Omary - Msamalia
JF-Expert Member
- Jan 19, 2020
- 2,079
- 4,521
Kuna mtu aliua mfanyakazi wake na mwili akatupa ila yuko nje sembuse Kigwangalla hata hajaua 😛 😛 😛
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi si walipata ajari mmoja kapona mmoja kafariki. Kupata ajari kuna kuua tena?Kwanini serikali hii inatumia nguvu kubwa kuficha ujinga?
Waziri ameua mchepuko kwenye ajali ikafichwafichwa, Kigwangala ametandika mtu nayo inafichwafichwa!!
Arusha kuna ufisadi wa mabilioni ya pesa lakini mkuu wa mkoa analindwa na serikali!
Hii imekaaje?Orodha ya majina ya vijana wote waliochaguliwa kwenda JKT na kambi zao
Hii ya Arusha siijui kaka tupe updateKwanini serikali hii inatumia nguvu kubwa kuficha ujinga?
Waziri ameua mchepuko kwenye ajali ikafichwafichwa, Kigwangala ametandika mtu nayo inafichwafichwa!!
Arusha kuna ufisadi wa mabilioni ya pesa lakini mkuu wa mkoa analindwa na serikali!
Punguani wewe kwa hiyo na huyo kigwangwala kampiga huyo msukuma risasi ili asigombee?Hao waliuawa na Mbowe ili wasigombee uenyekiti wa Chama
Maajabu hayataisha jamhuri hii ya Wahuni.Sasa kama huyo Kigwangala hajamdhuru mlinzi wake, kwanini na yeye anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika?
Wame flip kesi, Kimgwangala anaemda mahalamani kama mtoa mashataka kwa tuhuma za kuchafuliwa jina kwa madai ya uongoSasa kama huyo Kigwangala hajamdhuru mlinzi wake, kwanini na yeye anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika?
Huko Mwanza Vijana Wana umri wa miaka 66?RPC Mtafungwa wa Mwanza amesema kijana Omary aliyedai alipigwa risasi mguuni na Dr Kigwangalla alipewa PF 3 na baada ya kufika hospital Uchunguzi wa kitabibu imeonesha hana jereha lolote na mfupa haujavunjika
Hivyo Omary anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani
Aidha Uchunguzi wa Kesi zote mbili bado unaendelea na Dr Kigwangalla yuko nje kwa dhamana, amesema Kamanda Mutafungwa
Source: Ayo tv
Hii taarifa mbona imejichanganya sana?
Polisi Mkoani Mwanza wametoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa mitandaoni kumhusu Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini na Mmiliki wa Kiwanda cha kuchakata Pamba kitwacho Mwalujo Ginery kilichopo Kijiji cha Mwalujo, Wilaya ya Kwimba, Hamisi Kingwangala kudaiwa kumpiga risasi Mlinzi wake Jumanne Omary Misango (66) katika mguu wa kulia, ambapo imebainika Jumanne hakupigwa risasi bali haliwaongopea Polisi.
RPC wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amesema taarifa za awali zinaonesha kulitokea wizi wa mali kiwandani ikiwemo Gear Motor HP Radio made 02, Electrical Motor 05 na nyaya za umeme @ Armored Cable Mita 25 vyote vikiwa na thamani ya Tsh 28,525,000.
“Mei 22, 2023 saa 11:00 jioni Kigwangala alifika kiwandani kwake na kukatokea majibizano kati yake na Mlinzi wake, Mlinzi huyo alitoa taarifa Polisi kuwa alishambuliwa na kupigwa risasi mguu wa kulia, Askari walifika eneo la tukio na kufanya ukaguzi ambapo hakukuonekena viashiria vyovyote vya matumizi ya silaha ya moto”
“Hata hivyo Jumanne alipewa PF3 na kwenda Hospitali ya Wilaya ya kwimba kwa uchunguzi wa kitabibu, Hamisi Kigwangala alihojiwa na kufunguliwa kesi ya shambulio na yupo nje kwa dhamana”
“Uchunguzi umebaini kuwa hakuna jeraha wala mvunjiko wowote wa mfupa katika mwili wa Jumanne na hivyo amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Afisa wa Polisi na kuzua taharuki kwa Jamii kuwa amepigwa risasi, upelelezi wa kesi hizo mbili unaendelea na utakapo kamilika Watuhumiwa wote wawili watafikishwa Mahakamani, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi”
Credit: MillardAyo