Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Ulishawahi kusikia mtu kaitisha maandamano ya fujo?
Maandamano ya amani ni jina, ambapo panaweza kutokea fujo.
 
Inaelekea kikao cha juzi cha Kamati Kuu ya CCM kiliazimia kuanza rasmi kutumia polisi kuvuruga mikutano ya CHADEMA.

Tukumbuke vile vile Slaa aliwahi kutangaza kwamba CCM ilikuwa na mkakati rasmi wa kuanzisha vurugu.

Wanasikitisha sana viongozi wa CCM. Wanaogopa majina yao yatatajwa kwenye rabsha la kutoroshea fedha nyingi mafichoni Uswizi. Papo hapo CHADEMA inawasambratisha kila kona. Wameamua wajaribu kutegemea mbinu za kinduli.
 
Hayati Baba wa Taifa Mwl. J K. Nyerere alishawahi kutoa ushauri na kuiambia serikali ya wakati ule walipokuwa wanawazuia watu kumbeba Mh. Mrema kwamba "Kama kuna watu wanaotaka kumbemba Mrema wakati yuko katika chati waacheni wambebe, na hata kama wananchi wataamua kusukuma gari yake kwa umbali mrefu waacheni msiwazuie...." Waungwana wote kabla ya kuingia katika mjadala huu na kujibu juu swala hili nawaomba mtafakari kwa makini na uangalifu mkubwa na kutoa sababu unazodhania Polisi ambao wanajiita USALAMA WA RAIA wanakataza maandamano hata kama wanahakikishiwa kuwa yatakuwa ya amani na utulivi, badala yake wanatumia nguvu kubwa SANA kwa gharama yoyote bila kujali chochote kuyazuia bila ya sababu za msingi na kuhatarisha amani na hata kusababisha vifo, inatisha inaniuma sana !!!!!!!!!!!!!!! pengine katika mjadala huu mtawasaidia POLISI ya tanzania

Tueleze kwanza maandamano ya amani yapi ? yana utaratibu upi ? na waandamanaji wanatakiwa wafanye nn ? ukiweka wazi hayo ndipo tukujibu murua hapa jamvini

 
Inaelekea kikao cha juzi cha Kamati Kuu ya CCM kiliazimia kuanza rasmi kutumia polisi kuvuruga mikutano ya CHADEMA.

Tukumbuke vile vile Slaa aliwahi kutangaza kwamba CCM ilikuwa na mkakati rasmi wa kuanzisha vurugu.

Wanasikitisha sana viongozi wa CCM. Wanaogopa majina yao yatatajwa kwenye rabsha la kutoroshea fedha nyingi mafichoni Uswizi. Papo hapo CHADEMA inawasambratisha kila kona. Wameamua wajaribu kutegemea mbinu za kinduli.

Weka ushahidi kwa haya uliyoyasema hapa jamvini wote tujue, km huna ni bora kunyamaza kuliko kuongea kwa kudhani kwani utakuwa sio GT

 
Tatizo siyo polisi tatizo liko kwa wale wanao watumia. kwani polisi anafanya kazi km anavyoelekezwa na bosi wake.kitu kinachotakiwa kwa askari yeyote nikutii amri tu na sivinginevyo.tatizo liko kwenye matumizi namna unavyo watumia wewe km bosi wao.hakuna askari ambae anaweza kufanya kazi yoyote bila kuamliwa. vinginevyo anatakiwa ashitakiwe.tatizo liko kwa mabosi wao ambao wengi wanajuwa fika kuwa serekali ilioko madarakani ikiondoka lazima w ataondoka nayo.ili aendelee kuwepo madarakani nilazima ahakikishe anailinda serekali yake kwa gharama zozote.askari wa chini yeye hana tatizo lolote kwa sababu hakuna anachokipoteza ije serekali ya chama chochote kile, yeye atakuwepo tu.ukizingatia kuwa hakuna chama chochote kitakacho kuja na askari wake baada kupewa ridhaa Ya kuongoza dola,bali kitawatumia askari hawahawa waliopo.kinachotakiwa nikuiondoa sekali ya ccm madarakani kihalali ili askari watumike vizuri.

