Uchaguzi 2020 Polepole ni wa kupuuzwa, eti CHADEMA haina hospitali, kwani Muhimbili ni ya CCM?

Uchaguzi 2020 Polepole ni wa kupuuzwa, eti CHADEMA haina hospitali, kwani Muhimbili ni ya CCM?

Serikali Isiyo top heavy maana yake nini?
Kama kuna meyor wa jiji ni kwa nini juu yake kuwe na DED, DC, DAS, DMO,DEO, na viongozi wote wa idara zote za serikali; na juu Yao tena RC, RAS,DRAS, na hao wengine wote kwenye mkoa!!!!!
Hawa wote wapunguzwe na wizara zipunguzwe kabisa! Milia iwe tu ile ya Mwalimu Nyerere ila kule vijijini kuwe na viongozi wengi na wazuri waliochaguliwa na watu bila rushwa!
 
Hospitali siyo lazima zote zijengwe na serikali tu hata watu binafsi wanajenga. Kukiwa na uhuru haki na maendeleo ya watu, hospitali, shule, barabara, hoteli, nyumba nzuri za watu zitajengwa! Tunataka system ya serikali inayoruhusu watu wajiamulie mambo Yao na serikali iwape backup! Na serikali

Ati unadai Tunataka system ya serikali inayoruhusu watu wajiamulie mambo Yao. Kioja hicho na si hoja. Kwamba hakuna uhuru na haki katika nchi hii?

Tunajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu kuwachagua wawakilishi wetu kwenye chombo cha maamuzi, huo siyo uhuru wa maamuzi?

Kwamba wewe na mimi tuko huru kwenda kusikiliza Sera za Mgombea. Naye mgombea yuko huru kunadi Sera za chama chake. Ifikapo tarehe ya kipiga kura, wewe na mimi tuko huru kwenda kwenye kituo cha kupigia kira. Hapo kituoni, wewe na mimi tutakuwa huru kumpigia kura mgombea tunayempenda.

JITAMBUE kwanza nafasi uliyo nayo ya maamuzi pale utakapompigia kura mwakilishi mwenye sifa za kukuwakilisha kikamilifu kwenye chombo cha maamuzi (Diwani - Halmashauri, Mbunge - Bunge, Rais - Serikali).

Au ni uhuru gani unataka?
 
Du, kweli wewe ni Quinine wa kuuliza hata maswali ambayo hayawezi kuulizwa na chekechea. Nimebaki nacheke kwa hicho KIOJA
Ni mfano kukuomyesha issue sio hospitali, hospitali zipo bali kinachotakiwa ni kuwakengea wananchi uwezo wa kulipia kupitia bima ya afya.
 
Ati unadai Tunataka system ya serikali inayoruhusu watu wajiamulie mambo Yao. Kioja hicho na si hoja. Kwamba hakuna uhuru na haki katika nchi hii?

Tunajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu kuwachagua wawakilishi wetu kwenye chombo cha maamuzi, huo siyo uhuru wa maamuzi?

Kwamba wewe na mimi tuko huru kwenda kusikiliza Sera za Mgombea. Naye mgombea yuko huru kunadi Sera za chama chake. Ifikapo tarehe ya kipiga kura, wewe na mimi tuko huru kwenda kwenye kituo cha kupigia kira. Hapo kituoni, wewe na mimi tutakuwa huru kumpigia kura mgombea tunayempenda.

JITAMBUE kwanza nafasi uliyo nayo ya maamuzi pale utakapompigia kura mwakilishi mwenye sifa za kukuwakilisha kikamilifu kwenye chombo cha maamuzi (Diwani - Halmashauri, Mbunge - Bunge, Rais - Serikali).

Au ni uhuru gani unataka?
Mkuu uhuru unaotafutwa sio wa kupiga kura tu, uhuru sehemu za kazi, uhuru wa kufanya biashara nk nk.
 
Wewe ndio umemuelewa vibaya, huwezi kuwapa watu bima huku huna hospitali za kutosha ambazo watu wanaweza kwenda na kutimia bima zao.

Ulichoandika hapa juu, ndio mfano tosha jinsi Chadema inavyopenda kupotosha umma katika kila jambo.
Nani aliyekwambia hatuna hosp za kutosha nchi hii?

Kwa hiyo sasa wenye bima na wasio na bima hawapati huduma za afya.?

Shida mnafanya propaganda bila kufikiria.
 
