Polisi afukuzwa kazi kwa kusafirisha dawa za kulevya

Polisi afukuzwa kazi kwa kusafirisha dawa za kulevya

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Jeshi la polisi limemfukuza kazi askari wake mwenye namba E 8905 Koplo, Anthony Francis wa Kituo cha Polisi Kisarawe aliyekamatwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi.

Fracis alikutwa akisafirisha dawa hizo kiasi cha kilogramu 76 katika eneo la Nanenane, Manispaa ya Morogoro .

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema askari huyo alikamatwa akiwa amepakia dawa hizo katika gari yake aina ya Toyota Brevis eneo la nanenane Manispaa ya Morogoro.

Katika tukio jingine, jeshi la polisi linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kusafirisha milipuko yenye sumu katika basi la kampuni ya Feruzi kinyume cha sheria .

Jeshi la polisi mkoani Morogoro linaendelea na misako kwa wasafirishaji wa dawa za kulevya aina ya bangi ambapo watuhumiwa 22 tayari wanashikiliwa kwa kuhusiaka na biashara hiyo haramu.
 
Wacha apambane sasa na maisha ya kitaa. Hakuna namna.
 
Nilitegemea atahukumiwa nyundo za kutosha Kama wahalifu wengine wa bangi.
 
Mungu amtie nguvu katika maisha yake mapya huko uraiani.
Lkn kama mwanadamu anapaswa kujitafakuri na kuanza upya safari ya maisha huku akitubu na kufanya kazi kwa bidii na nidhamu.
 
Huyo ilitakiwa afungwe jela hata miaka 10 aone utamu wa maisha ya jela wanakowabambikizia wengine makosa na huko jela angeliwa kiboga iwe fundisho kwa wanoko wengine.
 
Mungu amtie nguvu katika maisha yake mapya huko uraiani.
Lkn kama mwanadamu anapaswa kujitafakuri na kuanza upya safari ya maisha huku akitubu na kufanya kazi kwa bidii na nidhamu.
Haendi uraiani,anaenda jera
 
Back
Top Bottom