Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

....[/QUOTE]
CHADEMA wanapoitisha maandamano tena ya amani kwa kufuata misingi ya demokrasia ni haki yao,viongozi wa chadema hawajashika madaraka kuweza kuchukua hatua dhidi wauaji(polisi) nadhani hawapaswi kulaumiwa labda wakichukua nchi 2015.
 
Mwingereza alituletea (Uhuru?) kwenye kisosi. Hilo ni kosa la kizazi cha mwanzo. Uhuru hupiganiwa. Ndo maana Mkoloni Mweusi yupo tayari kuua kwa kuwa anajuwa fika kuwa mwanadamu atadai na kupewa chochote bure, lakini siyo uhuru. we are at war with our black colonial master.
 
CCM ni makaburu wengine Africa, Wanataka kuhodhi nchi kwa kutumia mabavu. Hatuwaogopi.
 
Mwingereza alituletea (Uhuru?) kwenye kisosi. Hilo ni kosa la kizazi cha mwanzo. Uhuru hupiganiwa. Ndo maana Mkoloni Mweusi yupo tayari kuua kwa kuwa anajuwa fika kuwa mwanadamu atadai na kupewa chochote bure, lakini siyo uhuru. we are at war with our black colonial master.
Huyu kaburu mweusi lazima aondoke.
 
suala la cdm kuitisha mikutano ni SAHIHI katika nchi yoyote inayofuata mfumo wa vyama vingi. Labda hilo la uongoz wa cdm kuchukua au kutochukua hatua ndo tujadili.

kaka mkuu nimekusoma, sasa basi umefika muda viongozi wa cdm wachukue hatua zinazostahiki hasa
 
[h=2]Mauaji tena[/h]


Na Ashton Balaigwa



28th August 2012







Polisi watumia nguvu kuvunja maandamano
Wengine wajeruhiwa, risasi, mabomu vyarindima




Moshi ukiwa umetanda baada ya bomu la machozi kutupwa katikati ya barabara ambayo wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikuwa wakipita kwa maandamano kuelekeea kwenye mkutano wa hadhara mjini humo jana. Kulia ni gari lililokuwa limebeba baadhi ya wanachama wa chama hicho.


Mji wa Morogoro na viunga vyake jana uligeuka kuwa uwanja wa mapambano hali iliyolazimisha shughuli mbalimbali kusimama kwa saa kadhaa, zikiwemo ofisi na maduka kufungwa kwa muda baada ya Jeshi la Polisi kurusha mabomu ya machozi na risasi za moto ili kudhibiti maandamano ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mapambano hayo yalisababisha kifo cha mtu mmoja na wengine wawili kujeruhiwa sehemu mbali mbali za miili yao baada ya kupigwa risasi na askari wa Jeshi hilo wakati wa kudhibiti maandamano hayo yaliyokuwa yakipita katika mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro kabla ya kuelekea katika uwanja wa mkutano wa Operesheni Sangara uliokuwa ukifanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kiwanja cha Ndege.

Jeshi la Polisi lilitumia nguvu kubwa kuzuia maandamano ya Chadema yaliyoanzia katika eneo la Lupira jirani na kituo kikuu cha stendi ya mabasi Msamvu kuelekea katika eneo la mkutano.

Aliyeuawa hakuwa mwandamanaji na alitambuliwa kwa jina la Ally Nzona muuza magazeti wa mjini hapa.

Marehemu anadaiwa kupigwa risasi na polisi katika eneo la nyuma ya kichwa akiwa anasoma gazeti katika meza aliyokuwa akitumia kuuzia magazeti.

Waliojeruhiwa katika vurugu hizo walitambuliwa kwa majina ya Frank Mbalimba, mkazi wa Msamvu na Hashim Seif.

Ndugu wa marehemu aliyejitambulisha kwa waandishi wa habari kwa jina la Ally Athumani, alisema wakati akiwa amekaa na ndugu yake katika eneo la kwa Bene, waliona gari la polisi aina ya Land Rover Defender lenye rangi nyeupe likiwasogelea na ghafla askari mmoja alivyatua risasi iliyompata mwenzake katika eneo la nyuma ya kichwa (kichogo).

