#COVID19 Polepole: Watanzania tuendeleeni kutumia njia za asili kupambana na Corona

#COVID19 Polepole: Watanzania tuendeleeni kutumia njia za asili kupambana na Corona

Katibu mwenezi msitaafu wa CCM na mbunge wa kuteuliwa wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania bwana Humphrey Polepole amehoji ni kwa nini watanzania wanataka kuacha mbinu za asili zilizotusaidia mwaka jana kupambana na corona na tukaibuka na mafanikio makubwa kiuchumi na kijamii?

Bwana Polepole ametolea mfano wa nchi zote zilizojaribu kupambana na Corona kwa kufuata mfumo wa kimagharibi mwishoni wa mwaka 2020 ziliishia kupata ukuaji hasi wa uchumi kwenye nchi zao!

Polepole amesema ni Tanzania tu ndiyo iliyopata ukuaji wa uchumi chanya kwenye nchi zote za Afrika mashariki. Sasa kwa nini sisi watanzania tunaona aibu kujivunia hizo mbinu za asili? Amehoji mh Polepole.

Mwaka jana tulipambana na Corona kwa kutumia njia tatu.
1. Kumtanguliza Mungu mbele
2. Kufuata mbinu mbalimbali tunazoshauliwa na watalaamu wetu
3.Kuchapa kazi kwa bidii

Hivi aliyemwambia kumtegemea Mungu ni kwenye Corona tu ni nani? Mungu ni kila kitu, hata kwenye malaria mtegemee Mungu. Usiweke mipaka kwamba hapa na katika hili nitamtegemea Mungu ila hapa na hili hapana. Utakuwa unakosea ndugu yangu. Mungu ni yote katika yote
 
Waliokufa Kwa Corona waliotumia hizi mbinu za Kienyeji tunasemaje. Dada yangu alijufukiza, akala Nimcaf yet she died from Corona. RIP my sister. Hapa Tanzania tuseme tuu kuna Nguvu ya Mungu tusioielewa.
Hakuna nguvu yeyote mjomba Sema hakuna takwimu tu ila watu wanakufa kama kawaida
 
Mtu huumwi, kwenu hakuna aliyekufa hata mmoja, maisha yapo tu Kama zamani, Sasa unang'ang'ana na chanjo za nini? Ila kweli kufuatafuata huku mwishowe ujikute shimoni.
 
Kaangalie takwimu za world bank na NBS .

Jinga kabisa wewe
Nadhani akili pekee uliyoibakiza ni hiyo ya kutukana tu.

Takwimu ni za IMF 2020. Real GDP growth rate ya Kenya ilikuwa 1.93%; ya Tanzania ilikuwa 1.90%.

Ukitaka kujifurahisha unaweza kutumia zile za kupikwa, za Luoga.
 
Jinga kabisa wewe.

Lete page ya worldbank report
 
Corona virus inapona kwa immunity ya mtu mwenyewe - hili limehakikishwa kwa watoto na vijana - tatizo linakuja kwa wazee wa miaka 70+ pamoja na wale wenye magonjwa yemelezi - hawa tumesema ni lazima wapate chanjo haraka iwezekanavyo.

Corona virus kwa mtu kwenye afya mgogoro au magonjwa ya moyo hizo dawa za kienyeji ni lazima zidunde na hatimaye mgonjwa kufariki kwa kukosa hewa (mapafu kujaa maji)

Kwa hiyo taifa lifanye jitihana haraka sana za kuwachanja hili kundi lililo katika hatari...hizi siasa za mitishamba tuachane nazo kwenye suala la Corona.

Sasa badala ya kutumia mamilioni ya hela kuwekeza kwenye uchunguzi wa mitishamba ni kheri hizo pesa tukanunue dawa hasa hasa zahanati za kina mama wajawazito.

Tuachane na mzee wa V-eiteee, hana jipya kwa sasa !!
 
Corona ina miaka miwili sasa, hilo kundi unalolisema limepata madhara gani?
 
Mzee polepole ule unyakuo wa 2035 uliosema bado upo???
 
Hakuna haja ya kuteseka kuifuata wakati iko njiani inakuja na Dorothy Gwajima atapambana kuhakikisha Watanzania wote wanaipata
Si uifuate tu hiyo chanjo kama Mbowe alivyofanya?
 
Suala la kumtegemea Mungu katika kupambana na corona hakuepukiki. Ni ujinga na kiburi cha mwanadamu kudhani kwamba kila tatizo lipo ndani ya uwezo wa mwanadamu kusolve.

Mkuu wetu wa nchi awamu ya tano alilielewa hilo na neema ya Mungu ilitufunika na imeendelea kutufunika hadi leo hii. Wasiomwamini Mungu wapuuze tu, lakini kwetu sisi acha Mungu aitwe Mungu.
Then yeye ikamuua hiyo corona
 
Mwisho wa siku hii chanjo kuna ambao watahitaji zaidi na watalazimika kuchoma hata kama hawataki,kuna rafiki zangu wanatarajia kwenda australia mwakani mipaka ikifunguliwa lakini sharti la kwanza ni kuwa lazima wawe na hiyo certificate of vaccination,imagine watu kama hawa ukiwanyima chanjo means umewazuia kusafiri!
Huyo polepole pengine ye ndo kashafika hapa bongo maisha yamemnyookea ila asisahau kuna wengine wanataka kuvuka border wakatafute life huko kwenye nchi za wazungu na ili kufanya hivyo lazima wachome hizo chanjo!
Tukubaliane tu hizo chanjo lazima zije,kuna zitaowafaa,na zisiowafaa na ndo ikawa hiari!
Maisha hatufanani ndugu wajumbe!
 
Jinga kabisa wewe.

Lete page ya worldbank report
Kama una ndugu yako anayekupenda, ungemwomva akupeleke hospitali. Watu wengi wenye matatizo ya akili, huwa hamjitambui.
 
Kama una ndugu yako anayekupenda, ungemwomva akupeleke hospitali. Watu wengi wenye matatizo ya akili, huwa hamjitambui.
Hii ndiyo page ya world bank?
 
Mtu huumwi, kwenu hakuna aliyekufa hata mmoja, maisha yapo tu Kama zamani, Sasa unang'ang'ana na chanjo za nini? Ila kweli kufuatafuata huku mwishowe ujikute shimoni.
Mawazo ya kijima kabisa haya.
 
Back
Top Bottom