Polisi endesheni magari yenu kwa kufuata Sheria za usalama barabarani, hamko juu ya Sheria

Polisi endesheni magari yenu kwa kufuata Sheria za usalama barabarani, hamko juu ya Sheria

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Polisi wamekuwa wakiendesha magari yao vibaya sana bila kufuata sheria na taratibu za barabarani.

Watu wengi wamegongwa na kufa, na wengine kujeruhika kutokana na uendeshaji wao mbovu.

Pia uendeshaji mbovu huaribu vyombo ambavyo vimenunuliwa kwa Kodi za wananchi.

Na mbaya zaidi magari yao hayana bima, wakikugonga imekula kwako.

1617571466680.png

1617571515962.png
 
Huku chuga kuna Dogo aliwanyoosha,walimfungia barabara kwa kutumia l/Cruiser yao Dogo akawanyooshea akapita nao.
 
Serikali ifikirie namna bora zaidi ya kuwapata polisi wenye uelewa, weledi na waoweza kujisimamia huku ile kauli mbiu ya utii wa sheria bila shuruti wakiishi kwa vitendo
 
Wanajeshi na Police wao wako juu ya sheria za rodi.....wanapita hata upande usio wao
Ni ulimbukeni tu unawasumbua! Askari anaejielewa hawezi kufanya Ujinga huo wa kuendesha gari bila kufuata Sheria! Askari anaejitambua hufuata Sheria ili awe mfano kwa Raia wema!!
 
Ni ulimbukeni tu unawasumbua! Askari anaejielewa hawezi kufanya Ujinga huo wa kuendesha gari bila kufuata Sheria! Askari anaejitambua hufuata Sheria ili awe mfano kwa Raia wema!!
Hata wahalifu..... Tuki mess tuna mapolisi wa kutupigia simu, unaliongeleaje hili?
 
Hata wahalifu..... Tuki mess tuna mapolisi wa kutupigia simu, unaliongeleaje hili?
Hao siyo Mapolice ni wahalifu wenzenu walioko ndani ya Jeshi la Police! Sema huwa hawana muda mrefu sana ndani ya Jeshi,huwa system inawatema mmoja baada ya mwingine!!
 
Back
Top Bottom