“Sisi hatukushiriki katika maandamano, tulikuwa tunajitafutia riziki yetu kwa kuuza magazeti ndiyo maana hata walipotusogelea hatukuona sababu ya kuwakimbia, ghafla askari alitupa risasi ikampata ndugu yangu, masikini wamemuuwa ndugu yangu,” alisimulia Athumani huku akilia.

Kabla ya Jeshi la Polisi kuanza kufyatua risasi majira ya saa tano asubuhi, walimzuia kwa muda mkuu wa Operesheni Sangara wa Chadema, Benson Kigaila, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Zanzibar, Hamad Yusuph, hali iliyoamsha ari ya vijana kutoka maeneo mbali mbali kuingia barabarani wakiwa na mabango ya kulaani hatua hiyo.

Miongoni mwa waliokamatwa ni mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Abdallah Khamis, ambaye alikuwa akipiga picha za matukio hayo, ingawa baadaye aliachiwa.

Hata hivyo, baadaye kiongozi wa Polisi aliyekuwa katika eneo hilo alitangaza hali ya hatari na kuwataka wananchi watawanyike, amri ambayo haikutekelezwa na wananchi walioamua kuingia barabarani wakiwa na magari, pikipiki na baiskeli huku wengine wakitembea kwa miguu kuelekea katika eneo la mkutano.

Kutokana na hatua hiyo, askari waliokuwa katika magari zaidi ya 10, walianza kurusha risasi na mabaomu ya machozi hali iliyowafanya wananchi wakimbie kwa muda na kisha kurudi tena barabarani.

Hali hiyo iliwafanya askari waliokuwapo kuanza kuyasindikiza maandamano hayo kwa utaratibu hadi walipofika eneo alilokuwepo mkuu wao aliyetambuliwa kwa jina la Z. M Mukiko, ambaye aliwaamuru askari hao kuendelea na kamatamakata pamoja na kurusha risasi na mabomu.

Matukio ya kukamata kamata yaliendelea hadi kuwakumba wafanyabiashara waliokuwa pembezoni mwa barabara ya Kisunyale, wengi wao wakiwa ni wauza vyakula (baba lishe).

Jitihada za Jeshi la Polisi kuzuia maandamano hayo ilianza kufifia baada ya askari waliokuwa katika kazi hiyo kuishiwa mabomu ya machozi na kulazimika kutumia baruti pekee, hali iliyowafanya wananchi wazomee kwa kuimba “People’s Power”, risasi haziwezi kuzuia nguvu ya umma.”

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Godfrey Mtei, alipopigiwa simu kwa ajili ya kueleza idadi ya watu waliojeruhiwa na waliofariki, alisema kuwa alikuwa kwenye msiba hivyo hakuwa na taarifa rasmi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na wengine kujeruhiwa.

Kamanda Shilogile alisema kuwa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi ili kujua kama risasi zilizotumika kuua zilifyatuliwa na askari wake.

SLAA: POLISI WAMEUA DEMOKRASIA

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, alisema Polisi mkoani Morogoro limeitangazia dunia kuwa Tanzania hakuna demokrasia na kwamba sasa kuna jukumu la kupigania uwepo wa demokrasia nchini

Alisema hujuma za Polisi kwa Chadema zilianza siku nyingi na jana wamedhihirisha hujuma yao kwa kuamua kurusha risasi na kumuua Kijana Ally Nzona.

Akizungumza na umati wa wananchi katika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, Dk Slaa alisema baada ya amri ya Kamanda wa Polisi mkoani humo, Faustine Shilogile, askari walio chini yake wanasita kuchukua dhambi ya kufyatua risasi na mabomu kwa wananchi.

Alisema hata barua zinazoandikwa na polisi zinaonyesha kuwa ni watu wasiojua majukumu yao.

Alisema barua waliyoandika inaonyesha kama wametoa kibali cha maandamano wakati jukumu lao linatakiwa libakie kuwa ni la kulinda na siyo kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa.

Alisema Kamanda wa Polisi mkoani humo hajui hata madhumuni ya mandamano kuwa ni kuungwa mkono na watu, hivyo wanaposema watu wataacha kazi haileti mantiki katika akili ya kawaida.

“Hivi maandamano yanafanyiwa porini, hii ndilo tatizo la kuwa na viongozi wa kupachikwa pachikwa nami nina shaka nao kama akili zao zinafanya kazi sawa sawa kwa kuwa pasipokuwa na watu hakuna maandamano,” alisema Dk Slaa.

