Polisi: Kigwangalla hajampiga risasi mlinzi Jumanne

Polisi: Kigwangalla hajampiga risasi mlinzi Jumanne

Kwanini serikali hii inatumia nguvu kubwa kuficha ujinga?

Waziri ameua mchepuko kwenye ajali ikafichwafichwa, Kigwangala ametandika mtu nayo inafichwafichwa!!

Arusha kuna ufisadi wa mabilioni ya pesa lakini mkuu wa mkoa analindwa na serikali!
Hivi si walipata ajari mmoja kapona mmoja kafariki. Kupata ajari kuna kuua tena?
 
Kufuatia taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimhusisha mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini na mmiliki wa kiwanda cha kuchakata pamba kiitwacho Mwalujo Ginery, Hamisi Kigwangalla kudaiwa kumpiga risasi mlinzi wake, Jumanne Misango (66), Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limesema uchunguzi umebaini hakuna jeraha wala mvunjiko wowote wa mifupa katika mwili wa mlinzi huyo.

Jeshi la Polisi limesema taarifa za awali zinaonesha kuwa kulitokea wizi wa mali mbalimbali zenye thamani ya TZS milioni 28.5 kiwandani hapo kilichopo Kijiji cha Mwalujo, Wilaya ya Kwimba mkoani humo ambapo Kigwangalla alifika kiwandani na kutokea majibizano kati yake na mlinzi wake, ndipo mlinzi huyo alitoa taarifa polisi kuwa ameshambuliwa na kupigwa risasi katika mguu wake wa kulia.

“Baada ya taarifa hiyo kupokelewa, askari walifika eneo la tukio na kufanya ukaguzi ambapo hakukuonekana viashiria vyovyote vya matumizi ya silaha ya moto. Hata hivyo Jumanne alipewa PF3 na kwenda hospitali ya Wilaya ya Kwimba kwa uchunguzi wa kitabibu, Kigwangalla alihojiwa na kufunguliwa kesi ya shambulio, na yuko nje kwa dhamana,” imeeleza taarifa ya polisi.”

Aidha, Jeshi la Polisi limesema Misango amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Afisa wa Polisi na kuzua taharuki kwa jamii kuwa amepigwa risasi.

“Upelelezi wa kesi hizo mbili unaendelea na utakapokamilika watuhumiwa wote wawili watafikishwa mahakamani,” imeeleza.

Chanzo: Swahili Times
 
Kwanini serikali hii inatumia nguvu kubwa kuficha ujinga?

Waziri ameua mchepuko kwenye ajali ikafichwafichwa, Kigwangala ametandika mtu nayo inafichwafichwa!!

Arusha kuna ufisadi wa mabilioni ya pesa lakini mkuu wa mkoa analindwa na serikali!
Hii ya Arusha siijui kaka tupe update
 
Yaani mtuhumiwa wa wizi anakwenda kumshitaki victim halafu anasahaulika kidogo katika upelelezi kama suspect number 1.

Nimeupenda ubinifu alio tumia mlinzi ku distrupt attention kuwa kwake, vinginevyo sasa hivi angekuwa anakabiliana na sokomoko la kutoa maelezo ilikuwaje hadi vifaa vikapotea.
 
Hao waliuawa na Mbowe ili wasigombee uenyekiti wa Chama
Punguani wewe kwa hiyo na huyo kigwangwala kampiga huyo msukuma risasi ili asigombee?
Unajitia kutetea haki za watu wakati moyo wako umevia roho ya chuki kwa usiwapenda? Unatambua uwepo wa sheria leo? Unatambua uwepo wa wanaharakati za binadamu leo? Ulivyokuwa unawachafua kina Maria?
Unatambua haki za binadamu leo kwasababu kapigwa chuma msukuma?
Ulisema mara ngapi hapa wanaharakati wanapewa pesa na mabeberu na mashoga? So leo hizo wanazotumia kumtetea huyo msukuma hazitoki kwa mashoga?
Wakina kabendera walibambikiziwa case hapa mkawa mnashangilia!
 
RPC Mtafungwa wa Mwanza amesema kijana Omary aliyedai alipigwa risasi mguuni na Dr Kigwangalla alipewa PF 3 na baada ya kufika hospital Uchunguzi wa kitabibu imeonesha hana jereha lolote na mfupa haujavunjika

Hivyo Omary anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani

Aidha Uchunguzi wa Kesi zote mbili bado unaendelea na Dr Kigwangalla yuko nje kwa dhamana, amesema Kamanda Mutafungwa

Source: Ayo tv
Huko Mwanza Vijana Wana umri wa miaka 66?
 

Polisi Mkoani Mwanza wametoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa mitandaoni kumhusu Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini na Mmiliki wa Kiwanda cha kuchakata Pamba kitwacho Mwalujo Ginery kilichopo Kijiji cha Mwalujo, Wilaya ya Kwimba, Hamisi Kingwangala kudaiwa kumpiga risasi Mlinzi wake Jumanne Omary Misango (66) katika mguu wa kulia, ambapo imebainika Jumanne hakupigwa risasi bali haliwaongopea Polisi.

RPC wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amesema taarifa za awali zinaonesha kulitokea wizi wa mali kiwandani ikiwemo Gear Motor HP Radio made 02, Electrical Motor 05 na nyaya za umeme @ Armored Cable Mita 25 vyote vikiwa na thamani ya Tsh 28,525,000.

“Mei 22, 2023 saa 11:00 jioni Kigwangala alifika kiwandani kwake na kukatokea majibizano kati yake na Mlinzi wake, Mlinzi huyo alitoa taarifa Polisi kuwa alishambuliwa na kupigwa risasi mguu wa kulia, Askari walifika eneo la tukio na kufanya ukaguzi ambapo hakukuonekena viashiria vyovyote vya matumizi ya silaha ya moto”

“Hata hivyo Jumanne alipewa PF3 na kwenda Hospitali ya Wilaya ya kwimba kwa uchunguzi wa kitabibu, Hamisi Kigwangala alihojiwa na kufunguliwa kesi ya shambulio na yupo nje kwa dhamana”

“Uchunguzi umebaini kuwa hakuna jeraha wala mvunjiko wowote wa mfupa katika mwili wa Jumanne na hivyo amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Afisa wa Polisi na kuzua taharuki kwa Jamii kuwa amepigwa risasi, upelelezi wa kesi hizo mbili unaendelea na utakapo kamilika Watuhumiwa wote wawili watafikishwa Mahakamani, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi”

Credit: MillardAyo
Hii taarifa mbona imejichanganya sana?
Sasa hapo nani amejichukulia sheria mkononi wakati mmeshasema hakuna aliyefanywa chochote?
 
Back
Top Bottom