Polisi acheni kutumika kisiasa kuwalinda CCM, Corona ipo Upinzani tu, CCM hakuna?

Polisi acheni kutumika kisiasa kuwalinda CCM, Corona ipo Upinzani tu, CCM hakuna?

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
988
Nina mashaka kabisa kama kweli tuna jeshi la polisi hapa Tanzania kama siyo sehemu ya chama cha mapinduzi. Kwa sasa polisi bila haya wanatumika kisiasa kuilinda na kuitetea CCM huku wakikandamiza vyama viingine vya kisiasa.

Kama CCM wanakagua utekelezaji wa Ilani yao, ni kazi ya upinzani pia kufuatilia na kutoa mawazo mbadala kwenye miradi ile ile, hakuna aliye juu ya sheria katika taifa hili. Huwezi ukawa unatumika kulinda chama kimoja kufanya mikutano ya kisiasa lakini wengine wakikutana hata mikutano ya ndani unawaambia ni mikusanyiko eti kuna Corona, Mikutano ya CCM hakuna Corona? Haya mambo hayakubaliki kamwee!

Iko siku tutasema hapana mtupige na mtufunge wote wapinzani nchi nzima mtumalize. Tutasema sasa inatosha na unyanyasaji bado.
 
Angalieni haya yanayoendelea CCM lakini polisi wetu wapo kimya tu.
 
Aibu tupu jeshi la Polisi kuwa Green Guards

Please Bi Hangaya do Something.
 
Yaani wanasiasa wanakupa sababu ya kuzuia jambo fulani na wewe unaishikilia katika kujenga hoja!!! Utasumbuka sana.
 
Wapinzani wao wanasemaje maana ni kama hawapo
 
Zaburi 37:32 Mtu asiye haki humvizia mwenye haki,
Na kutafuta jinsi ya kumfisha.
 
Mithali 11:6 Haki yao wenye haki itawaokoa;
Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.
 
Kwani wapinzani wenyewe wanasemaje kuhusu corona ipo au haipo?
 
Mavuvuzela wako bize kujibu. Sijui wanatumwa au muwasho.
 
Back
Top Bottom