Polisi hawapaswi kuuunganisha wahalifu na kabila wala chama chao cha siasa, waache mara moja tabia hii mbaya

Polisi hawapaswi kuuunganisha wahalifu na kabila wala chama chao cha siasa, waache mara moja tabia hii mbaya

Watuhumiwa kama hawa unategemea polisi wawaite vipi?
IMG-20150426-WA0004.jpg
 
Ndugu yangu CHADEMA isikimbie kivuli chake. Wafuasi wake wanafanya mauaji na utekaji ni lazima watajwe. Watanzania sasa wamewafahamu kuwa ni chama cha kuteka, kuuwa na kuchoma moto majengo yake yenyewe. POOR CHADEMA
 
Mharifu ni mharifu tu.
 

Attachments

  • 707fe124a1f10f2be88b7154b5944547.jpg
    707fe124a1f10f2be88b7154b5944547.jpg
    33.9 KB · Views: 8
Race, kabila, vyama vya siasa. Huwa vinasaidia kwenye Criminal Investigation Ila sio kwenye Conclusions. Inategemea na mazingira ya tukio lenyewe.
 
Kwa hiyo hii bunduki ni ya wafuasi wa Cuf?View attachment 1591126
Kampeni za kizamani mno hizi ziliwahi kutumika enzi za ujima wa ngunguri!!

Mtuhumiwa kama ni mfuasi au mwanachama wa CHADEMA lazima iwekwe wazi.
Ikiwa hivyo ndivyo walaaniwe maccm wote na mashabiki wao waliofilisi nchi hii kwa kuiingiza mikataba mibovu, kuua viwanda, vyama vya ushirika na kutia wananchi umaskini wa makusudi hususan wakulima.
Je tunasibishe ccm na umaskini uliotopea Kongwa, Lindi, Nkasi, Liwale nk? Je yale majizi yaliyochoma benki kuu? Je yale yaliyo...?
 
Nipe mfano mmoja tu wa tukio la uhalifu ambapo Polisi walifanya hivyo nitakupa mifano mengine 10 ya polisi kufanya hivi dhidi ya upinzani
Wanajisahaulisha walivyomuua Mawazo kule Geita... na maandiko yao humu yanaakisi matendo yao.
 
Kuna mambo mengi polisi wa Tanzania wanatuhumiwa kukosa ujuzi wa kazi zao (professionalism) na hata kuwepo kwa madai kwamba tatizo la polisi wetu ni kwamba wengi wao ni wale ambao hawakuwa na matokeo mazuri shuleni. Labda ni kweli.

Na labda kuwepo kwa uwezekano huu ni pale ambapo wanawatambulisha watuhumiwa wa tukio fulani la uhalifu kwa vyama vyao, kwa mfano CHADEMA - japo ni mara chache sana nimesikia polisi wakitambulisha watuhumiwa wanachama wa wa CCM kwa chama chao.

Polisi wajiziulize, hivi wakimkamata mtuhumiwa Msukuma, au Mchaga, kwa nini hawasemi tumemkata mtuhumiwa Msukuma au Mchaga? Kama wanajua kufanya hivyo sio sahihi, kwa nini wanasema tumekamata watuhumiwa wafuasi wa CHADEMA?

Uhalifu haupaswi kuwa na kabila kama ambavyo haupaswi kuwa na chama. Kukitokea uhalifu au hata mauaji Polisi hawapaswi kuuunganisha wahalifu na kabila wala chama chao cha siasa. Mhalifu ni mhalifu, kwa kuwa anakamatwa mtu sio chama au kabila

Hivi kweli Polisi wetu hawaelewi kutambulisha watuhumiwa kwa chama ni kuchochea chuki na vurugu nchini kati ya vikundi na vikundi?

Mnawalaumu viongozi wa upinzani kuchochea vurugu, huku nyie wenyewe Polisi mnafanya matendo na kutoa kauli ambazo ni mbaya mara mia zaidi ya zile za viongozi wa vyama vya upinzani katika kuchochea vurugu nchini. Fanyeni kazi kwa kutumia akili tafadhali.

