Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

USISAHAU na kuijulisha Dunia jinsi sisi watanzania tulivyo wanafki. Nasubiri majibu ya Dunia baada ya kujua.

Apumzike kwa amani Aquilina, na pole kwa familia yake.
 
Wakuu ni ombi tu hizi picha zinazidisha hasira kwa wale walio namna moja au nyengine athirika na fujo au matukio hayo. Sidhani kama ni busara kuziweka kwani unachochea chuki katika jamii!! Ni mtazamo tu.
Wewe ni m.a.k.u.
 
Wakuu ni ombi tu hizi picha zinazidisha hasira kwa wale walio namna moja au nyengine athirika na fujo au matukio hayo. Sidhani kama ni busara kuziweka kwani unachochea chuki katika jamii!! Ni mtazamo tu.
huwezi kuficha mavi kwa kiganja, harufu itakuumbua tu.
 
utashangaa huyu kijana,polisi anaitwa benjamini kweli hivi wewe kijana tumepaka majivu jumatano unaamka asubuhi unasali unamuomba MUNGU niende salama kazini pepo na mashetani yote yakaondoke kwenye mwili wangu,kwamba nisimkwaze mtu yeyote mimi nikawe mlinzi wa amani kwa watu wote kama ni benki kama ni baharini kama ni stendi halafu mwisho unafyatua risasi kumpiga mtu mwingine JONI POMBE MAGUFULI MWEZI HUU NI MUHIMU KWAKO waambie kila kitu kitapita nawashangaaaaa sana askari WAKRIST tubuni na kuiamini Injili
 
Mimi sasa hivi hata mwanamke nakuuliza kwanza ww ni mrengo gani kabla ya affairs. Kama ni ccm tunaachana hapo hapo maana hawa wanawake ndo wanawapa kura na ndo mengi mashangingi ya CCM. Ukiwa pro ccm automatically unaunga mkono uhalifu wa polisi nchini ambao unapewa nguvu na hawa chichiem.
 
action and reaction are equal and opposite. that said brutality one day will change course. when, it is history that will tell.
 
You


While I completely discourage police brutality, it is unfortunately a worldwide phenomenon. My friend, you are speaking of gathering evidence for the world to see…to see what?...what is not seen!? Police brutality is happening in all countries, I wonder to whom do you want it seen!?…is it USA…or are u not informed of what is happening in America especially if police are dealing with black guys!?. No my friend, you are not going to achieve anything by gathering all the evidences! You would probably instead advocate for national-wide campaign to stand vs police brutality! However, citizens also they are obliged to comply with police legal instructions to avoid unnecessary turmoil!
 
duh
 
Of course sycophants like you will say or do anything to give excuses for this uncouth and evil regime, that what idiots do believing they are somewhat safe, for now. Contrary to what you insinuate about police brutality worldwide ours is state-sponsored police brutality witnessed mostly in similar fascist regimes. In the US any action that results in injury or loss of life investigation is immediately begun and if there is any wrong-doing, action is taken and culprits punished.
 