Siwezi kuamini kama kweli msomi kama huyo anaweza kuongea hayo. Nina mashaka yawezekana mnamlisha maneno
Huwezi kuwa msomi ukajiunga na CCM, wasomi walijitoa kwenda kuanzisha vyama vya Upinzani mwaka 1992 yakibakia makapi hadi leo. Halishwi maneno ni ya kwake mwenyewe au ya kutoka juu ambako nako hakuna kitu.
 
Nani aliyekwambia hatuna hosp za kutosha nchi hii?

Kwa hiyo sasa wenye bima na wasio na bima hawapati huduma za afya.?

Shida mnafanya propaganda bila kufikiria.
Hapo ndio mnawadanganya wananchi kwa kufikiri mkiwamwagia pesa, basi shida zao zote zitaondoka. Je, hizo hospitali unazozisema hapa zina x-ray, scanner au theatre za kutisha?

Kinachofanyika sasa ni kuongeza uwezo wa hizo hospitali kutoa huduma kwa ufanisi nchi nzima, kabla ya kufikiria bima gani iende kwa nani. Unampa mtu bima huku dawa, maabara, vyumba vya upasuaji, madokta na manesi hakuna, si mtakuwa mnawahadaa wananchi?
 
Tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi hakijawahi kuwa na Katibu Mwenezi hopeless kama huyu. Tunakoelekea kuna siku atasema barabara zote za Tanzania zinamilikiwa na CCM kama walivyojimilikisha viwanja vya michezo.

"Wanasema watatoa Bima ya Afya kwa Wananchi wote, niwaulize; Unaweza kutoa Bima ya Afya wakati huna Hospitali?." - Humphrey Polepole.

Hata kama ni propaganda fanya basi lkn ziwe na mantiki na zilete sense kwa wanaosikiliza, propaganda hizi za Polepole hata yule bibi kizee wa kijijini ambaye hakuuona mlango wa darasa hawezi kukubali ulaghai huu.
Amemaanisha hospitali walizojenga ama kusimamia ujenzi wake.

Kuwa na akili once in your lifetime basi khaa!
 
Hospitali siyo lazima zote zijengwe na serikali tu hata watu binafsi wanajenga. Kukiwa na uhuru haki na maendeleo ya watu, hospitali, shule, barabara, hoteli, nyumba nzuri za watu zitajengwa! Tunataka system ya serikali inayoruhusu watu wajiamulie mambo Yao na serikali iwape backup! Na serikali
haya ni mambo theoretical kabisa kwani tangu mwaka 1985 serikali ilirudisha sehemu za hospitali zilizokuwa zimetaifishwa na kuzifanya kuwa za binafsi tena, na kuhimiza hospitali za binafsi kujengwa lakini hakuna zilizojengwa kutoesheleza Tanzania yote. Miaka kwa miaka tukawa na tabia ya kwenda kutibiwa India; wakati mwingine kwa gharama za serikali na wakati mwingine kila mtu akijilipia binafsi kulingana na uwezo wake kwa vile hatukuwa na uwezo huo ndani. Ni muda sasa sijasikia watu kwenda kutibiwa india kwa wingi ule uliokuwapo nyakati hizo. Kuongea ni rahisi sana kuliko kutenda; halafu ni kwreli kuwa mwenye chuki huwa siyo objective hata siku moja.
 
Hapo ndio mnawadanganya wananchi kwa kufikiri mkiwamwagia pesa, basi shida zao zote zitaondoka. Je, hizo hospitali unazozisema hapa zina x-ray, scanner au theatre za kutisha?

Kinachofanyika sasa ni kuongeza uwezo wa hizo hospitali kutoa huduma kwa ufanisi nchi nzima, kabla ya kufikiria bima gani iende kwa nani. Unampa mtu bima huku dawa, maabara, vyumba vya upasuaji, madokta na manesi hakuna, si mtakuwa mnawahadaa wananchi?
Siyo kila mgonjwa anahitaji x-ray au kutibiwa moyo akiwa na bima atakwenda palipo na huduma husika.
 
Siyo kila mgonjwa anahitaji x-ray au kutibiwa moyo akiwa na bima atakwenda palipo na huduma husika.
Kwa hiyo hii bima mnasema hapa ni ya watu kuumwa vichwa na kupewa panadol?

Na lini Chadema itazijenga capacity huduma ya afya, au watu wakiwa na bima ndio mmemaliza mchezo. Sioni sera ya kujenga hospitali au kuzijengea uwezo wa kufanya kazi kiufanisi.
 
Back
Top Bottom