Kamanda Sirro, hili nalo linazidi uwezo wa kufikiri? Angalia usije ukaishia Makakama ya Kimataifa!
Ushauri wako ni mzuri mno unapaswa kufuatwa lkn hauzuii Polisi Nao ikiwabidi kutoa taarifa kwa mtindo huu.

Kwann, kuepuka malalamiko toka chama ambacho wanachama wake wamekamatwa taarifa inatoka kwa uwazi hawa ni wahalifu wamekamatwa kwa makosa yasiyohusiana na siasa.( Kifupi chake " hawa wahalifu ni wanachama wa ,,,,,"

Katika marekebisho hayo unayoyapigania jiulize unadhani ni sahihi kuwatolea mifano Askari Polisi walio katika vazi rasmi la kazi huku wakiwa wanalinda usalama wa eneo la mkutano?

Kwa asili jamii inawachukia Polisi, iwe Ulaya, Afrika au Amerika Polisi majukumu yake yanapelekea jamii yoyote kutowapenda nyakati kwa nyakati.

Jamii iliyona shida itampenda Polisi ambaye atashughulika na jamii halifu huku hali ikiwa verseversa.

Polisi ni kila kitu kila mahali hivyo kupendwa kwake ni wakati wote na kuchukiwa ni wakati wote.

Sasa wanasiasa wanapenda kushangiliwa kwenye mikutano yao, hivyo njia rahisi kwao ni kuwasema vibaya Polisi ili wapate vifijo lkn hali hii inaharibu nguvu za kiutendaji za asili za Askari mwishowe kuzidisha uhalifu.
 
Kuna mambo mengi polisi wa Tanzania wanatuhumiwa kukosa ujuzi wa kazi zao (professionalism) na hata kuwepo kwa madai kwamba tatizo la polisi wetu ni kwamba wengi wao ni wale ambao hawakuwa na matokeo mazuri shuleni. Labda ni kweli.

Na labda kuwepo kwa uwezekano huu ni pale ambapo wanawatambulisha watuhumiwa wa tukio fulani la uhalifu kwa vyama vyao, kwa mfano CHADEMA - japo ni mara chache sana nimesikia polisi wakitambulisha watuhumiwa wanachama wa wa CCM kwa chama chao.

Polisi wajiziulize, hivi wakimkamata mtuhumiwa Msukuma, au Mchaga, kwa nini hawasemi tumemkata mtuhumiwa Msukuma au Mchaga? Kama wanajua kufanya hivyo sio sahihi, kwa nini wanasema tumekamata watuhumiwa wafuasi wa CHADEMA?

Uhalifu haupaswi kuwa na kabila kama ambavyo haupaswi kuwa na chama. Kukitokea uhalifu au hata mauaji Polisi hawapaswi kuuunganisha wahalifu na kabila wala chama chao cha siasa. Mhalifu ni mhalifu, kwa kuwa anakamatwa mtu sio chama au kabila

Hivi kweli Polisi wetu hawaelewi kutambulisha watuhumiwa kwa chama ni kuchochea chuki na vurugu nchini kati ya vikundi na vikundi?

Mnawalaumu viongozi wa upinzani kuchochea vurugu, huku nyie wenyewe Polisi mnafanya matendo na kutoa kauli ambazo ni mbaya mara mia zaidi ya zile za viongozi wa vyama vya upinzani katika kuchochea vurugu nchini. Fanyeni kazi kwa kutumia akili tafadhali.

Kamanda Sirro, hili nalo linazidi uwezo wa kufikiri? Angalia usije ukaishia Makakama ya Kimataifa!
Mkuu,si tu kuwa na matokeo mazuri,bali hata kichwani hamna kitu.
Nimeishi nao pale Uzunguni - Dom,RPC watano,nawajua ndani nnje - empty kabisa.
 
Back
Top Bottom