Joyce Banda alipoingia tu alisafisha safu ya juu ya polisi,na pia swli ambalo mimi najiuliza siku zote na
inanifanya niwachukie polisi wote bila kujali ndugu yangu,wanapotutumwa kwenda kutawanya watu
kuna ulazima gani wa kutumia nguvu nyingi mpaka kufikia kuua wakati wanaopambana nao hawana hata
jiwe mkononi,kisa eti wanaandamana,inaingia akilini kuwa polisi kweli huwa wanatumia akili?hata kama
wametumwa na wakuu wao!!!!!!!
 
Tueleze kwanza maandamano ya amani yapi ? yana utaratibu upi ? na waandamanaji wanatakiwa wafanye nn ? ukiweka wazi hayo ndipo tukujibu murua hapa jamvini

Maandamano ya amani ni pale wananchi wanapoandamana kwenda mahali walipokusudia bila kufanya
vurugu zozote,yakiwa na utaratibu wa kulindwa na polisi bila kuwabugudhi waandamanaji hadi wafike
wanapokwenda kwa amani,na mwisho wanatakiwa waandamane sawa na maadhimio yao maana ni haki yao
kikatiba.
 
kupona kwetu ni kujilinda sisi wenyewe kwani tumetambua nia yao ni kuua na si kulinda tuache woga kwenye kutetea maslahi yetu na uhai,haipingiki kwamba kwa sasa adui wa mtanzania ni polisi,kwa sababu tumemjua adui yatupasa kujiandaa kumkabili,kama hawarejei misingi ya kazi yao wajihadhari kwani watz as soon tutachoka kupoteza wenzetu.
Well said kamanda,tunajiandaa kifikra na kiakili...adui yetu ni ccm na policcmagamba...
 
Wakati akielezea changamoto za sensa, msemaji wa Polisi Ndg. Chagenja amesema wamekamata watu zaidi ya 50 waliokuwa wanachochea watu wasijiandikishe kwa kisingizio cha uislamu, kwa kujua au kutokujua akahitimisha kuwa wanafanya uchunguzi lakini wanaamini kuwa hao si waislamu bali wanasiasa wa upinzani ambao walishasema kuwa watahakikisha nchi haitawaliki. Hii kauli ingetolewa na Nape sawa, lakini kutolewa na polisi, wakati waislamu walishaonyesha huo msimamo toka mwanzo na hawakusikilizwa ni kutowatendea haki wanasiasa wa upinzani na waislamu wanaopaza sauti zao lakini hazisikilizwi.

My take:
Nilitegemea polisi iwafanyie huo uchunguzi hao watuhumiwa ndiyo waje na tamko, kuja na kauli za mahaba ya kisiasa ni kuendelea kuridhalilisha jeshi la polisi, na kufanya watu waendelee kuamini ule msemo kuwa tuna polisisisiemu.

Source: Voice of America
 
Maoni ya Mhariri - Mwananchi 29 Agosti 2012.

KWAMBA askari polisi mjini Morogoro juzi walimuua kwa risasi kijana mmoja na kujeruhi wengine wawili wakati walipokuwa wakidhibiti maandamano ya wafuasi wa Chadema, ni taarifa ambazo zimetusikitisha sana na kutoa picha kwamba nchi yetu hakika bado ina safari ndefu kuelekea kwenye demokrasia ya kweli na utawala bora.

Tunasema nchi yetu bado ina safari ndefu kufikia vigezo vya demokrasia na utawala bora kutokana na matukio mengi makubwa tunayoshuhudia mara kwa mara katika sehemu kadhaa nchini. Aghalabu yamekuwapo matukio ya vifo na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu unaotokana na matumizi mabaya ya silaha na madaraka kwa upande wa Jeshi la Polisi. Mifano ya hali hiyo ya kusikitisha ni nyingi, lakini yatosha tu kusema hapa kwamba jeshi hilo kwa kiasi kikubwa limeshindwa kuelewa dhana ya ulinzi wa raia na haki ya mtu kuishi, ikiwa ndiyo dhima na dira kuu inayoliongoza jeshi hilo.

