Yimakatso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 7,060
- 9,468
Waende tu mahakamani wakapindishe ushahidi biashara inaisha mapema kabisa na kesi kufutwa.Wakuu kuna jamaa yangu alipatwa na tatizo wakawa wamempeleka polisi, kule polisi akapata dhamana kwa sababu kosa lake lilikuwa lina dhamana, akaenda kuzungumza na wale waliokuwa wanamshitaki na wakawa wameelewana kuwa mambo yasiendelee mbele zaidi yaani kufika mahakamani.
Sasa changamoto iliyopo ni polisi kukomaa hasa yule mpelelezi aliyepewa jarada (file), kesi kaipeleka mahakamani na bado anamkomalia jamaa afike mahakamani, wanaomshitaki jamaa hawataki kesi wao wanapigiwa simu na polisi za vitisho ili wafike mahakamani, sielewi shida ni nini?[emoji854]
Polisi wanaitafuta kwa nguvu zote aisee.
Huyo mpelelezi anataka rushwa sasa alivyoona jamaa wameyamaliza pasipo yeye kupata chochote ame mind.