Mama katika hili ndipo ananitia mashaka uwezo wake, huyu ni mwana CCM, yeye ndiye kamteuwa halafu kutwa yuko kwenye mitandao kutoa mafumbo. Ok dogo analoweza kufanya kumchukulia hatua ndani ya CCM maana haijawahi kutokea au kama ilitokea mtu kwenda na msimamo wa mwenyekiti wa chama maana ndiye anabeba sera za chama kukosolewa hadharani wakati CCM sifa kubwa huwa wanajinadi mambo yao yanajadiliwa ndani ya vikao na ni kweli hilo limewafanya kuwa tofauti ila tunaona siku hizi wanakimbilia kwenye mitandao. CCM hawayaoni haya au ndio kuna A na B. Mimi nadhani kuna tatizo kubwa katika CCM na Mama kama kapwaya au watendaji wake katika CCM wamepwaya. Huko nyuma haya usingeweza kusikia ndani ya CCM utawekwa kikao kama hujaondoka na ugonjwa wa moyo.