Polisi kuhusu taarifa za watu kutekwa: Ni kujiteka, wivu wa mapenzi na kugombea mali

Polisi kuhusu taarifa za watu kutekwa: Ni kujiteka, wivu wa mapenzi na kugombea mali

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
Jeshi la Polisi limetoa tamko kufuatia taarifa za watu kupotea, kutekwa au kukamatwa na wanaodaiwa kuwa askari. Polisi wamesema hufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuthibitisha ukweli wa tukio, na haiwezi kusemwa moja kwa moja mtu amepotea bila ushahidi.

Kwa mujibu wa sheria, mtu hutambulika kuwa amepotea rasmi baada ya miezi mitano kupita na mahakama kuthibitisha. Jeshi hilo limewahakikishia wananchi kuwa linachukua kwa uzito kila taarifa, huku likitoa wito kwa ndugu wa wahusika kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea.

Aidha, Polisi limeonya kuwa kusambaza taarifa za uongo ni kosa la jinai linaloweza kupelekea faini ya hadi milioni tano au kifungo cha miaka mitano.

FB_IMG_1750251237833.jpg


FB_IMG_1750251241800.jpg

FB_IMG_1750251244617.jpg

FB_IMG_1750251247124.jpg

Tanoo.jpg

Sita.jpg
 
Nimejutahidi kusoma ili nione taarifa za mzee kibao,mdude na wengine ambazo inaaminika waliuawa na polisi hawajazitaja kabisa.Hii inamaanisha wauaji ndiyo hao wanaotaka kutuhadaa ili maovu waliyoyafanya tuyasahau.
 
Mbona mdude taarifa zake hamna!Soka na wengineo chadema hamna!!

Sijaridhika kabisa mimi!!

Nimeumia kama jeshi letu linaweza kutoa taarifa shalow ziki deviate toka Kwa matukio kamili!!

Hivi mzee kibao alijiua kwa wivu wa mapenzi!!?soka alienda nchi za nje!!?

Aiseh!!
 
Eti Shekhe Zuberi Saidi Nkokoo alisingizia kutekwa ili akimbie maden anayodiwa na watu mbalimbali ya jumla ya shilingi 521, 500,000/= !!!!

Hata kama kweli ana madeni, ndio mnataka kutuaminisha hiyo ndio sababu?

Hao watu mbalimbali mnaosema wanamdai na mmehifadhi majina yao, kuna ubaya gani kuwataja kama mdaiwa mmemtaja?

Watanzania sio wajinga.
 
Back
Top Bottom