Yapo maeneo ambayo jeshi hilo limefanya vizuri na sisi tumekuwa msitari wa mbele kulimwagia sifa kila linapostahili kupongezwa. Lakini jeshi hilo limelaumiwa kwa mambo mengi ambayo hatuwezi kuyaorodhesha yote katika safu hii kutokana na ufinyu wa nafasi. Moja ya malalamiko makubwa ambayo yamekuwa yakielekezwa kwa jeshi hilo ni jinsi ambavyo limekuwa likivinyanyasa vyama vya upinzani na kuegemea kwa chama tawala. Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa siasa za vyama vingi nchini, Jeshi la Polisi limekuwa halionekani kuvitendea haki vyama vya upinzani na limekuwa linavunja sheria ya mwaka 1992 ambayo ilianzisha vyama hivyo.

Kwa mfano, jeshi hilo limekataa kuelewa au kutambua kwamba sheria hiyo ya vyama vya siasa haitoi mamlaka kwa jeshi hilo kutoa vibali kwa vyama hivyo kufanya shughuli za siasa, yakiwamo maandamano, mikutano ya ndani na ya hadhara na shughuli nyingine zozote za kisiasa. Sheria inasema kuwa, ili shughuli hizo zifanyike kwa amani na utulivu, lazima vyama hivyo vilitaarifu rasmi Jeshi la Polisi ndani ya saa 48 kabla ya kufanyika kwa shughuli hizo ili jeshi hilo litoe ulinzi. Lakini katika hali ya kushangaza, jeshi hilo limejipachika mamlaka ya kuratibu shughuli za vyama hivyo kwa kutoa au kukataa kutoa vibali vya kufanyika kwa shughuli hizo.

Swali ambalo limekuwa likiulizwa na wananchi wengi ni kuhusu sababu za jeshi hilo kutoa vibali pasipo pingamizi kwa vikundi vinavyoandamana au kufanya mikutano ya hadhara kuipongeza Serikali na viongozi wake? Kama kweli ajenda ya jeshi hilo siyo ya siri na inaendeshwa kwa dhamira safi, inakuwaje halifanyi hivyo kwa vyama vya upinzani ambavyo vimesajiliwa kisheria au vikundi vya wanaharakati vinavyotetea haki za kijamii? Inakuwaje basi vyama vya upinzani na vya kiharakati vikataliwe kuendesha shughuli zake kwa kisingizio cha kutokuwapo polisi wa kutosha kulinda shughuli hizo, lakini polisi wa kusha, tena wenye magari yaliyosheheni silaha za kivita wanapatikana kuzuia shughuli hizo zisifanyike?

Badala ya kulikemea jeshi hilo kwa kuvunja sheria na kukandamiza demokrasia, chama tawala na Serikali yake mara zote vimekuwa vikikaa kimya, huku vikichekelea pembeni na kuliacha jeshi hilo likitekeleza kile kinachodaiwa na vyama vya upinzani kwamba ni kutekeleza maagizo kutoka juu. Pengine ndiyo sababu kila mara jeshi hilo linaposababisha vifo vya raia kwa kisingizio cha kudhibiti maandamano ambayo hayana vibali vya polisi, Serikali hujitokeza na kulipongeza jeshi hilo kwa kusimamia sheria.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa jana. Akizungumzia tukio la Morogoro ambapo juzi mji huo na viunga vyake viligeuka uwanja wa mapambano, ambapo polisi waliua mtu mmoja kwa risasi wakati wakidhibiti maandamano ya wafuasi wa Chadema, Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi alisema polisi walikuwa wanatekeleza wajibu wao, huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa kufuata sheria.

 
Nimesoma mahali, kumbe Afande Saidi Mwema ni shemeji wa nanii!,

Kiukweli, ukimuangalia Saidi Mwema usoni, unamuona wazi, he is not brutal as opposed to Mahita, hii inamaanisha, genuinily anachukizwa na brutality ya vijana wake, swali linabaki ni what is he doing!.