Alisema sheria ya kukataa maandanmano inaainisha sababu ambazo zinaweza kutatulika na kwamba kuwaambia barabara hazitoshi ni kuamua kufinya demokrasia.

ISSA: TUPIGE TAKBIR

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Said Issa Mohamed, akihutubia umati wa wananchi alisema asubuhi ya jana akiwa anazungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ilifikia wakati wakashikana mashati kwa sababu ya kutetea maslahi ya aliyowaita vibaraka wa CCM.

Akizungumza huku akitumia aya mbali mbali za Koran, Issa Mohamed alisema kama Jeshi la Polisi linatumia posho wanazopewa na watu wanaotaka kulinda nafasi zao za ubunge kwa nguvu ya risasi, basi yeye yupo tayari kumwaga damu kwa ajili ya Watanzania.

“Tunajua huyu kamanda anatumika nami ninawaambieni mwanafalsafa mmoja wa Kiarabu alisema kama ukiona mtu anafikishiwa elimu na hanufaiki na elimu hiyo basi mtu huyo apigiwe takbir nne kwa kuwa atakuwa hana tofauti na maiti, nami nawaambieni Morogoro msiwe hivyo,” alisema Mohamed Issa.

MNYIKA: POLISI, CCM WASHIRIKA

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alisema CCM baada ya kuona mbinu yao ya kuandaa kufanya fujo katika mikutano ya Chadema imejulikana, wameamua kushirikiana na Jeshi la Polisi kutekeleza mkakati wao wa mauaji.

Alisema mipango mingi iliyokuwa ikifanywa na CCM dhidi ya Chadema imekuwa ikijulikana na sasa wanaona njia sahihi ni kuwatumia makamanda wa Polisi wanaonunulika.

LISSU AAHIDI KUMFUATA SHILOGILE

Tundu Lissu, Mkurugenzi wa Haki na Sheria Chadema, alisema suala la kuandamana halijawahi kuwa kosa la jinai ambalo adhabu yake ni kifo, kama ilivyotokea kwa kijana aliyeuawa na polisi.

Alisema hakuna damu ya Mtanzania aliyeuliwa bure kuwa itasahaulika, hata kama hao wanaowaamuru polisi kwa kudhani wataishi milele.

Alieleza kuwa wanasheria watamfuata Kamanda Shilogile popote alipo iwe amevaa sare au amevua kwa ajili ya kuulezea umma wa Watanzania kwa nini alimuuwa Ally Nzona.

“Tunawaambia tutawafuata popote walipo watuambie kwa nini wameamua kumwaga damu ya Watanzania, vilio vyetu havitapita hivi hivi leo na hata kesho,” alisema Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema).

CHADEMA KUBEBA MSIBA


Wakati huo huo, Kamanda wa Operesheni kwenye vuguvugu la mabadiliko (M4C) itakayoifikisha chama hicho katika mikoa mitano, Benson Kigaila, alisema Chadema itachukua majukumu ya msiba wa Ally Nzona pamoja na kushughulikia matibabu ya waliojeruhiwa.




CHANZO: NIPASHE
 
.......[/QUOTE]

Moderators sijawaelewa kwa nini hii thread imeunganishwa na hizi nyingine. Mnaanza kunitia wasiwasi sasa.
 
Tatizo siyo polisi tatizo liko kwa wale wanao watumia. kwani polisi anafanya kazi km anavyoelekezwa na bosi wake.kitu kinachotakiwa kwa askari yeyote nikutii amri tu na sivinginevyo.tatizo liko kwenye matumizi namna unavyo watumia wewe km bosi wao.hakuna askari ambae anaweza kufanya kazi yoyote bila kuamliwa. vinginevyo anatakiwa ashitakiwe.tatizo liko kwa mabosi wao ambao wengi wanajuwa fika kuwa serekali ilioko madarakani ikiondoka lazima w ataondoka nayo.ili aendelee kuwepo madarakani nilazima ahakikishe anailinda serekali yake kwa gharama zozote.askari wa chini yeye hana tatizo lolote kwa sababu hakuna anachokipoteza ije serekali ya chama chochote kile, yeye atakuwepo tu.ukizingatia kuwa hakuna chama chochote kitakacho kuja na askari wake baada kupewa ridhaa Ya kuongoza dola,bali kitawatumia askari hawahawa waliopo.kinachotakiwa nikuiondoa sekali ya ccm madarakani kihalali ili askari watumike vizuri.
 
