Polisi Kanda ya Ziwa tuondoleeni hatari hii barabarani madereva nyakati za usiku

Polisi Kanda ya Ziwa tuondoleeni hatari hii barabarani madereva nyakati za usiku

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Habari wadau
Maeneo ya Igunga, nzega, tabora, tinde, shinyanga, mizungwi, geita, chato, masumbwe, Isaka,kahama, ushirombo n.k

Ikiwa hujawahi tembea maeneo hayo usiku ni vigumu sana kuelewa hatari ya trekta mbovu, tela za punda na ng'ombe zinazotumika usiku kucha!

Maeneo hayo kuna treka za mkono maarufu power tila! Wanaziundia tella kubwa la kuvuta! Hivyo ziwapo barabarani huwa hazina taa wala reflector za tahadhali!

Mara nyingi wanazitumia usiku kucha kubeba mazao!

Nashauri polisi ifanye operesheni ya kuwabaini, kuwakamata na kuwapa mafunzo kwa lazima waendesha matela ya ng'ombe na power tilla ili kuepusha ajali!

Pia wahakikishe wanafunga taa mbili za ishara, alama za tahadhali mbele na nyuma ya vyombo vyao!

Ajali nyingi zinazochangiwa na hayo ma power tilla hufananishwa sana na bodaboda au baisikeli, kitu ambacho humshitua dereva wa gari pale ghafla anapoona tella kubwa linalovutwa kwa nyuma na power tilla barabarani.

Polisi Kanda ya Ziwa fanyeni opereshini hii maalum kuondoa tatizo hili ni hatari kwa wote!
 
Trafiki hawawezi kufanya kila kitu,huko kuna Wenyeviti wa Vijiji na mitaa hiyo ni sehemu ya Kazi Yao
 
Umewasahau na wabeba Mkaa kwenye Beiskeli halafu huwa wanatembea msululu waambiwe tu ikifika usiku wawe wanavaa viz vest kwa usalama wao.

Maana wakivaa mchana inakuwa ni rahisi kwa maliasili kuwaona.
 
Umewasahau na wabeba Mkaa kwenye Beiskeli halafu huwa wanatembea msululu waambiwe tu ikifika usiku wawe wanavaa viz vest kwa usalama wao.

Maana wakivaa mchana inakuwa ni rahisi kwa maliasili kuwaona.
Wanapenda giza
 
Back
Top Bottom