Pasco.
 
Nimesoma mahali, kumbe Afande Saidi Mwema ni shemeji wa nanii!,

Kiukweli, ukimuangalia Saidi Mwema usoni, unamuona wazi, he is not brutal as opposed to Mahita, hii inamaanisha, genuinily anachukizwa na brutality ya vijana wake, swali linabaki ni what is he doing!.

Pasco.

Pasco believe it or not, IJP Mwema ndo kalibadilisha jeshi na kuwa friendly mpaka tunawasema hivi. Na amefanya haya yote kuwaokoa asakri wa jeshi la polisi kwa kuamini kuwa hakuna aliye juu ya sheria na iwapo askari wataendeleza ubabe wa kikoloni, ipo siku wataangukia kwa wananchi waliokombolewa, watashitakiwa na kuburuzwa mahakaman.

siku zote amekuwa akisistiza kila mtu bila kujali nafsi uliyonayo kutii sheria. mi nampenda Mwema, he is good
 
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]HAPANA! Hizi siasa zinazoambatana na vifo, ni za wapi nyie ndugu? Nasema hivi mumeona ukimwi, ajali za barabarani na malaria havijawatoa machozi ya kutosha hadi tunafikia huko kwa kuuana kwenye maandamano?

Nasema hapana! Haya mambo mengine utadhani tuko Baghdad au Chechnya ya enzi hizo.

Siasa ndizo zifike mahali tuanze kunyofoa uhai wa watu wetu? Jamani tutajifunza lini?
Kwani hamnielewi ninazungumza nini? Juzi-kati si nafsi ya mtu asiye na hatia imepotea wakati polisi wakipambana na waandamanaji wa kile kinachoitwa Movement for Change? Hapana, haikubaliki na haitakubalika. Siasa zenu kama zinatudhuru mwisho wa yote mwataka mumtawale nani?


Nani kasema mabomu na risasi au ubabe unaweza kupambana na ari na nguvu ya nafsi? Naapa mnashindwa kusoma alama za nyakati.
Ukiacha hizi sababu za kueleweka kwamba mikutano na maandamano nyakati za kuhesabu watu sio sawa, hizi nyingine zinazotolewa mbona haziingii akilini jamani? Eti hamkusikia watu wenye akili zao wakisema barabara za Morogoro ni finyu hivyo haiwezekani watu kuandamana? Labda kama Morogoro imeumbwa upya. Mwataka tuamini kabisa kwamba hayajawahi kutokea maandamano na hayatatokea huko Morogoro? Jamani tuwe ‘siriazi' kwenye mambo mengine na tukitoa sababu basi ziwe na mashiko.
Ubabe huu sasa ndio umeondoa roho ya mja wa Mola. Hebu fikiria kama huyo aliyefariki ni ndugu yako. Nakuuliza wewe uliyeamua kuvunja maandamano hayo, hivyo kusababisha vurugu.


Kuna sababu nyingine inayochekesha ingawa matokeo yake ni huzuni.
Eti unaambiwa hakuna askari wa kutosha kulinda amani, lakini pindi waandamanaji wakiamua kuendelea na dhamira yao utashangaa hao askari wametoka wapi.
Mbona mnaanza kutufunza mazoea ya siasa zinazoambatana na milio ya risasi na mabomu? Nauliza hivi, siasa lazima zihusishe nguvu kiasi hiki? Mbona tulishazoea siasa ni sera lakini mwaendeleza yale yale tuliyoyalilia siku za nyuma. Mmesahau siasa hizi zimewahi kuua makumi ya watu huko visiwani na ikafikia mahali tukazalisha wakimbizi? Hayo bado hamyaoni? Mnasahau haraka namna hiyo?


Ukiacha hayo ya Wazanzibari yaliyowafanya hadi wakasusiana misiba na pilau, mbona tushaona siasa zetu zikianza kunuka damu? Hapana, wote tuseme hapana kwenye hizi siasa zinazoambatana na silaha.


