitali, kwani Muhimbili ni ya CCM?

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi hakijawahi kuwa na Katibu Mwenezi hopeless kama huyu. Tunakoelekea kuna siku atasema barabara zote za Tanzania zinamilikiwa na CCM kama walivyojimilikisha viwanja vya michezo.

"Wanasema watatoa Bima ya Afya kwa Wananchi wote, niwaulize; Unaweza kutoa Bima ya Afya wakati huna Hospitali?." - Humphrey Polepole.

Hata kama ni propaganda fanya basi lkn ziwe na mantiki na zilete sense kwa wanaosikiliza, propaganda hizi za Polepole hata yule bibi kizee wa kijijini ambaye hakuuona mlango wa darasa hawezi kukubali ulaghai huu.
 
Tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi hakijawahi kuwa na Katibu Mwenezi hopeless kama huyu. Tunakoelekea kuna siku atasema barabara zote za Tanzania zinamilikiwa na CCM kama walivyojimilikisha viwanja vya michezo...
Huyo mpuuzi sijui alisoma shule gani hapa nchini, maana hatumii angalau point ya akili zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi hakijawahi kuwa na Katibu Mwenezi hopeless kama huyu. Tunakoelekea kuna siku atasema barabara zote za Tanzania zinamilikiwa na CCM kama walivyojimilikisha viwanja vya michezo...
Ukiona kelele zinakuzidi tengenezeni na ninyi kwa serikali/chama chenu kwani mnafail wapi?

kweli Chadema ni UTOPOLO tu.
 
Sijajua kwa nini unashangaa! Hata nchi mbona ni ya ccm hata sisi wametutawala wawezavyo, ukitaka ushahidi angalia tunavyofokewa na kugombezwa nchi nzima kama watoto, watu wakisimama mbele yake wanatetemeka tu, halafu tupo tu na hatuna la kufanya...haki zetu zote wamebinafsisha ikiwemo ya kuongozwa na viongozi tunaowataka sisi, tumeporwa mpaka sauti zetu, tumeporwa kila kitu, kifupi sisi ni watumwa nchini kwetu wenyewe.
 
Wewe ndio umemuelewa vibaya, huwezi kuwapa watu bima huku huna hospitali za kutosha ambazo watu wanaweza kwenda na kutimia bima zao.

Ulichoandika hapa juu, ndio mfano tosha jinsi Chadema inavyopenda kupotosha umma katika kila jambo.
Tunaambiwa serikali imejenga hospitali na zahanati kila kata, hizo ndizo wataanza nazo Chadema, au Chadema wakiingia madarakani itabidi wazinunue kwa vile zimejengwa na serikali ya CCM.
 
Back
Top Bottom