Tatizo siyo polisi tatizo liko kwa wale wanao watumia. kwani polisi anafanya kazi km anavyoelekezwa na bosi wake.kitu kinachotakiwa kwa askari yeyote nikutii amri tu na sivinginevyo.tatizo liko kwenye matumizi namna unavyo watumia wewe km bosi wao.hakuna askari ambae anaweza kufanya kazi yoyote bila kuamliwa. vinginevyo anatakiwa ashitakiwe.tatizo liko kwa mabosi wao ambao wengi wanajuwa fika kuwa serekali ilioko madarakani ikiondoka lazima w ataondoka nayo.ili aendelee kuwepo madarakani nilazima ahakikishe anailinda serekali yake kwa gharama zozote.askari wa chini yeye hana tatizo lolote kwa sababu hakuna anachokipoteza ije serekali ya chama chochote kile, yeye atakuwepo tu.ukizingatia kuwa hakuna chama chochote kitakacho kuja na askari wake baada kupewa ridhaa Ya kuongoza dola,bali kitawatumia askari hawahawa waliopo.kinachotakiwa nikuiondoa sekali ya ccm madarakani kihalali ili askari watumike vizuri.
 
......[/QUOTE]
kweli mkuu wanatutawala hovyo kwa sababu hatupata uhuru wa mezani wangetuheshim kama uhuru tungepata kwa kumwaga damu kama msumbiji,wenzetu wanaheshimika.
 
Mara nyingi maelezo na msimamo wa jeshi la polisi ni kwamba kwenye maandamano vibaka na watu wenye nia mbaya hutumia fursa ya maandamano kufanya mabaya yao. Kwangu msimamo huo wa polisi hauna nguvu. Nianavyo: Msimamo wa jeshi ungepaswa kuwa kama ifuatavyo:Iwapo maandamano yatafanyika askari watakuwa standby kuhakikisha maandamano hayo yanafanywa kwa amani na akitokea kibaka yoyote athibitiwe. Msimamo huo ungekuwa una maana na tija sana. Ila wanachofanya polisi ni wao kuzua fujo na ghasia isiyokuwa na sababu yoyote. Msimamo wa polisi wa kuingilia maandamano naona ni msimamo unaotoka kwenye utawala wa kikoloni wa kuzuia mikusanyiko na maandamano wakiogopa 'native unrest'. Police action ya Morogoro haikuwa justified kwa njia yoyote hata kidogo! Waandamanaji ambao hawakubeba silaha yoyote walifanya jinai gani mpaka risasi zifyetuliwe na watu kuuwawa?Namwomba IGP atoe tamko.
 
Sio siri kuwa Jeshi la polisi halina mvuto tena hapa nchini. Kumefikia wakati ukivaa sare za Polisi unajitangaza wazi kuwa wewe unatembea barabarani huku akili zako umeziacha nyumbani. Hakuna busara inayotumika katika kukabiliana na majukumu ya kazi zao.

Hakuna tofauti na wanyama wanaotumika katika kazi za ulinzi wanapoamrishwa kukamata mhalifu, wao wanachojua ni kutii amri ya bosi wao tu na si chochote. Ikumbukwe hawa Polisi wanaishi na raia mitaani. Jeshi hili linatakiwa kufanyakazi kwa kutumia akili nyingi kuliko nguvu. Hata hao raia wanaopigwa mitaani wanazo silaha za kukabiliana na Polisi tofauti ni kuwa raia wanatumia busara zaidi kuliko askari. Msitake raia nao watoke na silaha zao.

Kuna mifano mingi duniani ambayo wananchi wamechoka manyanyaso ya askari na wakafikia hatua ya kupambana nao na matokeo yamekuwa ni ushindi kwa wananchi licha ya kutumia silaha nyepesi kama mawe, mapanga, marungu nk.

Kitendo cha Polisi kuua raia wasio na hatia ni ushenzi unaoonesha ushamba wa Polisi wetu kwa kutii amri za mabwana zao pasipo kutumia hekima.