Na
EDO KUMWEMBE

SIKU Fulani ya maisha yako. Hakutakuwa na wale walinzi kando yako. Hakutakuwa na rafiki zako kando yako. Hakutakuwa na wale washkaji zako wa mtaani kwako. Hakutakuwa na wale wapambe wako kando yako. Hata kama watakuwepo hautawaona.
Pua zako zitakuwa zimewekwa pamba ndani ya jeneza. Foleni ya watu itakuwa ikikuaga. Hautakuwa na fahamu. Ina maana atakayeshika kifua chako hatasikia mapigo yoyote. Hautajua kama anayekuaga ni rafiki yako au adui yako. Mama yako na dada zako kando ya jeneza watakuwa wakilia wakiliwazwa na rafiki zako, ndugu na jamaa zako.
Kaka zako watakuwa bize sana kuhakikisha watu wote walio msibani wanapata mahitaji yao. Mmoja atakuwa anahakikisha kila mtu amekula. Mwingine atakuwa akifarijiwa na rafiki zako wa karibu. Mwingine atakuwa kaburini kuhakikisha kaburi lako limechimbwa vema. Mwingine atakuwa anaongea na sheikh au askofu kuhusu mpangilio mzima wa mazishi.
Kama una cheo kikubwa sana basi wakubwa waliobaki watakuwa wanapiga saluti mbele ya jeneza lako. Hata hivyo haitasaidia sana. Haitakurudishia pumzi. Kama ulikuwa mwanamuziki mahiri sana, bado haitakurudishia pumzi. Alikufa Michael Jackson na bado hajarudishwa.
Kama ulikuwa kiongozi maarufu bado haitasaidia. Alikufa Mwalimu Nyerere na bado hajarudishwa. Alikufa Nelson Mandela, alikufa Martin Luther King, alikufa JF Kennedy. Wote hawa hawajarudi tena. Kila siku tunapita kando ya makaburi yao na kuishia kusema “Walikuwa mashujaa”. Lakini mbona hawanyanyuki chini ya udongo na kusimama?. Kumbe hawakuwahi kuwa wakubwa kuliko wewe.
Kuna mkubwa mmoja tu ambaye hapigiwi saluti lakini anabakia kuwa mkubwa. Anaitwa Mungu. Kwanini uringa sana hapa duniani? Ni swali linaloendelea kushangaza sana. Wakati mwingine maisha yanashangaza sana. Sana. Sana. Kuliko tunavyofikiri.
Wakati tukikaribia kukuaga, mtu ambaye ataendelea kuheshimika kwa muda tu, ndani ya siku hiyo, atakuwa MC wa shughuli hiyo. Hautaweza kumpinga. Yeye ndiye ambaye atatuambia muda gani ‘utabebwa’ kwenda eneo moja kwenda jingine. Yeye ndiye ambaye atatuambia muda wa maziko, muda wa kula, muda wa kwenda makaburini. Yeye ndiye ambaye kwa mbwembwe atatuambia matanga au Arobaini yatakuwa lini.
Leo utakuwa na mbwembwe nyingi katika kundi la mashabiki wa muziki wako wanaokuhusudu. Leo utakuwa na mbwembwe nyingi kwa walinzi wanaokulinda na silaha. Leo utakuwa katika baa Fulani ya sehemu Fulani ukitoa kila amri ambayo wanyonge wanatekeleza bila ya kuguna. Unalipa bili unaondoka. Lakini duniani kuna mkubwa mmoja tu.
Wakati mwingine unajidanganya kuwa unachofanya ni sahihi. Lakini mbona hautaki kusikiliza mawazo tofauti Edo? Ni kwa sababu ya maisha ya kidunia ambayo wakati mwingine huwa tunadhani ni marefu sana. Wakati mwingine huwa tunadhania kwamba tulizaliwa kabla ya Mlima Kilimanjaro.
Kama ungepewa pumzi ya kutafakari wakati tukikupeleka futi sita chini ya ardhi ndipo utakapogundua kuwa kuna vitu vilikuwa vikubwa kuliko wewe. Ndipo utakapogundua kuwa ile bahari ya Indi pale Coco Beach na kwinginepo ilikuwepo kabla ya wewe.
Tenda mema kadri unavyoweza. Hili sio suala la dini wala kabila wala rangi. Kuna sehemu mwanadamu unakosea sana lakini kiburi cha pumzi za muda ndicho ambacho kinatusumbua kwa sasa. Mwisho wa siku pumzi zikiisha tutaondoka makaburini kurudi nyumbani kwako na kuanza kuongelea maisha mengine ya duniani.
Nyakati hizo wengi tutajikumbusha kimoyomoyo kwamba kuna mkubwa mmoja tu ambaye anapaswa kututia hofu na sio wewe ambaye dakika chache zilizopita tulikuwa tumetoka kuweka mikono ya sala kando ya kaburi lako na kurudi nyumbani kwako kuondoa tarubai angali ukiwa haupo.
Hapa namzungumzia kila mtu mwenye madaraka makubwa na madogo, umaarufu, au pesa au hulka ya kujisikia kuliko wengine. Binafsi nilizaliwa nikiwa uchi juu ya kitanda fulani cha hospitali ya Ocean Road kuelekea mwishoni mwa miaka ya 1970. Siku nikipoteza pumzi watakaonizika wanaweza kuamua nizikwe nikiwa uchi. Maringo ya nini?
Ni nyakati tata katika nchi yetu. Katika ngazi ya mtu binafsi au taasisi zetu au serikali Kuu. Kuna sehemu tunakosea sana kwa kujiamini kupita kiasi. Maringo ya mwanadamu yanazidi kupitiliza. Inakera sana. Wengi wanafunga mdomo. Wengi wana hofu. Nilikuwa nawakumbusha tu, kuna mkubwa mmoja tu. MUNGU.
Usijivunie kuwa bosi wa Chadema. Usijivunie kuwa na sauti kubwa kwa Waislamu au Wakristo. Usijivunie kuwa bosi wa CCM. Usijivunie kuwa kiongozi mkubwa. Usijivunie kuwa tajiri wa mtaani kwako. Kuna sehemu moja unakosea sana.
Mwanamuziki Sunday Mjeda ‘Linex’ aliwahi kulalamika katika wimbo wa “Moyo wa Subira’ akitamani kurudisha nyakati nyuma arekebishe ubaya aliowahi kuufanya. Uzuri kwa Mungu, au ubaya kwetu, ni kwamba wakati watu wakitawanyika katika misiba yetu hatutaweza kurudisha nyakati nyuma. Ni nyakati hizo ndipo tutajua kwamba kuna mwanaume mmoja tu. MUNGU.
Walionielewa vizuri nadhani watakuwa wamenielewa vizuri sana, hasa kwa kila kitu kinachoendelea katika nchi yetu kwa sasa. Life goes on. Kuna Mungu mmoja tu. Na kuna mimi mmoja tu. Edo kumwembe. Na kuna wewe mmoja tu, unayesoma Makala hii. TUTAFAKARI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…