JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Licha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa tangazo linaloeleza kuwa haihusiki na jambo lolote linalohusu Kampuni inayoitwa Leo Beneath London (LBL) ambayo inavyoonekana kilio chetu ni cha Watu wengi, lakini nimeamua kuandika hapa kwa kuwa najua kuna wenzetu ambao wana msongo wa mawazo wanaendelea kama mimi wanaendelea kupigwa.
Ipo hivi wale ambao tulikuwa Wanachama, kila tukiingia kwenye mfumo huo kwa nia ya kuangalia nini kinaendelea, tunakutana na jumbe mbalimbali, mojawapo ni kuwa inatutaka kulipia hadi Tsh. 270,000 ili kuweza kuingia katika Akaunti husika na kufanya mchakato wa kunasua fedha zetu zilizokwama ndani.
Nafikisha ujumbe huu kupitia JamiiForums naamini ujumbe huu utafika sehemu nyingi kwa kuwa mimi siwezi kuwafikia BoT.
Ukifungua kwenye akaunti yako ya LBL kuna ujumbe ambao unakuja ukikuelekeza kulipa kulingana na kiwango cha fedha ambacho ulilipia wakati unajiunga.
Mfano levo ya P3 kiwango cha kujiunga ni Tsh. 540,000 hivyo unatakiwa kulipia nusu ya kiasi hicho ambacho ni 270,000 ili wakuwezeshe kufungua akaunti yako na uweze kutoa fedha zako zote zilizosalia kwenye Wallet uhamishe katika mitandao ya simu.
Kinachofanyika ni kuwa hasara inaongezeka kwa Watu kuendelea kuliwa zaidi licha ya juhudi nzuri za Serikali na Jeshi la Polisi linawakamata Watu.
Pia soma:
~ Jeshi la Polisi Morogoro lawakamata maofisa saba wa LBL kwa tuhuma za biashara haramu ya fedha
~ Benki Kuu (BoT): Hatujatoa leseni wala kuruhusu shughuli za LBL