Wao wanajitetea kwa kusema vita havina macho! Kweli??? hiyo vita ni dhidi ya nani? Ni vyema basi amiri jeshi mkuu atangaze vita baina ya Polisi na raia lijulikane ili raia nao wajiandae kwa mapigano.

Mapinduzi ni suala la wakati, wakati umefika hamuwezi kuzuia hata kwa B52.
 
Nimejaribu kufwatilia.kila sehemu serekali ya ccm ilipopoteza uhai wa wananchi wake. Ccm ilishindwa kabisa hata kufanya mikutano mfano arusha..ukiona serekal
flani inaua wananchi wake ujue uhuru wa hao wananchi umekaribia....
 
As far as I know, polisisiem hawatumii "reason" bali wanatumia "memory".
 
R.I.P Ally Zona>>
Jeshi la polisi kwa Tanzania halina mvuto kwa Wananchi kwani hata yule Mwanausalama aliyejinyonga pale Morogoro alikwisha sema.
Halifai kuitwa jeshi la polisi hili liitwe Jeshi La Vibaraka walio Madarakani Tanzania.
R.I.P ALLY ZONA
 
Wana JF,

Kulingana na matukio ya kikatili (mauaji) yafanywayo na mapolisi nchini sababu kuu ni kuzuia maandamano ya wananchi kwenye mikutano ya CHADEMA, moja ya kazi zao polisi ni kulinda raia na mali zao lkn wamegeuka wao ndo wezi na wauaji wa raia wasio na hatia(rejea mauaji ya Arusha, Songea, Morogoro na sehemu nyingine).

Hivyo hadi hapo hakuna umuhim kua na jeshi la polisi kwani raia wanaweza kulinda haki zao na mali,hiki ni kipindi cha mabadiliko nchini suala lisiloepukika polisi wanapaswa kuzingatia hilo, nashangaa hata wakuu wa polisi (IGP)Wanakaa kimya ni kama wanaridhia yanayotokea.

Niwaase polisi kwani nao ni binadam kwa hiyo kifo kipo kwa wote wanapaswa kuacha kutumia madaraka vibaya nyakati hizi watz hawakandamizwi pia, risasi haziwezi kumaliza uma wote naamini risasi zitaua lkn wapo watakaobaki tena wengi, kibao kitageuka kwao polisi.

Je wewe mtanzania mtazamo wako ni upi kuhusu jeshi la polisi?

katika mikoa yote ambako mauaji ya raia wasio na hatia, wakuu wa polisi wa wilaya na mikoa wasidhani wako salama, lazima watapelekwa mahakamani kama siyo leo ni kesho. Ama kwa hakika utawala huu wa ajabu sana, wanakusanya kodi kutoka kwetu kwa lengo la kununua silaha za kutuangamiza sisi wenyewe! Kupitia kodi zetu, wanalipwa mishahara inayowafanya watupige mabomu, virungu, risasi za moto n.k.
 
Tatizo siyo polisi tatizo liko kwa wale wanao watumia. kwani polisi anafanya kazi km anavyoelekezwa na bosi wake.kitu kinachotakiwa kwa askari yeyote nikutii amri tu na sivinginevyo.tatizo liko kwenye matumizi namna unavyo watumia wewe km bosi wao.hakuna askari ambae anaweza kufanya kazi yoyote bila kuamliwa. vinginevyo anatakiwa ashitakiwe.tatizo liko kwa mabosi wao ambao wengi wanajuwa fika kuwa serekali ilioko madarakani ikiondoka lazima w ataondoka nayo.ili aendelee kuwepo madarakani nilazima ahakikishe anailinda serekali yake kwa gharama zozote.askari wa chini yeye hana tatizo lolote kwa sababu hakuna anachokipoteza ije serekali ya chama chochote kile, yeye atakuwepo tu.ukizingatia kuwa hakuna chama chochote kitakacho kuja na askari wake baada kupewa ridhaa Ya kuongoza dola,bali kitawatumia askari hawahawa waliopo.kinachotakiwa nikuiondoa sekali ya ccm madarakani kihalali ili askari watumike vizuri.

Wanatakiwa kutekeleza amri halali na siyo amri haramu. Amri ya kuua watu wasio na hatia siyo amri harali, Kwani akiamliwa akamuue mama au baba yake au hata ndugu yake awaye yeyote atatekeleza hiyo amri.
 
Back
Top Bottom