Hizi siasa za silaha wacha tu tuendelee kuzisikia huko Mogadishu ingawa na wao twawaombea warudi kwenye amani.
Nauliza kama hapa ni miaka mitatu kabla ya uchaguzi tunaona hizi vurugu tutarajie nini ikifika mwaka wa uchaguzi?


Hivi nguvu hizi wanazotumia polisi kuzuia waandamanaji wangezitumia kudhibiti majambazi mbona tungekuwa tunalala milango wazi! Nasema simo kote huko!
Wengine tulishaanza kusahau haya mambo ya ufurukutwa, ukereketwa na uwashwa washwa? Watu tulishasahau kabisa yale mambo ya ngunguri kwenye siasa. Mwatupeleka wapi? Hivi bado hamjaoana hatari itakayokuwepo watu wanapozoea silaha za kweli na matoi ya Wachina?


Nauliza mnijibu, hivi hamjaona Watanzania sasa hawaogopi tena silaha kwa kiwango tulichokuwa tumezoea?


Enzi zile watu wakiona tu gari la ‘Fanya Fujo Uone' walikuwa wanakimbia na kujificha hadi uvunguni mwa vitanda vyao.


Leo hii tunawoana wanawasogelea kama vile ni sinia la ubwabwa limeletwa wanakaribishwa wabugie. Mkiona hivi mjue tuko kwenye hatari.
Nakumbuka maneno ya Dakta Slaa kwamba walioko madarakani ndio wanaweza kuondoa amani.


Kwenye haya maandamano ya siasa mbona pale ambapo polisi wanakaa kando hatuoni damu ikimwagika?


Si tumeona pale wanapozuia ndipo fujo inapotokea? Nauliza na hao makada wanaoropoka huku na huko hawana mioyo ya nyama? Watu wanalia na kuomboleza lijitu linaibuka na kutoa kauli ya kijinga badala ya kujua thamani ya damu iliyomwagika. Ndiko tumefika enyi watu? Bado mwasema eti sisi ni wadugu? Miye sipo kabisa katika haya yote. Simo kabisa.
Hata busara za wahenga mmeamua kuzifuta kabisa sio? Kwani hamjui bandu na bandu humaliza gogo? Hamjui kwamba kuondoa amani ni rahisi kuliko kuitengeneza?
Nasema tena iwe iwavyo kwani hamjui kwamba mkiendelea na mambo haya kishabiki badala ya kuyafanya kitaalam mnakaribisha machafuko? Nasema kwa matatizo yote haya tuliyonayo bado mwataka kuleta na mengine?


Hebu fanyeni hesabu mniambie tangu miaka miwili iliyopita tumepoteza uhai mara ngapi kwa sababu ya siasa? Mmefika hapo enyi watu?


Lakini, mbona mnaendelea kusema hii ni nchi ya amani na utulivu? Utulivu gani kama wanaotaka kutoa yaliyo moyoni mwao wanakutana na nguvu kubwa namna hii? Hili la sensa mbona halikusemwa kabla? Na hao wavaa magwanda wanajitetea kwamba walikuwa na kibali.


Hivi kwani aliyetoa kibali hakujua sensa ipo au naye alikuwa "maimuna" kwenye hili?
Wacha tu tushangae maana haya ni zaidi ya yale ya Firauni. Mimi sipo huko hata kidogo mtoto wa mama.


Hebu rudini kwenye siasa za kuchuana kwa sera pande zote mbili? Hailipi kuona upande mmoja unatumia nguvu kuzuia fikra mbadala.


Nasikia kuna mahali watu walifikia hatua hata ya kunyimwa chumba kwenye hizo mnazoita ‘guest house'. Huko simo ila sasa tunaanza kuona watu wamechoka hadi fikra sasa yanatokea ya kutokea.


Kwani hamjui ni amri ya maumbile vitu na watu kuzeeka halafu kufa? Mbona hawa jamaa wanaonekana wamezeeka kiasi kwamba lazima kundi lao sasa life kwa uchovu wa umri mkubwa? Naona wanajaribu kutumia chochote wawezacho kujipatia sapoti, lakini siasa ni kuingia kwenye moyo wa mtu sio kwatisha watu eti. Kwani hilo hamlijui?


