Polisi kufunguka leo kuhusu kilichomkuta Dk Ulimboka

Polisi kufunguka leo kuhusu kilichomkuta Dk Ulimboka

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Posts
10,965
Reaction score
5,339
POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, leo watazungumzia hatua ilizofikia katika uchunguzi wa tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Steven Ulimboka.

Pamoja na suala la Dk Ulimboka, imesema pia itazungumzia mambo kadhaa yanayohusu usalama wa nchi.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliliambia gazeti hili kuwa atazungumzia suala la Dk Ulimboka ili kuweka wazi kwa umma kuhusu tukio hilo lililokuwa gumzo katika siku za hivi karibuni.

Kamanda Kova alitoa kauli hiyo alipotakiwa na gazeti hili kueleza endapo Dk Ulimboka ni mmoja wa mashahidi katika kesi iliyokwishafunguliwa kuhusu tukio la kutekwa kwake.

"Tutazungumza na wananchi na wanahabari kwa ujumla kuhusu mambo mengine yanayohusu usalama wa nchi pamoja na hatua tulizofikia katika uchunguzi wa kitendo cha kutekwa na kupigwa kwa Dk Ulimboka," alisema Kova.
Hata hivyo, Kova hakutaka kuzungumzia suala la mtu anayedaiwa kujitokeza na kukiri kuwa ndiye mtekaji wa Dk Ulimboka na yale yaliyoandikwa katika gazeti la Mwanahalisi akidai kuwa mambo hayo yapo mahakamani.

"Sisi tutaweka wazi wajibu tulioufanya na hatua tulizofikia kuhusu kutekwa kwake, mambo mengine ni ya kimahakama, hatuwezi kuyaingilia," alisema Kova.

Kova aliwataka Watanzania kuliamini Jeshi la Polisi na kusisitiza kuwa linafanya kazi yake kwa uadilifu na litahakikisha kuwa ukweli kuhusu tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi, unafahamika.

Kutekwa kwa
Dk Ulimboka

Dk Ulimboka ambaye anatajwa kuwa kinara wa mgomo wa madaktari, alitekwa usiku wa Julai 26 mwaka huu na kujeruhiwa vibaya, kisha kutelekezwa katika Msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kutokana na tukio hilo, daktari huyo wa magonjwa ya binadamu alitibiwa kwa muda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na baadaye kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

Tangu arejee nchini, Dk Ulimboka amekuwa kimya na mara kadhaa akigoma kuzungumzia yaliyomtokea akisisitiza kuwa muda wa kufanya hivyo haujafika.

Lakini wakati daktari huyo akigoma kueleza kilichomsibu, wanaharakati wa masuala ya binadamu wameshatoa tamko kuituhumu Serikali kwamba inahusika, na hivyo kuitaka ilifungulie gazeti la Mwanahalisi walilodai kuwa lilifungwa kutokana na kuandika ukweli kuhusu tukio hilo. .
 
Hawana jipya hao zaidi kuendeleza sinema yao ambayo hakuna anayetaka kuiangalia...Watanzania tumeshaistukia.
 
Ni lini tutafika kukaacha kuhadaa wananchi, kama mimi ni mwanahabari nisingeeda hata kusikiliza hiyo taarifa. Kova anataka tuamini kuwa yale ambayo alieleza awali yalikuwa ya uwongo? Polisi wanataka kuaminiwa kwa lipi? kama wao wenyewe wameshindwa kujiamini na kutumikia haki na ukweli, je wananchi ndiyo watawaamini. Wajiaminishe kwanza ndipo na sisi wananchi tutawaaamini. Vinginevyo kuendelea kutuaadaa na kutupotezea muda.

Haiwezekani watu wanamteka mtu kweupe halafu polisi wanashindwa kubainisha ukweli, je matukio ambayo yanatokea kimya kimya kwenye jamii wataweza kuyafuatilia? Jerry Muro na wenzake walipokamtwa zililetwa picha za cctv na Kova huyo huyo akajivunia kuwa siku hizi jeshi lina vifaa vya kisasa je vifaa hivyo vilikuwa na kwa Jerry Muro tu?

Siamini kabisa kama Jeshi na Polisi na Usalama kwa ujumla wake walenshindwa kubaini ukweli wa suala Ulimboka. Polisi wakumbuke kuwa kuendelea kuficha ukweli au kuzembea katika kutafuta ukweli kutaendelea kuligharimu Jeshi la Polisi na kuendelea kuwapa nafasi watenda maovu kuendelea kufanya hivyo. Kama polisi wameshindwa kujenga imani kwa wananchi kwa nini sisi wananchi tusiamini kuwa usalama/polisi wana mkono wao kutekwa kwa Bw. Ulimboka? Kova atowe ukweli wa masuala ya msingi ili wananchi walipe Jeshi la Polisi imani wanayoitaka. Vinginevyo sioni kama ni rahisi kwa mwananchi wa kawaida kama mimi kuliamini jeshi ambalo limeshindwa kujiaminisha.
 
Eti jeshi la polisi linafanya kazi kwa uadilifu,kauli nyingine utadhani si watanzania hao.Hawa kina Kova wanaishi kwenye dunia yao wenyewe no wonder wako out of touch!eti uadilifu!
 
walishamalizana na Ulimboka sasa wanakuja kutoa porojo ambazo wanajua kwa vyotevyote vile Ulimboka hatapinga, wait and see!!

Maisha matamu, kweli ulimboka kanyamaza! haya mambo yanahitaji ushujaa of the highest degree. I can imagine the courage Mwakyembe has! I admire him, not ULIMBOKA. Anyway, "OBULOLA TIBUGALUKILWA"! Wahaya wanasema (uhai hauji mara mbili)
 
Ok sawa je Ulimboka anaasubiri nini kusema kilichomkuta??au anasubiri Kova atoe yakwake akagandamizie?Nakosa imani na Ulimboka!
 
Tusimkosoe kabla ya kumsikiliza. Naomba tuvute subira kidogo .
 
Nimechanganyikiwa kidogo kuhusu hili swaga zima la utekwaji wa Dr. Ulimboka. Kumbe kilichokuwa Mahakamani na hakihitaji kuzungumzwa nje ya Mahakama ni swala la yule Mkenya feki tu. Bilashaka kama Dr.Ulimboka angeomba kuzungumza na press wangemkataza kwa kisingizio cha kuwa swala lipo Mahakamani, ila wao ruksa katika kutulazimisha tuamini wanachotaka kukitengeneza.
 
Nina uhakika kauli atakayoitoa inaweza sababishia members ban humu.Nina uhakika itakuwa na maudhi ya ajabu.
 
Hili swala si lipo mahakamani? Au mahakama imetoa ruhusa kwa kova kuliongelea?
 
Kuna namna watu wanaliana timing,ngoja tusubiri.Ukweli haufichiki.
 
That is very kind of you dear Kova. Yaani siku zote hamjaongelea progress hadi Ulimboka arudi asije akapitwa na sinema yake mwenyewe!
Duh, mko juu!
 
Jamani hivi watanzania ni wasahaulifu au???? SI tuliambiwa hata lizungumzia tena SUALA hili KWA kuwa like mahakamani? Au ile kesi ya mkenya imeisha???? Tujuzeni
 
Ok sawa je Ulimboka anaasubiri nini kusema kilichomkuta??au anasubiri Kova atoe yakwake akagandamizie?Nakosa imani na Ulimboka!

Mnataka Ulimboka aseme nini kingine!?? amewataja watu,MwanaHalisi limewaandika kinagaubaga mmefanyia nini hizo taarifa!?
 
Back
Top Bottom