hata mimi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 1,356
- 1,442
Limekuwa neno maarufu sana kipindi hiki japo binafsi nilianza kulisikia kwenye clip ya Siro akimchana Mamboleo kuhusu uvaaji wa sare ya polisi (kimakosa) na kuanika watuhumiwa.
Nashukuru kuna mjumbe humu kafafanua kuwa PGO ni Police General Orders. Lakini swali langu ni kutaka kujua zaidi hiyo kitu na upatikanaji wake. Nauliza hivi kwasababu.
Zamani kidogo nikiwa mdogo kitambo hicho nikiwa primary (darasa la 4-5 hivi) nakumbuka Mzee alitoa vitu vingivingi kwenye makabrasha yake akidai ni takataka anataka kuvichoma moto.
Sasa tulikuwa na tabia (na yeye mwenyewe alishatuzoesha) kuwa kila anapokuwaga anafanya safisha safisha kwenye makabrasha yake basi ni lazima avikusanye vile asivyovihitaji na kutuachia sebuleni hapo tuchague tuvipendavyo vyote then vitavyobaki tukavichome moto.
Basi siku hiyo nakumbuka katika nilivyopendezwa navvyo na kuviokoa ilikuwa ni vitabu vidogo vidogo vitatu; viwili vilikuwa ni katiba ya NCCR Mageuzi kwa miaka tofauti tofauti (Kamoja kalikuwa kana cover kama bluu fulani hivi na kengine cover yake ilikuwa ina rangi mbili upande bluu na upande nyeupe.
Maswali yalikuwa hayachezi mbali pia nilimuuliza mara kwa mara sababu ya kuvitupa vitu hivyo kila mara alipokuwa akifanya hivyo. Katika vitabu vile nakumbuka alinijibu tu kuwa havina kazi kwasababu ni vya zamani zaidi (matoleo ya zamani) na pia yeye hajihusishi na siasa tena. Alisema yeye alikuwa ni Mpinzani damu enzi hizo NCCR-Mageuzi ndo iko moto ila mwaka 1995 ndo ilikuwa mwisho wa kujihusisha na siasa na hataki tena kuisikia wala sisi tujihusishe.
Tuache huko maana siyo lengo la uzi twende kwenye kitabu cha tatu sasa. Nakumbuka kitabu kile nilikuwa nakipenda sana na nilikuwa nasoma mara kwa mara. Kiliandikwa mambo mengi sana kuhusu kazi ya polisi na kwakuwa ni zamani sana siwezi kuyakumbuka yote ila kwa ujumla nakumbuka kilielezea namna ya kukamata mtu, kupokea na kuandika maelezo ya mtu, mahabusu, mavazi na vitu vingi vingi tu.
Kitu ambacho sikuweza kujua ni jina la kile kikitabu maana hakikuwa na kava na ukurasa wake wa kwanza uliokwepo ni kuanzia kwenye yaliyomo nakumbuka. Nakumbuka mzee nilimuuliza pia kwamba kwanini ana kitabu kinachoelezea mambo ya polisi (enzi hizo polisi tunawachukulia kama nini sijui) basi mzee alinijibu tu kuwa alikipata alipokuwa mgambo.
Dah najuta kupoteza vile vitabu (mchwa walikula vingine vilichakaa) pia najilaumu kwani kama kale kakitabu ndo PGO huenda saivi ningekuwa zangu napitia pitia PGO mdogo mdogo mwenyewe kila siku[emoji23].