Hamjajifunza kitu pale yule mbunge alipopanda jukwaani na bunduki yake kiunoni kuomba kura? Msipojifunza kwa yaliyotokea mbele ya macho yenu mtaelewa kwa mafunzo ya mwalimu gani enyi wanadamu? Mie simo huko kote ila roho inaniuma. Simo kabisa!

NA MZEE WA KUJITOA TANZANIA DAIMA
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Tatizomajeshi yetu nayo yamekuwa wadau wa siasa tena wa mlengo wa ufisadi ndio maana yote haya yalitokea na yataendelea kutokea kwa sababu mafisadi na chama chao cha mabwepande wako tayari kumlaza mtu yeyote anaepigania haki mabwepande,
Hao wakimbizi wa ngunguri ni kiji mfano tu cha udhalimu wa hawa POLICCM NA Kutumikishwa kwao.(WANASHINDWA KUJUA HATA WAOWANAPIGANIWA WAPATE MAISHA BORA NA WATOKANE NA KULALA NA WATOTO ZAO KWENYE NYUMBA ZA MABATI/MISONGAMANO)

USHAURI: TUJIFUNZE LAWAMA/KERO IPI TUIWAKILISHE NA KUMLENGA MUHUSIKA,fujo hizi zote zinatokana na Jeshi la polisi kubadilika na kuwa POLICCM.Majeshi yarudi kwenye neutral ground na wa achane na kutumiwa na chama cha mabwepande ''nature ichukue mkondo wake alie zeeka na kupoteza mvuto afe kifo salama'' msi Wasaidie wafe na raia(wapambanaji /wana mageuzi) wasio na hatia
 
Ni wazi polisi hawalindi tena wananchi.

Ni muhimu wananchi kupata ulinzi.

Ningependa thread hii tujadiliane namna ama njia ambazo wananchi wanaweza kujilinda wenyewe.

Ni wazi hatujafikia hatua ya kuomba msaada wa ulinzi toka nje ya nchi,hilo litatokea endapo serikali itakwenda kinyume na mbinu za umma/wananchi kujilinda dhidi ya udhalimu na mauwaji ya chombo cha serikali.

Nakaribisha maoni...
 
Sasa imekuwa too much kwa Jeshi la Polisi kuua wananchi wasio na hatia na kama Jeshi hili Halitashtakiwa litaendeleza mauaji haya!
Alternatively, Polisi wawe targetted wanakoishi mtaani na kutiwa adabu ili nao wajisikie insecure kama wananchi wasio na hatia wanavyojisikia!
 
wanaua wao, wanapeleleza wao,wanaunda tume wao, wajumbe wa tume ni wao, wanajipa ripoti wao, wanaisoma ripoti wao, wananpongeza na wanapandishana vyeo wao.

Drama, comedy, satire, travesty you name it
 
Mimi ninafikiri wamepewa Amri ya kuua si bure! Poor nchi dhaifu yenye watu DHAIFU chini ya uongozi dhaifu ila wenye ubabe!

What can we do zaidi ya kusema, kusema na KUSEMA na JK ambaye tulisema ni DHAIFU analijua hili na anataka kuonesha kwa vitendo nani ni DHAIFU!
 
hawa wamepewa maagizo waue, nawambia mkuu wa mkoa wa arusha bwana magesa wamekosana na mponjoro ocd mpya wa arusha baada ya kukataa kuinyanyasa chadema na amesema kuwa siwezi kuteleleza matakwa ya wanasiasa imekuwa ugomvi mkubwa sana mpaka huyu ocd akaandika barua ya kuacha kazi bwana mwema akaona c vyema huyu bwana kuacha kazi amemuamisha tena kwenda kawe huyu ocd ana msimamo mzuri sana
 
HATA KAMA CHADEMA WAMEKIUKA SHERIA KWA KIWANGO GANI! wangewashitaki, Solution sio kuuwa.
 
Back
Top Bottom