Polisi hawapaswi kuuunganisha wahalifu na kabila wala chama chao cha siasa, waache mara moja tabia hii mbaya

Polisi hawapaswi kuuunganisha wahalifu na kabila wala chama chao cha siasa, waache mara moja tabia hii mbaya

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
Kuna mambo mengi polisi wa Tanzania wanatuhumiwa kukosa ujuzi wa kazi zao (professionalism) na hata kuwepo kwa madai kwamba tatizo la polisi wetu ni kwamba wengi wao ni wale ambao hawakuwa na matokeo mazuri shuleni. Labda ni kweli.

Na labda kuwepo kwa uwezekano huu ni pale ambapo wanawatambulisha watuhumiwa wa tukio fulani la uhalifu kwa vyama vyao, kwa mfano CHADEMA - japo ni mara chache sana nimesikia polisi wakitambulisha watuhumiwa wanachama wa wa CCM kwa chama chao.

Polisi wajiziulize, hivi wakimkamata mtuhumiwa Msukuma, au Mchaga, kwa nini hawasemi tumemkata mtuhumiwa Msukuma au Mchaga? Kama wanajua kufanya hivyo sio sahihi, kwa nini wanasema tumekamata watuhumiwa wafuasi wa CHADEMA?

Uhalifu haupaswi kuwa na kabila kama ambavyo haupaswi kuwa na chama. Kukitokea uhalifu au hata mauaji Polisi hawapaswi kuuunganisha wahalifu na kabila wala chama chao cha siasa. Mhalifu ni mhalifu, kwa kuwa anakamatwa mtu sio chama au kabila

Hivi kweli Polisi wetu hawaelewi kutambulisha watuhumiwa kwa chama ni kuchochea chuki na vurugu nchini kati ya vikundi na vikundi?

Mnawalaumu viongozi wa upinzani kuchochea vurugu, huku nyie wenyewe Polisi mnafanya matendo na kutoa kauli ambazo ni mbaya mara mia zaidi ya zile za viongozi wa vyama vya upinzani katika kuchochea vurugu nchini. Fanyeni kazi kwa kutumia akili tafadhali.

Kamanda Sirro, hili nalo linazidi uwezo wa kufikiri? Angalia usije ukaishia Makakama ya Kimataifa!
 
Mchezo wanaofanya Polisi ni mauti ya Watanzania. Wajiulize ilikuwaje Kenya wakaishia kuuana baada ya uchaguzi.

HUwezi kuwa poyoyo wa kufikia hatua yakusema wanachama wa chama fulani wamekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya mwanachama wa chama fulani.

Umepeleka wapi akili zako wewe, umeazimisha?
 
Wakitangazwa wa CCM ni sawailw wakitangazwa wa kwenu inakuwa nongwa au siyo vumilieni tu.
Nipe mfano mmoja tu wa tukio la uhalifu ambapo Polisi walifanya hivyo nitakupa mifano mengine 10 ya polisi kufanya hivi dhidi ya upinzani
 
Muhalifu hana chama, kama ni CCM, ACT CUF, CHADEMA taja tu tukomeshe uhalifu! Tatizo chandimu siku hizi mmekuwa watetezi wa wahalifu na wazembe, kura yangu hampati ng'oo!
 
Kwa sifa za kuwa Polisi Tanzania unafaa sana!
 
Hii wala sio bahati mbaya, jamaa wanafanya hivyo kwa makusudi kabisa ili kutisha wapiga kura!
Na, ajabu, kesi zimeahirishwa mpaka baada ya uchaguzi ili ukweli usijulikane mpaka watakapotuuzia mbuzi ndani ya gunia!
 
Waendelee kuwataja tu,tuwajue wafuasi wa vyama gani wanaotuvunjia amani ya nchi yetu
 
Ni vigumu kubadilika kwani wanaitumia kikampeni zaidi ili wananchi wawaone CHADEMA ni wakorofi, ni mkakati maalum.
 
Ni vigumu kubadilika kwani wanaitumia kikampeni zaidi ili wananchi wawaone Chadema ni wakorofi, ni mkakati maalum.
ndio maana wanaitwa vilaza wa sekondari. Walikuwa wanapigania uji na ukoko wa ugali na wali badala ya kupiga shule
 
Kuna mambo mengi polisi wa Tanzania wanatuhumiwa kukosa ujuzi wa kazi zao (professionalism) na hata kuwepo kwa madai kwamba tatizo la polisi wetu ni kwamba wengi wao ni wale ambao hawakuwa na matokeo mazuri shuleni. Labda ni kweli.

Na labda kuwepo kwa uwezekano huu ni pale ambapo wanawatambulisha watuhumiwa wa tukio fulani la uhalifu kwa vyama vyao, kwa mfano Chadema - japo ni mara chache sana nimesikia polisi wakitambulisha watuhumiwa wanachama wa wa CCM kwa chama chao.

Polisi wajiziulize, hivi wakimkamata mtuhumiwa Msukuma, au Mchaga, kwa nini hawasemi tumemkata mtuhumiwa Msukuma au Mchaga? Kama wanajua kufanya hivyo sio sahihi, kwa nini wanasema tumekamata watuhumiwa wafuasi wa Chadema?

Uhalifu haupaswi kuwa na kabila kama ambavyo haupaswi kuwa na chama. Kukitokea uhalifu au hata mauaji Polisi hawapaswi kuuunganisha wahalifu na kabila wala chama chao cha siasa. Mhalifu ni mhalifu, kwa kuwa anakamatwa mtu sio chama au kabila

Hivi kweli Polisi wetu hawaelewi kutambulisha watuhumiwa kwa chama ni kuchochea chuki na vurugu nchini kati ya vikundi na vikundi?

Mnawalaumu viongozi wa upinzani kuchochea vurugu, huku nyie wenyewe Polisi mnafanya matendo na kutoa kauli ambazo ni mbaya mara mia zaidi ya zile za viongozi wa vyama vya upinzani katika kuchochea vurugu nchini. Fanyeni kazi kwa kutumia akili tafadhali.

Kamanda Sirro, hili nalo linazidi uwezo wa kufikiri? Angalia usije ukaishia Makakama ya Kimataifa!
Baada ya CCM kubanwa na jumuiya ya kimataifa huu ndo mpango wao sasa. Matukio yote maovu watapewa Chadema ili watengeneze balance ya kujitetea huko mbeleni. Uzuri jumuiya ya kimataifa wameshaushtukia huu mchezo
 
Miaka ya nyumba Police walikuwa wakikamata Majambazi wanasema walikuta na kofia na Tshirts za chama cha Upinzani na wanavionyesha kwenye Luninga... kwa kweli jeshi letu la Police mjirekebishe.

Hii point ya mtoa hoja ina mantiki sana.
 
Baada ya CCM kubanwa na jumuiya ya kimataifa huu ndo mpango wao sasa. Matukio yote maovu watapewa Chadema ili watengeneze balance ya kujitetea huko mbeleni. Uzuri jumuiya ya kimataifa wameshaushtukia huu mchezo
MKuu kama huu ndio mpango wao basi hawana akili timamu - athari za kuwaambia watu wa CCM wanachadema wamemuua mgombea wenu wa CCM zinaweza kuwa mbaya sana!
 
Back
Top Bottom